Rais Mwinyi asifu ukuaji utalii wa maadili
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema dhana ya utalii wa maadili inaendelea kukua zaidi kufuatia ujio wa viongozi mbalimbali wa kiimani nchini.
Rais Dkt Mwinyi alitoa kauli hiyo katika mazungumza na mlinganiaji wa dini ya Kiislamu, Dkt Zakir Naik wa taasisi ya Putrajaya ya Malaysia na ujumbe wake waliofika Ikulu kuonana naye
Dkt Mwinyi alieleza kuwa Zanzibar imekuwa na fursa kubwa ya kuendeleza utalii na ajira kwa vijana kufuatia utekelezaji wa dhana hiyo ya utalii wa maadili iliyokubalika na jamii
Mwinyi pia kipekee, alimkaribisha na kumsisitizia mwanazuoni atembelee maeneo zaidi ya kihistoria yaliyopo nchini na kuwa balozi wa kuitangaza Zanzibar kimataifa.
Aidha Dkt Mwinyi alimshauri Dkt Naik kufikiria kuitembelea Zanzibar kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kufanya mihadhara kwa Waislamu na Watanzania kwa ujumla ili kukuza uelewa wa dini. Kwa upande wake, Dkt Zakir Naik ambaye hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuizuru Zanzibar akiwa ameambatana na mwanawe Sheikh Fariq Zakir, amesifu maendeleo yaliyofikiwa nchini pamoja na muendelezo Mzuri wa harakati za dini ya Kiislamu hapa nchini na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha.