Mume Bora
Wino mwingi sana umemwagwa, na nguvu kubwa imetumika katika kuainisha nafasi ya wanawake Waislamu, haki za wanawake Waislamu, majukumu ya wanawake Waislamu, na nini kinamjenga mke bora Muislamu. Pengine ni kwa sababu kuna ufahamu mdogo kuhusu majukumu ya wanawake, kwa hiyo tunatoa msisitizo maalumu kupitia mihadhara, vitabu na mada mbalimbali. Lakini, kwa kuwa wanaume na wanawake wanategemeana, basi siyo busara sana kuweka msisiti zo kwa mmoja na kubaki kimya kwa mwingine. Wanaume wengi wanaonekana kuhisi kwamba wanawake, na hususan wake zao, ndiyo wanaopaswa kuwa Waislamu bora, wakati wao wenyewe na wanaume wenzao, wanafanya vile wanavyotaka bila ya kurejea Qur’an na Sunna.
Makala hii inakusudia kuweka mizania sawa, yaani kuelekeza kurunzi kwa wanaume, ili nao wawe na ufahamu kuhusu viwango vya Kiislamu kuhusu mume bora, na wajitahidi kufikia viwango hivyo kama wanavyo taka wake zao wafikie viwango vya mke bora Muislamu. Mahali pawazi pa kuangalia viwango hivi vya tabia na mwenendo bila ya shaka ni ndani ya Qur’an na Hadith. Kwa hiyo, tuanzie mwanzo. Je? Mume bora anafanyaje kab la ya ndoa? Sote tunafahamu, mwanaume huwa habadili tabia yake yote kuanzia siku yake ya ndoa. Bibi harusi anaunganisha maisha yake na ya mtu mwingine, ambaye haiba na tabia zake kwa kiwango fulani zinakuwa tayari zimeundwa. Kwa hiyo tabia ya kijana ina paswa kuwaje kwa wanawake kabla ya ndoa? Uislamu hauku bali mtazamo wa kawaida katika jamii za kisekula za ulimwengu wa Magharibi kwamba kabla ya ndoa kijana anatarajiwa “kufanya majaribio” kwa kuhangaika na makahaba wanaojiuza au kuwa na marafiki wa kike.
Kwa shughuli kama hizo, Qur’an imeweka adhabu ya kisheria ya bakora 100: “Mzinifu mwa namke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushik eni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwe nyezi Mungu na Siku ya Mwisho” [Qur’an, 24:2]. Na Qur’an Tukufu imeeleza zaidi, “Na wajizuilie na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake…” [Qur’an, 24:33].
Kuwasaidia vijana katika hali hii Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) katika Hadith iliyorekodiwa katika Bukhari ameshauri zaidi, “Vijana, wale miongoni mwenu wanaoweza kumudu mke anapaswa kuoa, hiyo itawaepusha na kuwaanga lia wanawake na kuhifadhi usafi wenu, lakini wale wasioweza wanapaswa kufunga, kwani hiyo ni njia ya kupoza matamanio” Kwa wale waliokuwa na uwezo wa kuoa, vipi wanapaswa kulien dea jambo hilo? Tumetaja kwamba vitendo viovu vya kuwa na marafiki wa kike na “ndoa za majaribio” ni kinyume cha sheria kwa Waislamu. Badala yake inatarajiwa kwamba familia na marafiki watabeba jukumu la kufuatilia tabia na mazingira ya anayetaka kuoa au kuolewa kabla ya kuruhusu ndoa kufungwa.
Kijana anatarajiwa kuwashiriki sha wazazi wake baadhi ya vipaumbele katika aina ya msi chana anayetarajia kumuoa na hili linatajwa kwenye Hadithi iliyo simuliwa na Abu Huraira ambapo Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) ameshauri: “Mwanamke anaweza kuolewa kwa sababu ya utajiri wake, famil ia yake, uzuri wake au dini yake. Lakini angalieni zaidi dini yake..” [Bukhari na Muslim]. Kwa maneno mengine msingi wa mafanikio katika ndoa una onekana kama ubora wa maadili ya mwenza. Bwana harusi bora Muislamu, kwa hiyo, anaingia kwenye ndoa akiwa na mtazamo wa mtu anayeanzisha familia juu ya msingi bora wa mapenzi na kuhurumiana, na siyo kupenda urembo, tamaa ya mali au hadhi ya kijamii. Qur’an imeueleza uhusiano wa ndoa kwa maneno haya: “Na katika Ishara zake ni kuwa ame kuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri.” [Qur’an, 30:21]. Na Qur’an imeeleza tena, “Wao (wake) ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.” [Qur’an, 2:187].
Majukumu ya Mume
Sasa baada ya kutafuta mchumba wake kwa njia ya heshima, na kumuoa katika utaratibu ulioagizwa na Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie), yaani bila ya fujo wala kujionyesha – nini majukumu ya mume Muislamu? Jukumu lake la kwanza ni kum tunza mke na kumlinda, na maju kumu mengine yote ya jumla kwa ajili ya ustawi wa mke wake, ambayo yameelezwa ndani ya Qur’an: “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayoyatoa.” [Qur’an, 4:34]. Hii inajumuisha kumlisha, kum visha na kumpatia makazi mke na watoto iwapo watapatikana kutokana na ndoa hii. Hili ni juku mu la kisheria, ambalo linabaki hivyo hata baada ya talaka mpa ka kukamilika kwa kipindi cha ‘Iddah’ au muda mrefu zaidi kwa mtazamo wa baadhi ya wana zuoni. Jukumu la kifedha kwa ajili ya kuhudumia familia ni la mume, na mke hana wajibu wa kuch angia gharama za uendeshaji wa familia, labda awe na uwezo na nia ya kufanya hivyo.
Wajibu wa kisheria wa mume haukomei tu kuhudumia famil ia kwa mahitaji yake ya msingi, kumtunza mke na kumlinda. Ana tarajiwa pia kuwa naye karibu na kumpa haki zake za ndoa, na kuepuka kufanya kitu cho chote ambacho kitamdhuru au kumuumiza. Utekelezaji wa majukumu haya ya mume unasimamiwa na Sha riah. Iwapo mume atashindwa kumtunza mke au atashindwa kumtembelea kwa zaidi ya kip indi fulani, bila ya kuwepo sababu zinazokubalika kisheria, basi mke ana haki ya kupewa talaka yake na Mahakama ya Shariah. Halikadhalika, iwapo mke huyu atathibitisha mahakamani kwamba mume wake anajidhuru, iwe kwa kunywa pombe, kuvuta dawa za kulevya, au kumpiga bila ya sababu, au kumdhalilisha yeye na wazazi wake na mambo men gine kama hayo, basi anastahili kupewa talaka yake. Katika nukta zote hizo zilizota jwa hapo juu, mume haruhusiwi kamwe kudai chochote katika mahari au zawadi alizompa mkewe. Ningependa kuweka angalizo hapo kwamba kila hali lazima ifanyiwe tathmini kulinga na na uhalali wake na mazingira yake.