FeaturedTHE MUSLIM MASTERMINDS
Trending

MUANZILISHI WA HESABU ZA ALGEBRA

Tukiangalia maisha tunayo ishi leo kupitia Compyuta, simu, kununua vitu online, intaneti, kwenda sehemu kwa kutumia ramani, mitandao ya kijamii instagram, facebook twitter google search nk,Yote hayo yanawezekana kupitia Algorithm

Algorithm ni neno la kilatini linatokana na jina la Mwannahisabati mkubwa wa kiislamu Al-Khawaarizmi. Bila akili ya ajabu ya Mwanahisabati huyu Mwislamu wa karne ya 8 Al-Khawarizmi, ulimwengu wa hesabu leo ​​ungeonekana tofauti sana, Wengine pia humuita Grandfather of Computer Science.

Jina lake kamili ni Muhammad ibn Musa Al-Khawaarizmi. Alizaliwa katika familia ya kiajemi mnamo mwaka 870 katika eneo la Asia ya kati huko nchini Uzbekstan.

Wakati Khalifa A’bbas al-Ma’mun alipoanzisha Nyumba ya Hekma huko Baghdad mwka 832, ijulikanayo kama Baytul Hikma ama House of Wisdom kipindi ambacho Uislamu ulistawi kiutamaduni, kiuchumi na kisayansi, Alkhawarizmi alisoma pia na kufanya kazi zake katika nyumba ya Hekima. Nyumba ya Hekima ikawa ni kituo kikubwa ambacho wasomi wa Kiislamu na wanachuoni walikusanyika, kutafsiri maandishi ya kisayansi, falsafa na kuchapisha utafiti asilia.

BAYTUL HIKMA
Nyumba ya Hekima

Al-Khwarizmi alikuwa mwanahisabati, mnajimu na mwanajiografia, Pengine labda alikuwa mmoja wa wanahisabati wakubwa waliowahi kuishi, kwani alikuwa mwanzilishi wa matawi kadhaa na dhana za kimsingi za hisabati. Katika maneno ya Profesa Hitti aliwahi kusema

Alkahawarizmi Aliathiri fikra za hesabu kwa kakiasi kikubwa zaidi kuliko mwandishi yeyote wa enzi za kati, karene ya 5 mpaka ya 15.

Profesa Phillip Hitti

Al Khawarizmi The Muslim Genius alikamlisha kazi zake nyingi huko nchini baghdad katika nyumba ya Hekma na ndie muanzilishi wa hesabu za Aljebra,

Katika kitabu chake maarufu alichokiita

الكتاب المختصر في حساب الجبر والمقابلة

Katika jina la asili la Kiarabu la kitabu hiki ndipo tinapata neno ALGEBRA

Aljebra linatokana na neo la Kiarabu “al-jabr”, lenye maana ya “muungano wa sehemu zilizovunjika” ni tawi mojawapo la hisabati pamoja na nadharia ya namba, jiometri na uchambuzi.

Hata hivyo ni muhimu kutambua kwamba kitabu hicho kilikusudiwa kuwa cha kivitendo zaidi na kwamba aljebra ilianzishwa ili kutatua matatizo halisi ambayo yalikuwa sehemu ya maisha ya kila siku katika himaya ya Kiislamu wakati huo.

Alkhawarizmi alikuwa akikokotoa sheria za mirathi za Waislamu na kisha akajenga zaidi jiometri ya wagiriki na kuendeleza mawazo ya msingi ambayo wanafunzi wengi wa hesabu wa shule leo wanaweza kutambua.

Kitabu hicho cha kilikusanya utatuzi wa maswala ya kila siku katika maisha kwa wakati huo, kama vile kugawanya ardhi, kulipa wafanyakazi na kugawanya mirathi.

Kitabu hicho baadae kilitafsiriwa kwa kilatini karne ya 12 ambacho leo kinajulikana kama

The Compendious Book on Calculation by Completion and Balancing

Kitabu chake hiki kilileta mapinduzi ya hisabati katika nchi za magharibi, kikionyesha jinsi matatizo magumu yanavyoweza kugawanywa katika sehemu rahisi na kutatuliwa na kutoa mkusanyiko wa sheria pamoja na maonyesho ya kutafuta suluhu za milinganyo ya mstari na ya quadratic kulingana na hoja angavu za kijiometri.

Na baadae karne ya 19 Alogoritms ilkuja kumaanisha seti ya sheria za hatua kwa hatua za kutatua matatizo,

Mwanzo ni mwa Karne ya 20 Alan Turing Mtaalamu wa hesabu wa Uingereza na mwanasayansi wa kompyuta  alijkita kutambua ni ni jinsi gani mashine inaweza kufuata muundo wa Algorithims na kutatua hesabu zilizo ngumu.

Wakati wa vita vya pili vya Dunia Alitengeneza mashine iitwayo Bombe ambayo ilitumia Algorithims kuvunja code za Enigma kifaa cha siri kilichotumiwa na jeshi la Ujerumani kusimba jumbe za kimkakati.

Algorithms ni utaratibu wa maagizo na hutumika takriban katika vifaa vyote vinavyotuzunguka. Kila mara unapobonyeza kitufe au kugusa skrini yako, unakiambia kifaa chako kifanye jambo fulani na jinsi kifaa chako kinavyoitikia maagizo hayo hiyo ni Algorithm.

Kitabu kingine Al-Khwarizmi kilikuwa ni juu ya somo la hesabu, ambacho kopi zake halisi za kiarabu zilipotea na kilidumu katika tafsiri ya Kilatini pekee.

Tafsiri ya Kilatini ya kitabu chake cha hesabu iliratibu nambari mbalimbali za Kihindi na kuanzisha mfumo wa nambari wa nafasi ya desimali kwa ulimwengu wa Magharibi.

Al-Khawarizmi alikubali wazo la kuitambua sifuri kama namba, hili liilifungua ulimwengu mpya kabisa wa uwezekano wa hisabati,

Kwani kutumia mfumo wa zamani wa namba za Kirumi kulifanya hesabu ya hali ya juu isiwezekane, Lakini kwa mfumo wa nambari unao anzia 0 hadi 9 ilikuwa rahisi na al-Khawarizmi aliweza kuendeleza nyanja kama vile aljebra na kumfanya leo hii atambulike kama The Father Of Aljebra – Baba wa Aljebra.

Moja ya kipengele cha msingi cha hisabati ilikuwa ni jinsi ya kuandika nambari, ambapo mifumo kadhaa ilitumika ikiwa ni pamoja na kutumia namba za Kiarabu, pmoja na nambari za Kirumi.

Lakini Al-Khawarizmi alianzisha mfumo tofauti wa nambari ambao leo ndio unatumika Duniani, kuanzia namba 0 mpaka 9. Namba  hizo zinafahamika kama Arabic Numerals. Mfumo huu ni rahisi na wa haraka zaidi katika kufanya mahesabu kuliko mfumo wa namba za Kirumi.

Kwa miaka 700 mbele baada ya kifo chake, wanahisabati wa Ulaya wanamtaja katika kazi zao kama “Algorithms” ambapo inatokana na jina lake Al-Khawarizmi.

Hivyo jamii ifkirie na kuliangalia somo la hesabu kuwa ni msaada mkubwa katika maisha yetu ya kila siku tunayo ishi, na watoto wetu kutambua umuhimu wa hesabu na kuanza kuipenda.

Leo, Uislamu unachukuliwa na kuonyeshwa tofauti, lakini Ulimwengu unasahau kwamba zamani kulikuwa na ustaarabu wa Kiislamu ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa na kusababisha maendeleo makubwa katika sayansi na kurahisisha mfumo wa maisha yetu ya leo.

Unaweza kuisikiliza makal hii pia kupitia

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also
Close
Back to top button