
Wekezeni katika makuzi bora ya watoto
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameitaka jamii kuhakikisha kwamba wanafanya juhudi kubwa za kuwekeza kwenye makuzi na malezi bora kwa watoto ili kuepuka taifa kuaribikiwa na vijana kimaadili.
Mhe. Othman ameyeyasema hayo huko msikiti wa Ijumaa uliopo Mtegani Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja alipowasalimia waumini wa Kiislamu baada ya kukamilisha ibada ya swala ya Ijumaa alipoungana nao kwenye msikiti huo.
Amesema kwamba jamii ya Wazanzibari hivi inaendelea kuelekea kuharibikiwa kimaadili kwa kuwa vijana wengi wanafuata na kuiga mila za kigeni jambo ambalo linachangiwa na wazazi kutokujitadi katika kuwekeza kwenye ulezi bora na makuzi sahihi kwa watoto ndani ya jamii.
Amefahamisha kwamba imani na uislam kwa wazanzibari inaharibika kutokana na jamii na hasa wazazi kukosa kuwekeza vyema kwa vijana ambao ndio wanaokuja baadae na kwamba iwapo akukuzwa na maadili mema itokuwa vikumu kujakuyapata baadae.
Amesema ni vyema kwa jamii kuendelea kujikita katika mambo ya maadili mema na kuyapanga sasa kwa kuwalea vyema vijana ili Zanzibar iweze kuendelea na historia njema ya hulka na maadili bora ya uislamu ambapo hata wagezi waliotembelea Zanzibar waliijua Zanzibar ni nchi tukufu iliyogubikwa na tabia na akhalaki njema za uislamu .
Amefahamisha kwamba hata watawala wa kikoloni waliweza kubariki taratibu na kuiridhia baadhi mila na kufuata na kushiriki katika kulinda mila za wazanzibari na pia wakapitisha sheria za kulinda mila ikiwemo ya kuzuia pombe kali.

Aida alisema kwamba katika kumbukumbu za kihistori zinaonesha kuwepo kesi maarufu kati ya Mjerumani na Muingereza ambao ulikuwa mgogoro wa ardhi iliweza kuamuliwa kwa kutumia sheria za kiislamu ambayo ndio iliyokuwa sheria mama ya Zanzibar na wote waliridhia kutumika kwa sheria hiyo kwa kuwa wazanzibari wenyewe ndio walitumia na kujengeka kwa maadili ya sheria hizo.
Naye Khatib wa Swala ya Ijumaa Sheikh Haroub Sose amewataka waislamu na jamii kwa jumla nchini kuacha kufanya mambo maovu na kuiheshimu miezi minne mitukufu ya mfunguo pili, tatu na mfunguo nne na mwezi huu wa Rajab kutokana na kuwa na matukio muhimu ya uislamu.
Mapema Mhe. Othman aliungana na waumini, ndugu, jamaa na wanafamilia kuzuru makaburi ya baadhi ya, Masheikh, wanazuoni na watu mashuhuri huko Makunduchi kuwaombea dua akiwemo Sheikh Idrissa Abdulwakili, Sheikh Hassan Bin Ameir, Shekh Ali Haji Pandu na Sheikh Mamoud Kombo.
Mwisho
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo Ijumaa Januari 17, 2025.