
Israel yageuza hospitali Gaza uwanja wa vita huku dunia ikiangalia
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, amelaumu kushindwa kuchukuliwa hatua kusimamisha janga la haki za binadamu linaloedelea huko Gaza kupitia mashambulizi ya Israel dhidi ya hospitali.
Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Türk amesema uharibifu wa hospitali kote Gaza unawanyima Wapalestina haki yao ya kupata huduma za afya zinazofaa. Aidha alisema vituo hivyo pia hutoa mahala salama kwa watu ambao hawana mahali pen-gine pa kukimbilia.
Akitoa mfano wa matukio ya karibuni, Türk alitaja uharibifu wa hospitali ya Kamal Adwan ambayo ni ya mwisho kufanya kazi eneo la Gaza Kaskazini . “Baadhi ya wafanyakazi na wagonjwa wali-lazimika kutoka hospitalini huku wengine, akiwemo Mkurugenzi Mkuu, wakiwekwa kizuizini, kukiwa na taarifa nyingi za kuteswa na kunyanyaswa.”
Nalo Shirika la Afya Duniani kupitia mwakil-ishi wake Dkt. Rik Peeperkorn, mwakilishi wake katika eneo la Ukingo wa Magharibi na Gaza, imetoa angalizo juu ya janga baya la kiafya huko Gaza, ambapo asilimia saba ya watu wameuawa au kujeruhiwa tangu Okto-ba 2023. “Mwaka 2025 unaanza kwa hali ya huzuni na wasiwasi mkubwa huku mapigano yakiendelea kushika kasi,” alisema.
Dkt. Peeperkorn alionya kwamba uhamish-aji muhimu kwa ajili ya matibabu unafanyika polepole sana, na zaidi ya watu 12,000 bado wanasubiri matibabu nje ya nchi. “Kwa kiwango cha sasa, itachukua miaka mitano hadi 10 kuwahamisha wagonjwa hawa wote walio mahututi,” alibainisha. WHO imethibitisha mashambulizi 654 kwenye vituo vya afya tangu vita ianze Oktoba 2023 na kusababisha mamia ya vifo na maje-ruhi.