Huu ndio mlo unaofaa kwa mgonjwa

Miongoni mwa vipindi vya mpito katika maisha ya mwanadamu ni uzima na ugonjwa, mambo mawili yaliyo nje ya uweza wake wa mwanadamu. Kila mwanadamu katika kipindi fulani cha maisha huumwa, tofauti ni ukubwa wa maradhi na kiwango cha kujitokeza ambapo baadhi huumwa mara kwa mara na wengine mara chache. Chakula ni muhimu kwa kila mtu lakini zaidi kwa mgonjwa kwa sababu kinahitajika kuimarisha kinga za mwili, kujenga na kuupa mwili nguvu na kuzisaidia dawa kufanya kazi vizuri ili mgonjwa apone haraka.

Chakula kwa mgonjwa pia husaidia dawa kufanya kazi vizuri na hivyo humwezesha mgonjwa kupona haraka. Kula vizuri kadhalika kunasaidia kuwezesha mwili uweze kupambana na wadudu wanaosa babisha maradhi. Wagonjwa lazima wale vizuri hata kama hawana nguvu. Miili yao inahi taji virutubisho ili kuwa hai, kupam bana na maradhi na kuziba upotevu wa virutubisho. Virutubisho ambavyo mtu yoyote anahitaji, ikiwemo wag onjwa, ni pamoja na wanga, protini, mafuta, protini, vitamini, nyuzi lishe (dietary fibers) na maji ya kunywa.

Athari ya magonjwa

Mara nyingi maradhi yanamfanya mgonjwa kupoteza hamu ya kula. Maradhi pia yanaongeza mahitaji ya virutubisho mwilini. Maradhi yanasababisha lishe duni (malnutrition) na kuongeza mata tizo zaidi. Kama wagonjwa hawata kula vizuri, mwili utatumia mafuta na misuli ili kupata nishati na viru tubisho. Matokeo yake mgonjwa anapun gua uzito na anakuwa dhaifu zaidi. Pia, kwa kutokula vizuri, kinga ya mgonjwa inadhoofika zaidi na hati maye mwili unashindwa kupambana na maradhi/maambukizi. Kwa kukosa kula vizuri, wagon jwa pia wanapoteza zaidi maji. Hii hutokea zaidi kwa wagonjwa wa tumbo la kuharisha au kipindupindu au homa. Hii ina maana kuwa wag onjwa, licha ya chakula wanahitaji pia kunywa maji safi na salama. Sisi wazima tunaouguza inabidi tuwasadie wagonjwa kula vizuri na kunywa zaidi na mara kwa mara. Kama mgonjwa hasikii njaa, apewe chakula kidogo ila mara kwa mara. Mgonjwa anayeweza kula kiasi kingi, apewe. Mara nyingi wagonjwa wanahitaji vyakula laini kama vile viazi au ndizi zilizopondwa, uji, supu na vyakula vitamu. Mpe mgonjwa maji yaliyochem shwa, juisi iliyotengenezwa vizuri hasa nyumbani, maji ya madafu, supu, uji. Mpe maziwa yaliyochem shwa au maziwa mgando, chai.

Miiko ya vyakula

Kabla ya kuanza kutayarisha chakula cha mgonjwa ni lazima kufahamu ugonjwa wake na kujua miiko ya mlo aliyopewa na daktari kuhusu ugonjwa wake. Kila mgon jwa anahitaji chakula cha aina yake kutokana na hamu aliyonayo au maagizo ya daktari. Wapo wagonjwa wanaozuiwa kuweka chumvi, sukari au mafuta kwenye vyakula vyao. Ni muhimu kufuata maagizo ya daktari bila ya kumhurumia mgonjwa kwani kuvunja maagizo hayo ni sawa na kumuangamiza. Kwa mgonjwa asiyejiweza kula chakula cha kawaida iwe ni kuto kana na kuzidiwa au kwa maelek ezo ya wataalamu wa afya, ni vizuri kumtayarishia kile kitakacho yeyush wa kwa urahisi. Wagonjwa wenye homa kali au homa za matumbo wanahitaji aina hii ya chakula. Pia, chakula cha maji maji ni muhimu kwani mara nyingi mgon jwa hupoteza nguvu na maji kwa wingi. Uji mwepesi, mchuzi, juisi, maziwa na supu nyepesi iwe ya samaki au kuku wa kienyeji ni mifa no ya vyakula muhimu kwa mgonjwa.

Vyakula laini

Chakula cha kawaida, kama vile mgonjwa wa homa, ni vizuri kumta yarishia chakula kitakachoyeyushwa na kutumiwa na mwili kwa urahisi. Pia, chakula cha maji maji ni laz ima kwani wakati mtu akiwa na homa mwili wake hupoteza nguvu na maji kwa wingi sana. Vyakula vya maji maji ni kama vile uji mwepesi, mchuzi, maji ya matunda, maziwa na supu nyepesi kama vile ya nyama nyeupe mfano samaki na kuku hasa wa kienyeji. Ngozi ya kuku ina kiwango kikubwa cha mafuta aina ya lehemu (choles terol), kwa hiyo isiliwe. Vyakula vingine laini vyaweza kuwa viazi vya kuponda na kutia maziwa; papai la kuponda au matunda mengine laini, nyama ya kusaga, samaki laini wa kuchemsha, yai lililopikwa, ugali laini sana na mboga za majani. Kwa mgonjwa aliyefanyiwa operesheni au mama aliyejifungua kwa operesheni au hata kwa njia ya kawaida, chakula chake kiwe laini ili choo kubwa ipatikane kwa urahisi bila kujikakamua. Matunda kama mapapai na mbogamboga kama bamia zinasaidia mgonjwa kupata haja kubwa laini.

Usafi wa chakula cha mgonjwa

Chakula cha mgonjwa kitayar ishwe katika hali ya usafi. Mtu aki wa mgonjwa kinga yake ya mwili dhidi ya vijidudu vya maradhi huwa imedhoofika na ni rahisi kwa mtu huyo kushambuliwa na vijidudu vya ugonjwa mwingine. Chakula kilichotengenezwa katika hali ya uchafu kinaweza kuongeza vijidudu vya maradhi mwilini kwa mgonjwa. Wakati unapopakua chakula cha mgonjwa, pakua kidogo kidogo kutoka katika kila aina ya chakula kwani iwapo utampakulia mgon jwa chakula kingi anaweza kuona uvivu kula na kuamini kuwa hawezi kumaliza.

 

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button