Gazeti imaan

Ghorofa lililodondo kaariakoo: Maswali magumu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hadi asubuhi la Jumapili Novemba 17, 2024 atu 13 wamefariki dunia, na wengine 84 kujeruhiwa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam

Jengo lililodondoka ni la ghorofa nne na lilikuwa katika makutano ya Mtaa wa Congo na Mchikichi. Rais pia amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuongoza timu ya wataalamu wa ujenzi kukagua
majengo yote ya eneo la Kariakoo na kumpa taarifa, huku akilitaka jeshi la polisi kupata taarifa ya kina
autoka kwam mmilili wa jengo lililoporomoka na jinsi hatua za ujenzi zilivyokuwa Ripoti zinasema ghorofa hilo lilianguka ghafla saa tatu na dakika tano asubuhi wakati mafundi ujenzi walipokuwa kazini wakitoboa kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka ndipo shughuli ya uokoaji ilipoanza
ikihusisha raia na vikosi vya majeshi ikiwemo JWTZ, Polisi, JKT na Zimamoto.

Kwa kuwa si mara ya kwanza majengo kudondoka tayari mijadala imeanza juu ya kama kuna udhibiti wa
kutosha wa ubora katika ujenzi wa majengo marefu. Gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa huko Kilimanjaro kijiji cha Sembeti, Marangu Desemba 19, 2022 watu watano walifariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa
baada ya jengo la ghorofa mbili lililokuwa linaendelea kujengwa kuanguka.

Nako Zanzibar Januari 25, 2017 jengo moja katika Mtaa wa Hurumzi, Unguja lilianguka wakati mafundi
wakilifanyia ukarabati na kuua fundi mmoja. Wakati mijadala ikiendelea, maoni ya wengi ni kuwa
huenda majengo mengi yanajengwa chini ya kiwango, hasa eneo la msingi usioendana na urefu wa jengo, ingawa kwa jengo lililodondoka safari hii linatajwa kuwa linatajwa kuwa na zaidi ya miaka 10.

Kwa nini lidondoke sasa, ndio swali linalotatiza wataalamu huku baadhi ya watu wakitilia shaka matengenezo yaliyokuwa yakiendelea. Hata hivyo, bila uchunguzi ni ngumu kujua nini kilitokea.
Wapo waloibua hoja ya udogo wa viwanja vya Kariakoo na kutaka viwanja kadhaa vya ‘high density’ viunganishwe mbele na nyuma ndio kipatikane kiwanja
kimoja kikubwa cha kujenga ghorofa imara yenye ‘basement’ kubwa kupaki magari.
Maeneo mengine yaliyodokezwa na wataalamu kuwa ni ya kuangaliwa ni ni usimamizi dhaifu wa ujenzi kiuhandisi na pia kubadilisha matumizi ya majengo kutoka hoteli au makazi hadi stoo ya kuhifadhia mizigo mizito na hivyo kusababisha jengo kuelemewa.

Matumaini ya Watanzania wengi ni kuwa changamoto iliyotokea itatumika kuchunguza maeneo yenye
udhaifu na hivyo kuepuka ajali kama hizi siku za usoni.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button