MHADHIRI wa Kimataifa Sheikh Fariq Naik amesema kuwa ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali ya duniani ni wajibu kwa jamii ya Kiislam kurudi kwa ALLAH SW akiwa ni pamoja kufanya ibada za usiku Qiyaam al-layl
Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislam katika msikiti wa Jamia Zinjibar Zanzibar,Sheikh Fariq Naik amesema kuwa miongoni mwa njia bora ya kuweza kutatua matatizo hapa duniani na kesho akhera ni kuamka kufanya ibada nyakati za usiku
Ameongeza kuwa ili kupata nguvu na umoja katika umma wa Kiislam ni wajibu kurudi katika muongozo wa Mtume Muhammad SAW
Sanjari na hilo amewataka viongozi wa familia kuwa imara kwa kuwasiamia wale wanaowaongoza kuamka kwaajili ya Qiyaam al-layl kwani njia nzuri ya mafaniko pamoja na kuwalinda kutokana na maovu
Sheikh Fariq Naik ambae ni mtoto wa Mhadhiri wa Kimataifa Dakta Zakir Naik ameongeza kuwa swala za usiku ni sehemu nzuri kufutiwa madhambi ya mwanadamu
Mhadhiri huyo wa Kiamtaifa anatarajiwa kutoa mhadhara mwingine katika ukumbi wa Diamond Jubilee Januari 2,2025
Kongamano hilo kutoka kwa wahadhiri hao wa Kimataifa limeadaliwa na Taasisi ya The Islamic Foundation kwa ksuhirikiana na Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar,huku pia likiwa limefuatiliwa na mamilioni ya waislam kupitia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo Radio na Tv Imaan ambavyo vilikuwa vikirusha matangazo yake moja kwa moja (LIVE)
Imehaririwa na Mrisho Salum Tozo