Habari
AJIRA 20,000 KATIKA KITUO CHA BIASHARA NA USAFIRISHAJI CHA EACLC

Ni matamanio ya Rais Samia vijana wa kitanzania kupata fursa za ajira kama anavyoeleza katika nukuu hii fupi alipokuwaanazungumza na vijana wajasirimali katika kituo hiki jana “Hongereni sana, tunaposema tunatengeneza mazingira kwa vijana haya ndo mazingira yenyewe. Ni kazi sasa kutumia fursa hii kutengeneza bidhaa kwa kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya kuviuza nje, Bidhaa zetu zinapendwa sana huko nje, serikali haiwezi kumshika kila moja,kazi ya serikali ni kutengeneza
mazingira, kwa hiyo badala ya kulaumu tumieni fursa hizi kujiinua”.
