Bi Farhat Naik kudarasisha wanawake UDSM
Ustadhat Farhat Naik naye atakuwa bize na shughuli za kidaawah kama ilivyo kwa mumewe na Dkt Zakir Naik na mwanawe sheikh Fariq Naik.
Bi Farhat ambaye anakuja nchini akiwa ni sehemu ya ujumbe wa mumewe, Dkt Naik, anatarajiwa kuhudhurisha mada katika kongamano kwa ajili ya wanawake wenzake litakalofanyika katika ukumbi wa New Library uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) siku ya Januari 4, 2025.
Dkt Naik na ujumbe wake watakuwa nchini kwa takriban wiki moja kwa ajili ya Kongamano la Amani linalojumuisha mfululizo wa mihadhara ya wazi Zanzibar na Tanzania Bara, miwili kati ya hiyo bi Farhat.
Ukiacha mhadhara wa Dar es Salaam wa Januari 4, bi Farhat pia atafanya mhadhara Zanzibar siku ya mwaka mpya katika Ukumbi wa Mkutano wa Sheikh Idris Abdulwakil uliopo Kikwajuni kisiwa cha Unguja ambapo anatarajiwa kutoa hamasa kwa wanawake kushikamana na dini yao na kujibu maswali mbalimbali.
Mmoja wa waratibu wa ziara ya wageni hao na kongamano hilo la amani kutoka taasisi ya The Islamic Foundation Limbanga Mohammed amethibitisha kuwepo kwa kongamano hilo la wanawake linaloanza asubuhi.
Injinia Limbanga amesema wakati Ustadhaat Farhat anazungumza na wanawake katika ukumbi huo, mumewe Dkt Naik atakuwa na ratiba ya kuonana na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali.
Katika ziara hiyo mbali na kulingania pia wanatarajiwa kutembelea maeneo yenye vivutio vya utalii, hasa Zanzibar, kabla ya kukamilisha ziara yao Januari 6, 2025 na kurejea makwao