Darsa la wikiFamiliaFeatured

WATOTO WETU SIKU EID

Kutoka kwa Bi. Aisha (Allah amridhie) amesema kuwa Abu bakr (Allah amridhie) aliingia kwake (kwa Aisha) wakiwepo wajakazi wawili wakipiga dufu mbili na wakiimba kuhusu masiku yao huku Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) akiwa ame jifunika na nguo yake. (Abubakr) akawakemea kwa kuwakataza, (lakini) Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) akafunua nguo yake akasema: “Waache ewe Abu bakr. Kwa hakika, haya ni masiku ya Idi [sikukuu].” Wanazuoni wamefafanua kuwa kauli ya Mtume inaonesha kuwa ni jambo la kisheria kuwapa watoto wasaa wa michezo katika siku za Idd, na huwasaidia kuwapa furaha ya nafsi na kuupumzisha mwili. Pia, fursa ya kucheza inadhihirisha kuwa, furaha katika Idd ni katika alama za dini.

Uislamu ni dini inayokwenda sambamba na maumbile. Katika kufanya michezo mbalimbali, kuna kuiburudisha roho na kuuchan gamsha mwili na kurejesha nguvu baada ya uchovu wa ibada. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alimwambia Abdullah bin Amr (Allah amridhie): “Hivi sikukufahamisha kuwa wewe unafunga mchana na unasima ma kisimamo cha usiku?” Akas ema: “Ndiyo ninafanya hivyo ewe Mjumbe wa Allah.” Akamwambia: “Usifanye hivyo. Funga na ufungulie. Simama na ulale kwani hakika kiwiliwili chako kina haki na jicho lako lina haki na mkeo anazo haki zake juu yako.” Alichomaanisha Mtume ni kuwa, si kwamba kila wakati ni ibada bali kuna nyakati za mapumziko, nyakati za kukaa na familia na kuna nyakati za michezo yenye manufaa.

Hata hivyo, miongoni mwa mambo yanayochangia kuharibu na kusababisha mmomonyoko wa maadili ni michezo isiyozinga tia mipaka ya kisheria kimavazi na pia katika michanganyiko ya wanaume na wanawake, ikiwemo uimbaji nyimbo ambazo zimeam batana na ala za miziki. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alisema: “Kutakuja kuwa na watu katika umma wangu wanahalalisha zin aa, kuvaa hariri, pombe na miziki.” [Bukhari]. Kuwakusanya watoto na kuanza kuwapigia ngoma na miziki wakiimba na kucheza ni kuwalea katika malezi mabaya ya kupenda vitu hivi vya haramu na hatimae kuviinga. Ukipita mitaani utakuta maban go ya vijana yakielekeza mipango na maandalizi ya safari za ufuk weni katika sikukuu za Idd zinazo jumuisha vijana wa kiume na wa kike na kutawaliwa na ulevi, miziki na maasi mengine. Kufanya haya ni kuiharibu sura nzima ya sikukuu ya Kiislamu inay opingana na vitendo vyote vyenye kukiuka taratibu za dini. Si jambo jema kuandaa mazingira ya furaha kwa kumuasi Allah Aliyetukuka. Ni jukumu la walezi na wazazi kuhakikisha kuwa familia zao zinasherehekea Idd katika sura inayoonesha utofauti mkubwa kati ya sherehe za Kiislamu na sherehe nyingine.

Kwa upande mwingine, katika sikukuu ya Idd, watu hupenda kuvaa mavazi mapya na mazuri. Hili si jambo baya wala si jambo linalopingana na sharia. Kiuhali sia, Uislamu unatutaka tuvae nguo mpya na nzuri, kadri ya uwezo unavyoturuhusu. Hata hivyo, tatizo lipo katika aina ya mavazi yenyewe tunayoyan unua, hasa upande wa wanawake na watoto. Asilimia kubwa ya mavazi haya hayazingatii vigezo vilivyoainishwa katika shari. Tusi chukulie udogo wa mtoto kama kisingizio cha uhuru wa kumvali sha mavazi ya ajabu. Hii ni hatua ya malezi ambayo inataathira kubwa kwa mustakbali wa mto to. Waswahili wanasema: “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” na “Samaki mkunje angali mbichi”. Tuhakikishe kuwa wake zetu na mabinti zetu wanavaa mavazi ya stara ili tupate rehema za Allah

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button