Events

Diwani Michael ataka watoto kupelekwa madrasa

Katika kuhakikisha jamii inaendelea kuwa na maadili mema, wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto shule za Kiislamu, ikiwemo madrasa.

Hayo yalisemwa na Diwani wa Kata ya Mbagala, Michael Makwega katika mahafali ya tano ya awali katika shule ya Mbagala Islamic yaliyoandaliwa na City Forest Day Care.

Diwani huyo alisema hatua hiyo ya kupeleka watoto shule zinazofundisha maadili mema zitasaidia taifa kuzalisha viongozi bora. Naye Sheikh wa Kata ya Mbagala, Mohamed Salum, amehimiza umuhimu wa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia. Pia alihimiza walimu kuweka shuleni kwa ajili ya watoto vyakula ambavyo havitahatarisha afya zao.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button