Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amewataka waislam wa visiwa hivyo kujikokeza kwa wingi kuweza kusikiliza na kujifunza masuala mbalimbali ya dini tukufu ya Kiislam kutoka kwa Mhadhiri wa Kimataifa Dr Zakir Naik
Sheikh Wadi ametoa kauli hiyo wakati wa mapongezi ya Mhadhiri huyo wa Kimataifa Dakta Zakir pamoja Sheikh Fariq Naik katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,ambapo amesema kuwa katika muhadhara huu jamii ya watanzania wataweza kujifunza masuala mbalimbali
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa ujio wa Dr Zakir ni faraja kwa waislam na wasiokuwa waislam wa Tanzania
Mwenyekiti Aref amesema kuwa licha ya ratiba ngumu ya mhadhiri huyo,amekubali kufika nchini Tanzania kwaajili kufikisha elimu iliyojaaliwa ikiwa ni pamoja na kuhimiza umuhimu wa amani
Nae Dr Zakir Naik amesema kuwa katika mihadhara hiyo atwaeza kutoa mada mbalimbali kuanzia hapo Zanzibar na baadae katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam Januari 2,2025 kuanzia saa 12 jioni hadi saa 5 usiku huku mhadhara wa Mwisho ukiutoa katika uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa January 5,2025 kuanzia majiara ya saa 12 asubuhi hadi saa 7 adhuhuri