
Kiingereza bado pasua kichwa kidato cha Pili
Kiingereza ambayo ndiyo lugha ya kuji-funzia kwa wanafunzi wa sekondari imeendelea kuwa mwiba, baada ya robo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa majaribio wa kidato cha pili mwaka 2024 kupata alama F.
Jambo hilo linatajwa kuwa moja ya sababu ya wanafunzi wengi kupata F katika masomo mengine kutokana na kushindwa kuelewa lugha inayotumika katika kufundishia na kujibia mitihani, huku wakitaka tathmini ya kina kufanyika kujua lugha gani inafaa katika kufundishia.
Matokeo ya mitihani ya upimaji yaliyo-tolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (Nec-ta) Januari 4, 2025 yanaonyesha wanafunzi 202,448 kati ya 796,413 waliofanya mtihani wa Kiingereza walipata daraja F katika somo hilo huku 288,858 wakipata daraja D. Hiyo ikiwa na maana kuwa ni asilimia 38.31 pekee ya wanafunzi ndiyo waliweza kupata daraja A hadi C ambayo kwa idadi yao ni 305,107.
Hiyo ni tofauti na somo la Kiswahili amba-po ni asilimia 8.26 pekee ya wanafunzi ndiyo walipata daraja F. Waliopata A hadi C katika somo hilo ni asilimia 63.2 zaidi ya waliokuwa na wastani huu katika somo la Kiingereza kwani walikuwa 498,003.
Nini maana yake
“Siyo tu wamefeli Kiingereza, inaonyesha hawana uelewa wa kutosha kusoma masomo yao ya sekondari kwa lugha ya Kiingereza,” alisema mwalimu Richard Mabala ambaye ni mdau wa elimu.
Alisema matokeo haya yanaonyesha ni kwa namna gani wanaofaidika na Kiinger-eza kinachotumika katika kufundisha ni wale waliosoma shule za michepuo ya Kiinger-eza kwa sababu kimekuwa kikitumika kwao tangu awali.
“Ili tufanikiwe katika hili labda tufanye shule zote ziwe za Kiingereza lakini hai-wezekani kufanya hivyo kwa sababu hatuna walimu wa kutosha kufundisha lugha hiyo kama somo,” alisema. Alisema umefika wakati sasa wa kufanyika kwa majaribio ili kuruhusu Kiswahili kutu-mika hata kwa nusu ya shule nchini, ili kujua kama waliofeli mitihani ilikuwa ni kushindwa kuelewa lugha au masomo.
“Tufanye kitu kuonyesha Kiingereza haki-wezekani na matokeo haya tunayaona ni ya wanafunzi ambao walipewa wiki sita za mwanzo kujifunza Kiingereza, lakini haileti mabadiliko makubwa.” “Basi kama hatuwezi kubadilisha tutafute shule za mfano tugawanye, ndani ya shule moja nusu wajifunze Kiswahili nusu Kiin-gereza na wafanye mtihani tuone matokeo,” alisema.
Katika hatua nyingine, Mabala alisema suala la Kiingereza kuendelea kuwa lugha ya kufundishia ni mwiba, huku akieleza kuna wakati ambao aliwahi kusikia kuwa walimu wa shule ya msingi walipewa mtihani wa Kiingereza na wengi walifeli lakini walipope-wa mtihani huo kwa Kiswahili walifaulu.Ali-tumia nafasi hiyo kuitaka wizara ya elimu au taasisi za elimu wafanye hizi tafiti ili waone kama kuna tofauti.
Siyo kilio cha leo
Hili linasemwa wakati ambao kwa nyakati tofauti kumewahi kuwa na mvutano kati ya wadau mbalimbali wa elimu na Serikali kuta-ka lugha ya kufundishia shule za umma kuwa Kiswahili badala ya Kiingereza kinachotu-mika sasa. Hiyo ni kutokana na wao kueleza ni ngu-mu kwa wanafunzi waliosoma Kiswahili kwa miaka saba kuhamia ghafla kujifunza maso-mo yote kwa Kiingereza wanapoingia kidato cha kwanza.
Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa majadiliano hayo, Serikali ilisisitiza kuwa Kiingereza kitaendelea kuwa lugha ya kujif-unzia katika shule za sekondari huku ikitafu-ta namna ya kuwaandaa wanafunzi kumudu lugha hiyo kabla ya kuanza masomo rasmi wanapojiunga kidato cha kwanza.