Habari
KITUO CHA EACLC KICHECHEO CHA UKUAJI WA VIWANDA.

Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC) kinatarajiwa kuwa kichocheo mahsusi cha ukuaji wa viwanda nchini kwa kuweka soko kubwa, la moja kwa moja, kwa bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji wa ndani. Kupitia mfumo wake wa usambazaji wa kisasa na huduma jumuishi za kibiashara, kituo hiki kitaleta uwiano kati ya wazalishaji na wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo kutoa uhakika wa masoko kwa bidhaa zitakazozalishwa hapa nchini kama vile mazao ya kilimo yaliyongezewa thamani
