Biashara na UchumiFeaturedImaan Newspaper

Jenga uchumi wako binafsi

Tumezoea kusikia kuhusu kujenga uchumi wa nchi na kuleta maendeleo. Tunaambiwa kuwa uchumi unakuwa kila mwaka na hivyo maisha ya watu yanaimarika. Hilo linaweza kuwa sahihi iwapo wewe na mimi tunajidhatiti kujenga uchumi wetu binafsi. Abadan, ukuaji huo wa uchu mi hautomnufaisha yule ambaye amekaa maskani asubuhi na jioni akizungumza kuhusu mechi na siasa. Wala ukuaji huo wa uchumi hautomsaidia aliyekaa nyumbani na kutazama filamu mbalimbali au kucheza ‘games’ za kieletroniki na kadhalika. Ili uchumi wako binafsi uimarike lazima kila mmoja wetu ajidhatiti katika mambo matatu yafuatayo muda wote wa uhai wake.

Ajifunze misingi ya elimu ya biashara

Iwe mfanyabiashara au mfan yakazi, elimu ya biashara ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu. Unatakiwa ujue biashara ni nini na inaendeshwaje. Baadhi ya mambo mahsusi kila mmoja wetu anapaswa kuyajua ni pamoja namna ya kuibua mawazo ya kibiashara ambayo yatatatua tatizo la mtu au watu kwa njia ambayo watu hao watakauwa tayari kulipia ili kupata ufumbuzi wako.

Mengine ambayo tunapaswa kuyajua ni namna ya kupata mitaji, namna ya kuuza bidhaa au hudu ma, namna ya kuweka mahesabu, namna ya kuzungumza na wateja, na namna ya kuitangaza biashara. Elimu ya biashara hufunzwa katika shule za sekondari kupi tia somo la commerce (biashara) na book keeping (uwekaji rekodi za biashara). Kwa bahati mbaya, watu wanahiyari ya kuyawacha masomo hayo wanapoingia kidato cha tatu. Kwa maoni yangu, ilipaswa kuwe na somo moja ambalo ni mju muiko wa masomo haya ambalo watu wa arts (sanaa) au science (sayansi) wataendeleya kusoma ili wajipatie ujuzi wa biashara. Somo hili ni muhimu ili kuhakik isha anayemaliza kidato cha nne awe na msingi imara wa kuweza kujiajiri na kujenga uchumi wake na wa familia yake. Uendeshaji biashara wa kimazoea tunaoufan ya kupitia ushauri wa rafiki badala ya kutumia wataalamu hautoshi kukuimarisha kiuchumi. Uzuri ni kwamba, hata ikiwa ulipitwa na masomo hayo, bado hivi sasa katika umri ulionao unao muda wa kusoma maudhui fulani za somo la biashara na kuufanyia kazi. Hatua hizi zitakuweka katika mstari wa kujenga uchumi wako. Soma sana vitabu au sikiza mazungumzo yanayolenga kuku ongozea maarifa katika ufanyaji biashara iwe ya vitu au ya kutoa huduma (mwajiriwa)

Tumia muda wako vizuri

Muda ndiyo rasilimali kubwa aliyopewa mwanadamu, na neema kubwa kabisa ni mtu kuwa na Imani/Tawhid. Kama Muislam ushapewa neema ya Tawhid, kina chofuata ni kutumia rasilimali ya wakati vizuri kwani hakika, waka ti/ muda ndiyo uhai wenyewe. Ukitoka kazini au ukishafunga biashara yako jioni, jiulize mas wali yafuatayo: Kitu gani napaswa kufanya ili kuboresha utenda ji wangu kazini au kuboresha biashara yangu? Watu wengi huwa hawana jawabu la swali hili. Hiyo siyo dosari. Dosari ni kuri dhika kwa kukosa jawabu! Dosari ni kudhani kuwa hamna anayejua jawabu! Dosari ni kujifungia ndani ya fikra zako na ukaacha kutumia mlango wa kutafuta ushauri kutoka kwa wengine. Imesemwa: “Omba ushauri kwa wenye ujuzi, utapata nuru ya maarifa yao.” Hivyo, badala ya kupoteza muda wako wa jioni ukishafunga kazi au mwisho wa wiki, tumia muda huo kujumuika na familia yako na pia kukusanya maarifa mapya ili kuboresha zaidi kazi zako. Hili ni jukumu lako la kila siku ili kujenga uchumi wako.

Weka malengo yako na ujilazimishe kuyatimiza

Ni muhimu uwe na malengo ya kukuza kipato chako kila mwaka iwe kwa kupitia ajira, kulima, kuzalisha au kwa kufanya biashara ambazo zinaboresha maisha ya watu wengine. Tunaishi katika wakati ambao taarifa za watu wengine ni nyingi mno katika magazeti, mitandaoni na mitangazo. Taarifa hizi zinawe za kukupa maarifa na nyingine zinaweza kukutoa katika malengo yako. Hivyo ni muhimu ujilazi mishe kuyafikia malengo yako kila mwaka na usikubali kuon doka katika malengo uliyojiwekea na kuishi katika malengo ya wen gine. Sasa tupo katika mwaka mpya wa Kiislamu, chukua kalamu na karatasi uandike kipato ambacho ungependa ukifikie ifikapo mwisho wa mwaka na nini unapaswa kufanya ili kufikia malengo hayo. Usipofanya hivyo, usilala mike pale gharama za maisha zinapoongezeka na wewe miaka nenda rudi umejifunga katika kip ato cha miaka ya nyuma! Kila siku zinavyoenda unataki wa ujenge uchumi wako au vingi nevyo hali ya kiuchumi itakuwa na changamoto ya kutegemea wengine. Weka malengo na kisha tekeleza peke yako au pamoja na wengine!

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button