RAIS SAMIA AMEKUJA NA MKAKATI WA KUPUNGUZAMSONGAMANO WA MALORI, UHARIBIFU WA BARABARA.

Hii ina maana kuwa treni za SGR zinazofanya safari 5 kwa siku
kati ya Dar es salaam na Dodoma zinaweza kupunguza wastani
wa malori 500 hadi 1,000 yanayotumia Barabara ya Dar es
Salaam na Dodoma. Kwa hakika Kupungua kwa malori haya ni
hatua muhimu katika kupunguza msongamano uliokithiri
kwenye barabara hasa ya Morogoro, Mandela, ambazo ni njia
kuu za kuelekea katika Bandari ya Dar es Salaam. Kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia (2020) msongamano wa
magari jijini Dar es Salaam serikali inapoteza zaidi ya shilingi
bilioni 4 kila siku, kwa watu kukaa kwenye msongamano na
kushindwa kufanya kazi za uzalishaji, matumizi makubwa ya
mafuta, na uchakavu wa magari. Ni kwa msingi huo kuwa
uzinduzi wa safari rasmi ya usafirishiji wa mzigo kupita reli ya
kisasa kutasaidia kuondoa upotevu wa mapato haya ya serikali.

