
Taasisi ya The Islamic Foundation Kuimarisha ushirikiano na shule ya sekondari ya Kiislam ya Kirinjiko
MWENYEKITI wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa Taasisi hiyo ipo tayari kushirikiana na Shule ya sekondari ya Kiislam Kirinjiko iliyopo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro katika kutatua changamoto mbalimbali zinawakabili
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mkurugenzi wa Utawala wa Taasisi ya The Islamic Foundation Arafat Badru amesema kuwa watahakikisha wanakwenda kuimarisha ushirikiano ili kuwezesha shule hiyo kufikia malengo yaliyokusudiwa
Arafat amebainisha hayo wakati akizindua wiki ya maadhimisho ya miaka 25 ya Kirinjiko Islamic pamoja na nembo rasmi ya maadhimisho hayo hafla iliyofanyika katika shule hiyo iliyopo Same Mkoani Kilimanjaro
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kituo Cha Kiislam Cha Kirinjiko Mfaume Kihongosi amesema kuwa miongoni mwa mahaitajio ya Kituo hicho ni Maktaba ya Kisasa pamoja na kisima kirefu cha maji
Akizungumzia lengo la shule hiyo Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kiislam ya Kiriinjiko Mwalimu Mohammed Makimu amesema kuwa ni kuwaanda vijana wenye maadili mema huku pia akisema kuwa takribani wanafunzi elfu 4 wameshahihitimu katika shule hiyo kwa kindi cha miaka 25










