AJIRA 50,000 ZA MOJA KWA MOJA NA 150,000 ZISIZO ZA MOJAKWA MOJA KUZALISHWA KUPITIA KONGANI YA VIWANDA KWALA

Juhudi hizi za Rais Samia za kuweka mazingira wezeshi kwa sekta
binafsi kuwekeza katika miradi mikubwa kama hii inalenga
kutibu tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana wa kitanzania
katika mradi huu utakapo kamilika. Kulingana na wachambuzi
wa Uchumi nchini, mradi huu ni mkubwa kuliko wote eneo la
Afrika Mashariki na Kati na ni mkakati wa msingi uliowezeshwa
na sera nzuri ya Uchumi wa Rais Samia wa kutambua nafasi ya
sekta binafsi katika kuwaletea wananchi maendeleo zaidi na
upatikanaji wa fursa za ajira. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali
uwepo wa mradi huu utaongeza ufanisi katika usafirishaji wa
mizigo hasa kwa mataifa haya ya Afrika Mashariki na Kati
ambapo kitakwimu nchi zaidi ya 10 zitanufaika moja kwa moja.
Kongani ya Kwala inatarajiwa kuwa kitovu cha viwanda
vinavyoongeza thamani ya mazao ya ndani kama pamba,
choroko, maziwa na samaki, hatua itakayoongeza kipato cha
wakulima na wavuvi na kukuza ajira.