Habari

AMYC wakutana kujipanga upya katika da’awah

TAASISI ya Ansaar Muslim Youth Center yenye makao yake makuu jijini Tanga imefanya mkutano mkuu wa mwaka 2024 ili kutathmini maazimio na maagizo ya mkutano mkuu wa dharura wa mwaka 2022.

Mkutano huo umekutanisha mamudir, manaib mudir kutoka majimbo mbalimbali yaliyo chini ya taasisi hiyo kwa ajili ya kujadili, kuboresha na kutoka na maazimio ya kuendeleza harakati za kuipeleka dini.

Akihutubia mkutano huo, Mudir wa taasisi hiyo, sheikh Salim Barahiyan aliwataka viongozi waliohudhuria mkutano huo kujitoa kwa hali na mali na kuwa na utaratibu wa kuhudhuria mikutano mikuu ili kushauriana katika mambo yenye maslahi mapana na Uislamu.

Naye Naibu Mudir, sheikh Ally Nassoro alisema kuwa ni matarajio yao kuwa maazimio yote waliyokubaliana yatakwenda kuleta tija katika kwa jamii inayo wazunguka wao wenyewe na wengine kwa ujumla. Huu ni mkutano wa 28 wa mwaka 2024 wa taasisi ya Ansaar Muslim Youth Center yenye majimbo 17 yanayosimamia idara tano zikiwemo elimu, ustawi wa afya, habari na uenezi, uchumi na da’awah huku pia ikiwa na matawi 609 kwa Tanzania bara na visiwani.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button