Events

BRELA Yafuturu na watoto yatima na kuwapa zawadi ya Idi

KATIKA kuhakikisha watoto waishio katika mazingira magumu wanaondokana na changamoto ya futari pamoja na daku  katika Kipindi hichi Cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  imetoa msaada wa bidhaa mbalimbali katika kituo cha kulea watoto Yatima cha TUYATA cha Kilichopo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya futari ya pamoja na kuwakabidhi msaada Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema kundi hilo limesaulika wakati huu wa mwezi mtukufu wa ramadhani kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwafuturisha wasiokuwa na uhitaji na kuwasahau wenye uhitaji ndio maana wao wakenda kwa watoto hao

Aidha wakala huo umetoa Magodoro ili kuhakikisha watoto hao wanalala katika maeneo mazuri hali ambayo itawafanya kutojioana wanyonge

Sanjari na hilo BRELA Itawalipia watoto 100 safari ya kwenda Dodoma kwa kutumia Treni ya Kisasa ya SGR ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dakta Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule ameipongeza BRELA kwa kujitoa kwao kwani pia wameweza kutoa chakula ambacho kitawatosha watoto hao hadi katika sikukuu ya Eid el fitri ambayo inatarajiwa kuwa mapema wiki ijayo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button