TZS 46b Kukamilisha Miradi ya Dharura (CERC) Mkoani Kagera ndani yamiaka minne (4)

Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekeza kiasi cha TZS 46bilioni kukamilisha miradi ya dharura ya barabara mkoani Kagera, ikihusisha miradi mitano (5) mikubwa yenye athari kubwa katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kuimarisha huduma za
kijamii na kiuchumi.
Mpango huu wa dharura, unaojulikana kama CERC PROJECTS (Contingency Emergency Response Component), umewezesha utekelezaji wa miradi mitano muhimu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ikilenga kuondoa vikwazo vilivyokuwepo kutokana na miundombinu duni au iliyoharibika.
Miradi hii ni pamoja na ujenzi wa madaraja na barabara unganishi ambayo ni nguzo muhimu kwa kuimarisha usafirishaji ndani ya mkoa na kuunganisha maeneo
yenye shughuli nyingi za kiuchumi.
Miradi hiyo ni:
– Daraja la Kyanyabasa lenye urefu wa mita 105
– Daraja la Kalebe lenye urefu wa mita 60
– Daraja la Kamishango lenye urefu wa mita 45
– Daraja la Kyetema lenye urefu wa mita 45
– Daraja la Kanino lenye urefu wa mita 30
Pamoja na hayo, miradi hiyo inahusisha pia ujenzi wa barabara unganishi zinazorahisisha usafiri kutoka na kwenda kwenye maeneo haya ya madaraja,na kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
