Projects Department

Msikiti mpya, wa kisasawafunguliwa Tarime

Taasisi ya The Islamic Foun dation imezindua msikiti mpya wa kisasa wilayani Tarime, mkoani Mara uit wao ‘Masjid Othman bin Affaan’ ambao umegharimu takriban shi lingi za Kitanzania milioni 200. Akizungumza katika uzinduzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Mara, Msabaha Kassim, ameisifu taasisi hiyo, hususan Mwenyekiti wake Aref Nahdi, kwa kazi hiyo nzuri ya kuendeleza dini kwa kue neza misikiti. Sheikh Msabaha alimwam bia Nahdi:

“Hakika umeipam ba Tarime …umefanya jam bo kubwa,”

na akakumbusha kuwa kwa mujibu Uislamu, viwanja vilivyo bora ni vile vilivyojengwa misikiti.

Aref Nahdi, mwenyewe, aki zungumza na Waumini katika uzinduzi huo alisema kukami lika kwa msikiti nyongeza katika orodha ndefu ya misikiti zaidi ya 1500 ambayo taasisi ya The Islamic Foundation imejenga tan gu kuanzishwa kwake miaka 24 iliyopita. Katika kipindi hicho taasisi hiyo pia imechimba visima zaidi ya 3 0 0 0 , inalea watoto yatima 953 ambao wenye uwezo wanasomeshwa hadi chuo kikuu na baadhi wakip atiwa kazi katika idara mbalimbali za taasisi hiyo na vilevile inaende sha shule, Mahad za Kiislamu na zahanati,.

Awali, akitoa maelezo kuhusu msikiti uliozinduliwa, Mkurugenzi wa The Islamic Foundation mkoani Mara, Bashir Abdallah alisema mradi wa ujenzi huo ulianza Janu ari 11, 2022 na kukamilika Machi 15, 2023. Bashir alisema takriban milio ni 192 zimetumika katika mradi huo, bila kujumlisha gharama nyingine kadhaa kama za upimaji majengo, mazulia, spika ambapo kwa makadirio ya Gazeti Imaan, vitu hivyo vinaweza kupandisha gharama nzima za ujenzi hadi kufikia Tsh milioni 200. Bashir, katika shukran zake kwa niaba ya Waumini, licha ya kum taja Mwenyekiti Nahdi na vion gozi wengine waandamizi wa The Islamic Foundation, aliwashukuru pia wazee waliofanikisha kupata kiwanja hicho kwa ajili ya msikiti takriban miaka 40 iliyopita.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa The Islamic Foundation, Sheikh Ibrahim Twaha alitoa khutba ya Ijumaa ya uzinduzi akisisitiza umuhimu wa kuutumia msikiti inavyotakiwa, ikiwemo kutekeleza ibada na kusomesha watu dini ili kutengeneza raia wema. Pia, alisisitiza umuhimu wa kuutunza ipasavyo msikiti katika masuala ya usafi. Sheikh Twaha pia alionya dhidi ya tabia ya kuendeleza migogoro katika nyumba za Mwenyezi Mun gu. Pia, alitaka Waumini wakae chonjo dhidi ya watu wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani ya nchi. Awali akiongea katika uzin duzi huo wa msikiti

Mkuu wa Wilaya wa Rorya, Juma Chikoka ambaye pia alikuwa akimuwakili sha mkoa alitoa wito kwa Wais lamu wawaombee viongozi wa nchi ambao wanafanya mambo makubwa ya maendeleo na pia waliombee taifa.

“Mheshimiwa Rais ameende lea kusimamia masuala ya kide mokrasia na pia diplomasia na hivyo uchumi unaendelea kufun guka,”

‘Othman bin Affaan’ jina la msikiti uliozinduliwa ni la Khalifa wa Tatu aliyetawala Dola ya Kiisl amu baada ya kufariki mtangulizi wake, Umar bin Khattwab ambaye naye alimrithi Abubakr as-Swiddiq aliyepokea uongozi kutoka kwa Mtume kutoka kwa Mtume (rehe ma za Allah na amani zimshukie). Radhi za Allah ziwashukie Maswa haba wote hao watukufu.

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button