FamiliaFeatured

Mambo 7 yanayosababisha watoto kuchukia baba zao

Si mara moja tumesikia na kuona katika jamii mtoto au watoto wanamchukia baba yao. Chuki hii inaweza kuonekana kwa namna mbalimbali, ikiwemo kutomjali kabisa, kumpuuza, kumnyanyapaa, kutowasiliana naye au kutumia lugha mbaya wakati wa kuongea.

Mara chache watoto hufikia hatua hata ya kumtukana baba yao au kumpiga, ingawa hayo ni nadra kutokea na ikiwa hivyo huwa ni dalili ya mtoto mbaya aliyekubuhu katika uovu.

Kwa ujumla, mtoto hapaswi kumchukia baba lakini kadhia hizi, aghlabu, hutokea kwa sababu maalum. Hebu tuone baadhi ya sababu hizi ili wazazi wa kiume tuchukue tahadhari.

1. Ubakhili

Mosi, ubakhili

Wapo wanaume ambao hawajali familia, siyo kwa sababu hawana pesa bali tu wana vpaumbele vingine. Kutoka katika familia za aina hii, utasikia mtoto analalamika kuwa baba yake alikuwa na pesa lakini hakumsommesha au walikua katika mazingira ya tabu, kiasi cha kutelekezwa.

Mtoto aliyepitia madhila ya aina hii, mara nyingi anaweza asisahau na atakuwa na kinyongo na hata kulaumu shida zake zote ni kwa sababu baba haakumjali. Hivyo wakinababa acheni ubakhili kwa familia.

2. Kutokuwaonesha watoto mapenzi

Ukatili na vipigo

Wapo watoto ambao hawana kumbukumbu ya mambo mema waliyofanyiwa na baba zao kwa sababu mazuri yalifunikwa na ukatili, vipigo, mashambulizi, ubabe na kadhalika.

Baadhi ya watu hukumbuka namna kipindi cha utotoni baba alipoingia nyumbani walikimbilia ndani na kujificha kwa kuogopa adhabu na mateso, hata bila sababu.

Kama wewe ni mzazi wa aina hiyo usishangae watoto kukosa mapenzi na wewe.

Kumdhalilisha na kumtesa mama yao

Mama ana hadhi maalumu kwa mtoto. Kwa kulijua hilo, wakinababa makini hawawezi kutesa wake zao wakiwa pamoja kwenye ndoa au baada ya kuachana kwa sababu huo ubaya humfanyii huyo mzazi mwenzako peke yake bali pia watoto.

Unaweza kuhoji mwanaume anamtesaje mwanamke aliyeachana naye? Mara nyingi hili hutokea kwa kutopeleka matumizi ya watoto ikiwa wanaishi na mama au kujaribu kumzuia asiolewe tena.

Kama ambavyo wewe usingependa mama yako anyanyaswe, adhalilishwe, aonewe, ateswe; jua kuwa na wanao vilevile hawataakubali na ukimtesa mama yao wataishi na kinyongo dhidi yako.

Kumbuka wewe mkeo lakini wao ni mama yao. Basi mheshimu kwa sababu yao.

Kutojisikia fahari kwaajili yake

Kumlinganisha na wengine ili kumtweza.

Wazazi wengi hutumia mbinu mbaya ya kimalezi ya kumlinganisha mtoto na wengine kwa nia ya kumkosoa. Wazazi, hususan wakinababa tujue kuwa mbinu hii ni mbaya kwa sababu aghlabu haina tija bali humakatisha tamaa mtoto.

Tujue kuwa Mwenyezi Mungu amemuumba kila mtu kwa namna yake na kumpa vipawa fulani ambavyo wengine hawana. Huyu anaelewa haraka, yule anahitaji muda. Huyu ana akili sana kwenye masomo ya nadharia lakini yule anaelewa haraka kivitendo.

Kama mwanao hajabarikiwa kipaji fulani, mtie moyo afanye vizuri bila kumtia wivu kwa kumtajia wengine. Msome mwanao vema utagundua naye ni mahiri kwenye eneo fulani kuliko wengine. Jivunie kwa hilo kuliko kutaka awe kama fulani.

Kumgombeza mbele za watu.

Hii ni tabia nyingine mbaya ya baadhi ya wazazi wa kiume: kumsema mtoto mbele za watu kwa namna ambayo inamuabisha.

Tabia hii ikishamiri, msishangae mtoto akajenga kinyongo na hasira dhidi ya mzazi wake. Athari ya kumuabisha mtoto hadharani haiishii kwenye kujenga chuki bali aghlabu watoto wa aina hii hupoteza kujiamini mbele za watu.

Mwisho niwaombe wazazi wa kiume muwe waangalifu. Ni haki yenu kuwalea watoto mnavyoona inafaa lakini ni muhimu kutahadhari musiwajengee chuki watoto dhidi yenu katika maeneo haya.

Nazi haishindani na jiwe. Mzazi ni jiwe ambalo mtoto akishidana nalo aghlabu ataharibikiwa lakini hamuoni raha ikiwa watoto watakuwa huku wakiwapenda na kuwakumbuka kwa wema?

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also
Close
Back to top button