
Events
Wasomesheni watoto Qur’an- wito
Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wao madrasa ili waweze kupata mafundisho ya dini, kuijua Qur’an pamoja na kumjua Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa na Sheikh wa Kata ya Makongo iiliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Abdallah Swalehe katika maonyesho ya kusoma hadith yaliyoandaliwa na Madrasa Swabrul Imaan iliyopo mtaa wa Kibululu Kata ya Goba jijini Dar es Salaam.