Habari
TZS 26.241B Kuboresha Bandari za Bukoba na Kemondo

Matokeo ya uwekezaji huu ni pamoja na ongezeko la mapato ya bandari kutoka takribani TZS milioni 23 kwa mwezi mwaka 2020 hadi kufikia TZS milioni 75 kwa mwezi mwaka 2025.
Aidha, bandari ya Kemondo imekamilisha kikamilifu uboreshaji wa miundombinu (100%), wakati bandari ya Bukoba iko katika hatua ya mwisho wa utekelezaji kwa asilimia 99%. Hii ni dalili thabiti ya mafanikio makubwa katika kuboresha huduma za usafirishaji majini na kuimarisha uchumi wa Kagera chini ya uongozi wa Rais Samia.
