
KAMBI YA MATIBABU YA MACHO BILA MALIPO
Kambi ya Matibabu ya Macho Bila Malipo iliyoanza tarehe 15 Juni na kuendelea hadi leo tarehe 18 Juni imeandaliwa na The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Mercy Outreach Global.
Kambi hii inafanyika katika Zahanati ya Al Jamii for Mothers and Child Care iliyopo Msamvu, Morogoro, ambapo wananchi wameendelea kunufaika na huduma za uchunguzi, Upasuaji wa Mtoto wa jicho, ushauri na matibabu ya macho kutoka kwa madaktari bingwa.





















