Hapa na Pale

Serikali itakavyokabiliana na  mabadiliko sera za misaada Marekani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inajiimarisha katika kukuza uchumi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kumudu maeneo yote muhimu yakiwemo ya sekta ya afya, elimu na maji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo Februari 6, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inajipangaje na mabadiliko ya sera za nje za Marekani ambayo yanakwenda kuathiri utekelezaji wa sera za elimu, afya na uchumi hususani miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na USAID.

“Uwezo tunao, tunazo maliasili,” alisema na kuongeza kuwa  jukumu lililo mbele ya Watanzania  ni kushirikiana kuhakikisha wanatumia maliasili na rasilimali zilizopo kujenga uchumi wa ndani kuwezesha mipango na bajeti itekelezeke.

Majaliwa alizidi kufafanua kuwa Tanzaniia inaheshimu sera za mambo ya nje za nchi nyingine na inatekeleza mikataba kwa mujibu wa sera hizo kama ilivyokubaliana na nchi husika katika maeneo mbalimbali. Pia, Majaliwa alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuifanya Tanzania kuwa na uhusiano mzuri na nchi mbalimbali duniani.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button