Habari

Ujumbe wa Dkt. Naik kwa walimwengu

Mhubiri na mlinganiaji maarufu wa dini ya Kiislamu duniani, Dkt. Zakir Abdul Karim Naik amewakumbusha Waislamu na watu wa dini nyingine kutambua kuwa wameletwa duniani kwa ajili ya kumuabudu Allah na si kufanya starehe na kutafuta maisha mazuri ya dunia.

Akitoa mada kwenye Kongamano la Kimataifa la Amani katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Dkt. Naik alisema, binadamu wote, bila kujali wanaishi nchi gani wameamrishwa kumuabudu Mola Mmoja (Allah) kama ilivyoelekezwa katika vitabu vitakatifu.

Katika mazungumzo yake yaliyochukua takribani saa tatu, Dkt. Naik alinukuu aya ya Qur’an inayosema:
Nasi hatukukutuma (Muhammad) ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote,
na kusisitiza kuwa Allah hajaleta dini ya Kiislamu kwa waarabu peke yao bali kwa watu wote duniani.

Kwa sababu hiyo, Dkt Naik alisema inapasa watu wote kufuata Uislamu kwa kuwa ndiyo dini aliyoelekeza Mwenyezi Mungu wanadamu wote kuifuata.

Alisema kuwa Mtume Muhammad (rehema na amani imshukie) na Yesu (Nabii Isa – amani ya Allah iwe juu yake), wote wamekuja kulingania dini moja lakini wametofautiana katika sheria za kawaida.

Katika kutilia nguvu hoja yake, Dkt. Naik alinukuu baadhi ya ibara zilizopo kwenye biblia, ikiwemo ile ya kwenye kitabu cha Mathayo 15:24 inayosema:
Hakika mimi (Yesu) nimetumwa kwa ajili ya kondoo (wana) wa Israel waliopotea.

Vilevile, Dkt Naik alinukuu kwenye kitabu cha Yohana ambapo Yesu amesema:
Sitozungumza isipokuwa kile ambacho nimeambiwa na mwenyewe (baba mungu), na nitahukumu kwa kile ambacho amenipa yeye.

Dkt. Naik amesema, kwa mujibu wa maandiko hayo inamaanisha kuwa, Yesu (Nabii Isa) hakuwa na hukumu zake binafsi bali hukumu alizokuwa akizitoa ni zile alizopewa na Mungu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button