FamiliaFeatured

UMUHIMU WA FAMILIA

Uislamu unaitazama familia kama msingi wa jamii bora. Ni kwa sababu hii, Uislamu unahimiza wanamume na wanawake kuanzisha familia baada ya kufunga ndoa inayokubalika kisheria. Uislamu umerahisisha utekelezaji wa ibada ya ndoa kwa kuondoa vikwazo vya kijamii na kiuchumi vinavyokwamisha mchakato wa kufunga ndoa. Kwa kutambua hatari ya zinaa, Uislamu unapinga mila, desturi na mambo mengine yanayopelekea watu kushindwa kuingia kwenye ndoa, kama vile mwanamke kudai mahari kubwa na gharama zilizopitiliza za maandalizi ya harusi.

Uislamu, pia unapinga ushoga na ndoa za jinsia moja, kwa sababu hayo ni mambo yanayopingana na asili ya mwanadamu. Qur’an inaele-za wazi kuwa kila kitu kimeumbwa (kimetengenezwa) kwa jozi, yaani viwili viwili. Kwa hiyo, jozi ya mwa- namume na mwanamke ni sehemu ya asili ya binadamu. Vigezo vya kuchagua mchumba Uislamu umetoa muongozo kati- ka suala la kutafuta mke mwema.

Katika hadith iliyosimuliwa na Abu Huraira (Allah amridhie), Mtume (rehema za Allah na amani imshukie) amesema:

“Mwanamke huolewa kwa mambo manne: Kwa mali yake, nasaba yake (ukoo), uzuri wake, na dini yake. Tafuta mwenye dini uwe salama (usiharibikiwe katika maisha yako).” [Bukhari na Muslim]. Aidha Mtume amesema: “Akiku- jieni yule ambaye mmeridhika na dini yake na tabia yake muozesh- eni. Msipofanya hivyo kutakuwa na fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa.” [Tirmidhi].

Akiku jieni yule ambaye mmeridhika na dini yake na tabia yake muozesheni. Msipofanya hivyo kutakuwa na fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa. Tirmidhi

Uislamu umerahisisha mchakato wa ndoa ili kuziba na kudhibiti mianya inayopelekea watu kufanya zinaa. Na ndoa imesisitizwa kutoka- na na umuhimu wake katika kuihifadhi jamii na zinaa na kulea watoto katika maadili ya dini. Malengo mengine ya ndoa ni kuleta utulivu wa moyo kati ya mume na mke, kupandikiza map- enzi, huruma na ushirikiano baina yao, kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri, kuweka haki na wajibu baina ya mume na mke, na kukaa pamoja kwa wema. Allah Aliyetukuka anasema:

“Na kaeni nao (wanawake) kwa wema, na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkachukia kitu, na Allah ametia kheri nyingi ndani yake.” [Qur’an, 4:19]

Akasema tena Allah:

“Nao (wanawake) wanayo haki kwa sheria (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia wau- me zao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Allah ni Mwe- nye nguvu (na) Mwenye hekima.” [Qur’an, 2:228]

Kuhusu talaka Uislamu unasisitiza watu kufun-ga ndoa ya kisheria na kuishi kwa wema. Lakini hali halisi inaonesha kwamba baadhi ya nyakati maisha ya ndoa huwa machungu kutokana na wanandoa kugombana au kutofautiana maoni au mitazamo. Kwa kuliona hilo, Uislamu umechagua njia ya kutatua mizozo ya ndoa ili kuchunga maslahi ya pande zote mbili, yaani mume na mke pamoja na maslahi ya watoto. Kwa vile tofauti kati ya mume na mke ni jambo la kimaumbile.

Uislamu unawataka wanandoa kuwa na subira, uvumilivu, kusameheana na kuishi kwa wema. Allah Mtu- kufu anasema:

“Na kaeni nao (wanawake) kwa wema, na kama mki- wachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkachukia kitu, na Allah ametia kheri nyingi ndani yake.” [Qur’an, 4:19].

Endapo itatokea wanandoa kukwaruzana au kutoelewana, Uislamu umeagiza iundwe mahakama ya ukoo ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao. Allah anasema:

“Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume, basi pelek- eni mwamuzi mmoja katika jamaa wa mwanamume na mmoja katika jamaa wa mwanamke. Kama waki- taka mapatano Allah atawawezesha…” [Qur’an, 4:35].

Na endapo suluhu itashindikana, Uislamu umeruhusu mume kumuacha mkewe talaka moja, kwa maana ya talaka rejea. Na inafaa kwa mume kumrejea mkewe aliyempa talaka moja kabla ya kumalizika muda wa eda (kabla ya kupita miezi mitatu au hedhi tatu). Katika kipindi chote cha eda, mke anatakiwa kubaki katika nyumba ya mumewe pasina kufanya tendo la ndoa. Ikitokea wawili hao wamefan-ya tendo la ndoa ndani ya muda wa eda, hapo talaka itakuwa imekatika na mume huyo atakuwa amemrejea mkewe. Na kama muda wa eda umemalizika pasina kurejeana, basi hiyo itakuwa ni talaka ya kutengana kidogo. Wanazuoni wa sheria ya Kiislamu, talaka hii wanaiita ‘Baainata As– Swughraa’.

Related Articles

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button