Masauni azindua msikiti Coco Beach

Asifu The Islamic Foundation

Nipongeze The Islamic Foundation chini ya mwenyekiti, Aref Nahdi kwa kuhudumia jamii hasa kupitia ujenzi wa misikiti za ambazo zimechangia kuimarisha amani hapa nchini.

CRDB kuja na hati zinazofuata misingi ya Shariah ya Kiislamu (Sukuk)

Mashitaka 31 ya mauaji yawakabili wamiliki wa ghorofa Kariakoo

Hofu yazidi mataifa yakijiuliza Trump mpya atakujaje

Rais Samia anayoonadi mkakati wa nishati

Marais wataka tafakuri ya fursa za miaka 25 ya EA

 

Masauni azindua msikiti Coco Beach

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amepongeza taasisi ya The Islamic Foundation kwa kuwezesha ujenzi wa msikiti wa kisasa katika eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam. Amesema msikiti huu wa kisasa utahifadhi waumini zaidi ya 300 na pia kuchangia utulivu na amani ya kijamii.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi, alisifu jitihada za Sheikh Ibrahim Twaha na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aref Nahdi, kwa kutekeleza wajibu wa kidini na kijamii. Amesisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa viongozi wa dini katika kuimarisha utamaduni wa maelewano.

Katika hafla hiyo, viongozi mashuhuri walihudhuria wakiwemo Sheikh Abdulrahman Ishaq kutoka Qatar, pamoja na mjumbe maalum kutoka Saudi Arabia. Hafla hiyo ilifana na ilihitimishwa na dua ya pamoja ya kuombea umoja na amani.


Msikiti Coco Beach

Msikiti Coco Beach

Masauni azindua msikiti Coco Beach

Masauni azindua msikiti Coco Beach

Overlay Image
Sukuk Miundombinu

Uzinduzi wa Sukuk ya Miundombinu kwa Maendeleo ya Taifa

Serikali imezindua Hati Fungani ya Samia ya Miundombinu (Sukuk) kama mbadala wa kifedha unaofuata misingi ya Shariah ya Kiislamu, ikiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya barabara na kuchochea ukuaji wa uchumi. Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais, alisema kuwa Sukuk itavutia wawekezaji wa ndani na nje, huku ikiepuka mikopo yenye riba, kipengele muhimu cha Sukuk.

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika Mlimani City, Dkt. Mpango alisisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuunga mkono uchumi wa taifa. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Nsekela, alieleza kuwa Sukuk inatoa fursa kwa wale wanaotaka kuwekeza kwa njia inayohusiana na misingi ya Shariah, kwa kutoa faida isiyotokana na riba.

Hati fungani za Sukuk zinatofautiana na hati fungani za kawaida kwani hutolewa malipo ya kuponi kutokana na faida ya shughuli za kibiashara, badala ya riba. Hii inahakikisha uwekezaji unafanywa katika shughuli zinazokubalika kisheria.

Mpango huu umeundwa ili kuboresha mtandao wa barabara, kupunguza ucheleweshaji, na kutoa fursa bora za mikopo kwa wakandarasi wazawa, hasa wale wanaotekeleza miradi ya barabara chini ya TARURA. Uzinduzi huu unadhihirisha mafanikio katika kupata ufadhili mbadala wa kuendeleza miradi ya miundombinu ya taifa.

Sukuk hii inatoa fursa kwa watu wa dini zote kuwekeza, bila kubagua imani yoyote. Lengo la kukusanya Sh. Bilioni 150 linatarajiwa kusaidia kuboresha miundombinu muhimu ya barabara nchini.

Image 1 - Jengo Lililoporomoka

Mahakama Yazua Mashtaka 31 ya Mauaji dhidi ya Wamiliki wa Jengo Lililoporomoka Kariakoo

Wamiliki wa jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 31 ya mauaji kutokana na tukio hilo. Washtakiwa walitajwa kuwa ni Leondela Mdete, Zenabu Islam, Ashour Awadh Ashour, Bela, Ashery Sanga, Venance Aman, Linus Hasara, Pascalia Kadiri, Issa Issa, Lulu Sanga, Happyness Malya, Brown Kadovera, Sein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, Catherine Mbilinyi, Elton Ndyamukoma, Mariam Kapekepe, Elizabeth Kapekele, Hadija Simba, Frank Maziku, Rashid Yusuph, Ally Ally, Ajuae Lyambiro, Mary Lema na Khatolo Juma.

Wakili wa serikali, Adolf Lema, alidai kuwa washtakiwa hawa walishindwa kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha usalama wa jengo hilo, na hivyo kusababisha vifo vya watu wengi. Mahakimu walikataa ombi la dhamana kwa washtakiwa hao, wakitoa masharti magumu ikiwa ni pamoja na wadhamini wawili wenye uwezo wa kulipa bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.

Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, na kesi imeahirishwa hadi tarehe 12 Desemba 2024.

Image 2 - Uchunguzi wa Tukio
Mahafali Image 1
Mahafali Image 2

Wazazi Wapewa Siri Mafanikio ya Watoto Kielimu

Wazazi wametakiwa kuhakikisha wanasimamia malengo ya watoto wao katika kutafuta elimu kwa kuwafundisha mambo.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi katika mahafali ya Shule ya Awali ya Imaan iliyopo Kilakala, Ali Islam, ambaye aliwataka wazazi kuwafundisha watoto mambo hayo mawili ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Baada ya kuona mazingira ya shule hiyo na viwango vya ufahamu wa watoto, Ndugu Islam aliupongeza uongozi wa taasisi ya The Islamic Foundation kwa kuweza kuboresha mazingira ya shule hiyo ya Imaan na taaluma.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Wazazi wa Shule hiyo, Mhandisi Abeid Mlapakolo alisema kuwa maboresho yaliyofanywa katika shule hiyo umefanya iwe na mazingira mazuri ya kufundishia kwa walimu na kujifunzia kwa wanafunzi.

Naye Mkuu wa Shule za Imaan na Foresti Hill, mwalimu Ramadhan Sekitya, amesema kuwa shule imekuwa na matokeo mazuri kutokana na ushirikiano ulipo baina ya wazazi, walimu na mmiliki, taasisi ya The Islamic Foundation.

Hata hivyo, Sekitya aliwataka wazazi wengine kuendelea kuwamini kwa kuwapelekea watoto ili kuweza kuwapatia malezi bora na elimu kwa misingi ya dini ya Kiislamu.

Dkt. Hussein Mwinyi: Fidia Nono kwa Wakazi kwa Miradi ya Maendeleo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema watakaotoa maeneo yao kwa ajili ya miradi ya maendeleo watapatiwa fidia ya nyumba bora. Dk. Mwinyi alisisitiza kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa nyumba inaendelea kwa kasi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa nyumba za Chumbuni unaosimamiwa na Shirika la Nyumba Zanzibar, Dkt. Mwinyi alisema kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na ya kisasa kwa kuendeleza juhudi zilizopangwa tangu Mapinduzi ya 1964 chini ya uongozi wa Hayati Abeid Amani Karume.

Mradi wa Chumbuni unatarajiwa kuwa na nyumba 3,000, huku mipango ya miradi mingine ikilenga maeneo ya Kikwajuni, Kisakasaka, Kwa Mchina, na Mabaoni. Rais alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kununua nyumba hizo ili kuboresha maisha yao na kufurahia makazi yenye ubora na muundo wa kisasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Sultan Said, alieleza kuwa mradi huu ni moja ya mikakati madhubuti ya shirika hilo, ambalo sasa limejikita katika utekelezaji wa miradi yenye tija badala ya kushughulikia migogoro ya muda mrefu.

Rais Samia Apewa Mabilioni Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi

Tanzania imeahidiwa msaada wa dola za Marekani milioni 782.2 kutoka kwa Mfuko wa Maendeleo ya Dunia kwa ajili ya miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi. Hatua hii inalenga kusaidia nchi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kukuza nishati safi.

Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa mrejesho wa ushiriki wa Tanzania kwenye COP29 uliofanyika Baku, Azerbaijan, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema msaada huo ni hatua kubwa kwa maendeleo endelevu. Tanzania pia ilisisitiza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia ili kupunguza utegemezi wa nishati zisizo salama kama mkaa na kuni.

Dkt. Hussein Mwinyi Image

Pamoja na masuala mengine, Waziri wa Sheria wa Rwanda, Justice Emmanuel Ugirashebuja, alieleza changamoto mbili zinazoikabili jumuiya hiyo, ikiwa ni pamoja na nchi wanachama kutotoa michango yao.
Waziri huyo aliyemwakilisha Rais Paul Kagame, aliomba hatua kali zichukuliwe kuhakikisha michango inatolewa.

Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikitimiza miaka 25 tangu iliporejeshwa, wakuu wa nchi wanachama wamependekeza tafakari pana ya kubaini kama nchi wanachama zinafaidika vya kutosha na fursa zilizopo ndani ya jumuiya hiyo. Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi hicho, bado jumuiya hiyo inapaswa kutafakari kama uchumi wa nchi wanachama unafaidika vya kutosha na fursa zilizopo.

Rais alisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kutimiza wajibu wao wa kutoa michango ili kuhakikisha sekretarieti ya EAC ina rasilimali za kutosha kutekeleza majukumu yake. Waziri huyo alikosoa hatua ya majeshi ya Afrika Mashariki kujiondoa katika operesheni za kulinda amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), akisema inakiuka maagizo ya viongozi wa jumuiya.

“Hatua hii ya kumaliza mamlaka ya kijeshi inakiuka agizo la pamoja la wakuu wa nchi wanachama. Hii imeleta usumbufu, imeondoa imani, uwazi na uwajibikaji pamoja na maana ya ushirikiano,” alisema.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ametumia kikao hicho kumpongeza Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, mmoja wa marais watatu waliorejesha jumuiya hiyo mwaka 1999 baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977, kwa mchango wake mkubwa ndani ya jumuiya. “Mheshimiwa Museveni amekuwa mwalimu, msuluhishi na muunganishi wetu ndani ya jumuiya; tunapopotaka kukengeuka, anaturudisha katika misingi ya jumuiya,” alisema Rais Samia.

Marais pia walizungumzia fursa zilizopo ndani ya jumuiya hiyo na umuhimu wa kuchukua hatua kuhakikisha malengo yanafikiwa. “Tuna kila sababu ya kuona fahari kwa hatua hii, lakini tunapaswa kujiuliza kama chumi zetu zinafaidika vya kutosha na fursa zilizopo ndani ya ukanda wetu, kiasi cha kufurahia kutanuka kwetu,” aliongeza.

Makubaliano usitishwaji mapigano Israel, Lebanon yatafanikiwa?

Wakati idadi ya vifo ikiongezeka katika mzozo nchini Lebanon huku vifo 3,768 vikiripotiwa, idadi kub-

wa Mashariki ya Kati, Lebanon imeidhinisha wa ikitokea miezi miwili iliyopita.

likiwakilisha makundi yote ya wananchi wa Lebanon, mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, na walitangaza yakiwemo yale yanayoongozwa na Hezbollah.kuwa mapambano yao yangesimama pale tu Israel inge- tia kikomo vita vyake. Hii ni hatua kubwa inayolenga kumaliza zaidi ya mwa-

ka mmoja wa machafuko yaliyosababishwa na mgogoro kati ya pande hizi mbili.

Makubaliano ya sitisho la mapigano yanataka Israel kuondoa majeshi yake Kusini mwa Lebanon huku Hez- bollah ikirudi Kaskazini mwa Mto Litani.

Makubaliano haya, yaliyopitishwa na baraza la mawa-

ziri la Israel Jumanne usiku, yalianza kutekelezwa saa kumi alfajiri Jumatano. Katika kipindi cha vita hivi, watu

Katika kipindi cha siku 60, jeshi la Lebanon litachukua udhibiti wa eneo hilo na kuwa nguvu pekee ya kijeshi. wapatao 1.2 milioni wamelazimika kuhama makazi yao Kikosi cha kimataifa, kinachoongozwa na Marekani na

kushirikisha wanajeshi wa kulinda amani wa Ufaransa, kitasaidia kusimamia utekelezaji wa makubaliano haya.

Pamoja na matumaini ya kurejesha amani, makubalia-no haya yameibua maswali mengi kuhusu uhakika wa utekelezaji wake.

Wakosoaji wanaonya kuwa sitisho hili linaweza kuwa la muda mfupi kama hakutakuwepo na suluhu ya kisiasa inayoijumuisha Iran. Wakati huo huo, ukosefu wa msaa- da wa kutosha kwa walioathirika na vita, hasa Waislamu huenda ukazidisha changamoto za kijamii na kiuchumi katika taifa hilo ambalo tayari linakabiliwa na mdororo mkubwa wa kiuchumi.

Hofu yazidi mataifa yakijiuliza Trump mpya atakujaje

Vurugu zaua 4 baada ya jaribio la kupora msikiti India Za Kihindu za msimamo mkali (Hindutva),

Hari Shankar Jain, alidai kuwa msikiti wa karne ya 16 ulijengwa kwa makusudi kwenye eneo la hekalu la Kihindu. Tukio hili limeacha makovu makubwa, huku vijana wengi wakipoteza maisha na jamii nzima kuathirika.

Jibu la changamoto zinazokabili Waislamu duniani ilikimbilia kufanya uchunguzi bila kuwapa nafasi ya kue-wengi wao wakiwa Waislamu. Hatimaye Waislamu. Waislamu wanahisi kuwa uchunguzi wa msikiti huo, uliojengwa enzi za utawala wa Kiislamu wa Mughal (karne ya 16 hadi katikati ya karne ya 18), ni jaribio la kuchochea mgogoro wa kidini. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na silaha za moto, kama inavyothibitishwa na video zilizotanda mitandaoni.

Tukio hili limefananishwa na mgogoro wa msikiti wa Babri wa mwaka 1992, ambao ulisababisha ghasia kubwa na vifo vya karibu watu 2,000. Aidha, Waislamu wa eneo hilo wanadai kuwa mahakama imeonyesha upendeleo kwa upande wa walalamikaji, jambo linalokiuka haki zao za kikatiba. Msikiti huo, uliodumu kwa karne nyingi, unadaiwa kunyang’anywa kwa nguvu na hekalu kujengwa mahali pake.

Licha ya mauaji ya Waislamu wanne katika tukio hili, Polisi wamewakamata zaidi ya watu 25, huku wengine 2,500 wakifunguliwa mashtaka. Vyama vya upinzani, kama Congress na AIMIM, vimeishutumu serikali ya chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) kwa kuchochea mgawanyiko wa kidini kupitia uchunguzi wa msikiti huo. Mbunge wa Chama cha Samajwadi (SP), Zia-ur-Rehman Barq, pia ametuhumiwa kuchochea vurugu hizo, ingawa amekana tuhuma hizo, akisema, “Hii ni njama iliyopangwa.”

Kiongozi wa SP, Akhilesh Yadav, amesema, “Hili ni tukio la kusikitisha na ni matokeo ya siasa za chuki za serikali hii.” Vyama vingine vinataka uchunguzi wa kimahakama ili kuhakikisha haki inatendeka, huku wakisisitiza kuwa mauaji ya waandamanaji ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Katika hatua nyingine, vurugu hizo zimesababisha kufungwa kwa shule na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti katika eneo hilo. Hali hii inaendelea kuonyesha athari mbaya za siasa zinazolenga kugawanya jamii kwa misingi ya dini.

Republican vikiendelea, wasiwasi umeibuka mion-Kwa mujibu wa uchambuzi uliochpishwa katika tovuti yaShirika la Habari la Uturuki, Anadolu, Mataifa kama Somalia, Libya, Sudan, na Yemen yaliyokumbwa na marufuku hiyo yalipata athari ya mgawanyiko wa familia, ugumu wa kufanyabiashara, na kuzorota kwa mahusiano ya kidiplomasia.

Mnamo mwaka 2017, Trump alisaini agizo la kiutenda-ji lililozuia kwa muda wa siku 90 wahamiaji na wakimbizikutoka Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria, na Yemen kuingiaMarekani.

Hatua hii ilitafsiriwa na Waislamu wengi kama shambulio dhidi ya mataifa yao na imani yao. Hali hii imeendelea kuwa chanzo cha hofu hasa baada ya ushindi wake wa hivi karibuni,huku baadhi ya wachambuzi wakihofia uwezekano wa vikwa-zo hivi kurudi tena.

Kwa mujibu wa Mohamed Husein Gaas, Mkurugenzi waTaasisi ya Utafiti wa Amani ya Raad, athari za marufuku hizo zilikuwa kubwa kwa familia na fursa za kielimu na kitaaluma.

Gaas alisema hatua hizo zilionekana kama ubaguzi dhidiya mataifa ya Kiislamu. Huku akihofia kuwa huenda Trump akarejesha vikwazo hivyo, anaamini kwamba msimamo wakeunategemea mkakati wa kisiasa wa utawala wake mpya.

 

Hata hivyo, baadhi ya watu, akiwemo Anwar Abdifatah Bashir, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Amani na Utawala ya Afrika Mashariki wamekuwa na mtazamo tofauti, waki-amini kuwa Trump sasa anaweza kuwa na mtazamo wa kisiasauliopevuka na hivyo kutorejesha vikwazo hivyo.

Kwa ujumla, wachambuzi wengi wanasema hatua yoyoteya kurejesha vikwazo vya usafiri itazidisha mgawanyiko wa kidiplomasia kati ya Marekani na Afrika, hasa kwa mataifa ya Kiislamu.

Mpaka sasa, hakuna mwelekeo wa wazi wa sera za marekani chini ya Rais Donald Trump katika awamu yake hii ya pili kama rais wa 47 wa taifa hilo, licha ya ukweli kwamba hofu nawasiwasi umejaa kwa watu jamii na mataifa ya Kiislamu, husu-sani yaliyokumbana na zuio la 2017.

 

 

Tunapojenga madrasa na kuwasahau walimu tutafika?

Katika gazeti hili toleo lililopita kuliku-

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliwasisitiza Waislamu kujenga madrasa nyingi zaidi ili kuwapatia watoto mafunzo ya kiimani ambayo yatawawezesha kuwa raia wema na waadilifu kwa familia na taifa kwa ujumla.


Kauli hii ya Rais Samia inapaswa kutufikiri- sha na kuchukua hatua ambazo zitakuwa na manufaa kwa watoto wetu na taifa kwa ujumla. Sababu ya kusema hivyo ni kwamba madrasa zina umuhimu mkubwa katika kutoa elimu ya dini kwa watoto na vijana wetu, hususani katika zama hizi ambazo jamii inakabiliwa na.

Tatizo la mmomonyoko wa maadili.


Ni jambo lililo wazi kwamba elimu ya dini ina nafasi ya kipekee katika kujenga taifa imara lenye watu waadilifu na kuipunguzia serikali mzigo wa kupambana na maovu katika jamii. Cha kushangaza ni kwamba baadhi ya wazazi hawawapeleki watoto wao madrasa wala kuwa- himiza kufanya ibada ya sala na nyinginezo. Hayo pia ni matokeo ya kutoipa kipaumbele cha kutosha elimu ya dini.


Elimu ya dini ni muhimu mno kwani ina mchango mkubwa katika kuwaandaa vijana kimaadili na kuwapatia ufahamu wa dini yao. Kimsingi, tunaweza kusema kuwa, elimu ya dini ni tiba ambayo mwanafunzi anatembea nayo muda wote.


Katika hili, wazazi, walimu na Waislamu kwa ujumla wana wajibu wa kuwatayarisha vijana.

Wa Kiislamu kwa ajili ya changamoto tete na za kudumu za kimaadili.


Tunapomulika matatizo makubwa yanayozikabili madrasa, ni muhimu pia tuangazie suala la maslahi ya walimu. Ni ukweli kuwa walimu wengi wa madrasa hapa nchini hawana mishahara na badala yake wanategemea ada ndogo za wanafunzi kuendesha maisha yao.


Hii ni changamoto kubwa kwa Waislamu ambayo haipaswi kuachwa tu hivi hivi. Kuto- kana na changamoto hiyo, tungependa kutoa nasaha kwa wazazi wa wanafunzi na Waislamu kwa ujumla kuhakikisha wanaweka malengo, mipango, mikakati na juhudi za makusudi ili kuwawezesha walimu kiuchumi.


Iwapo kila mmoja akitekeleza wajibu wake, In shaa Allah, tunaweza kufikia lengo la kuwapa vijana wetu elimu nzuri ya dini.

Mara nyingi ninapokuwa maeneo ya mtaani kwetu huwa nawakum- busha vijana wenzangu kwenda msikitini kutekeleza ibada ya sala pindi muda wa sala un- apowadia. Hata hivyo walio wengi hunijibu kuwa nguo walizovaa hazina udhu, wakimaani- sha si twahara huku baa- dhi yao wakidai kuwa bado hawajajaaliwa na Mungu.

 

Si hao tu, pia wapo baa- dhi ambao huacha sala kwa kisingizio cha kut- ingwa na shughuli nyingi za utafutaji riziki. Nikizita- fakari kauli zao hujiuliza wanajua wanachokise- ma? Je, hawajui kwamba wapo duniani kwa ajili ya kumuabudu Allah?

Unataraji nini kwa Allah ikiwa waipuuza sala?

The Warning Against Neglecting Salah

Kuacha sala ni kujivika sifa ya kiburi na maji- vuno ukapita ni ishara ya kutojali na ni unafiki mbele ya Allah Ta’ala. Allah anawaonya wale wenye kupuuza sala (wanaosali pasina kutekeleza ipasavyo sharti na nguzo zake) kwa kusema:

“Ole wao wanaoswali. Ambao wanapuuza swala zao, ambao wanajionyesha.” [Qur’an, 107:4–6].

Allah anasema katika Hadithil Qudsiy: “Kiburi ni (mfano wa) vazi langu la chini, na utukufu ni (mfano wa) vazi langu la juu. Atakayejaribu kuninya’nganya moja kati ya (mavazi yangu hayo) mawili, nitamtupa motoni na wala sijali.” [Muslim].

The Significance of Salah

Sala ndiyo nguzo kuu ya dini ambayo nafasi na umuhimu wake ni kama kichwa katika kiwiliwili. Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) amesema:

“Mfano wa sala tano ni kama mto mkubwa unaopita mbele ya mlango wa mmoja wenu na ikawa mtu anaoga ndani ya mto huo kila siku mara tano.” [Muslim].

Hii inathibitisha kuwa Muislamu hapaswi kupuuza sala, na yeyote miongoni mwetu akikengeuka na kuacha wajibu huu atakuwa ni mwenye kuangamia hapa duniani, kaburini, na Siku ya Kiyama. Mtume pia amesema:

“Hakika jambo la kwanza kabisa kuhesabiwa katika matendo ya mja Siku ya Kiyama ni sala yake. Ikitengemaa, atakuwa amefaulu na ameokoka; na ikiharibika atakuwa amerudi patupu na amepata hasara.” [Tirmidhi].

Iblis’ Plot Against Salah

Hatupaswi kamwe kughafilika na ibada ya sala wala kuleta uvivu katika kuitekeleza, bali tuichukulie kuwa ni jambo la kwanza katika maisha yetu. Lakini wakati tunahimizana kutekeleza ibada ya sala tutambue kuwa, Iblis (shetani aliyelaaniwa) amechukua ahadi ya kuhakikisha kuwa anatupoteza na kutufitinisha.

Iblis ameelekeza nguvu kubwa ya vitimbi vyake katika kutuweka mbali na ibada ya sala pamoja na kututia shaka na wasiwasi wakati tunaposali. Hii ni kazi kubwa anayoifanya Iblis kwa lengo la kutekeleza azma yake aliyoiweka mbele ya Allah Ta’ala pale aliposema:

“Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika njia yako iliyonyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.” [Qur’an, 7:16–17].

Tangu zama na zama, Iblis amekuwa akifanya hila za kuwanyima Waislamu ladha ya ibada ya sala.

Ujumbe mahsusi kwa Waislamu wa Marekani

Hivi sasa, Donald Trump anajiandaa kuingia Ikulu ya Marekani kwa awamu yake ya pili mwezi Januari mwakani. Kuna nukta kadhaa muhimu za kuzingatia kama Waislamu, si tu wa Marekani bali wa ulimwengu mzima.

Katika toleo lililopita, tuliishia na nukta ya uhusiano mbaya wa Marekani na China iwapo utabadilika katika awamu ya pili ya utawala wa Donald Trump nchini Marekani.

Ujumbe mahsusi kwa Waislamu wa Marekani

PKK. Trump Hawezi Kumuiga Biden

Suala la Palestina halipo mikononi mwa Rais wa nchi bali lipo katika udhibiti wa Dola Kuu ya Marekani (Deep State), kwa sababu Israel ni mradi wa kimkakati ambao ni lazima ulindwe na kuimarishwa.

Kama ilivyo kwa uhusiano wa Marekani na Urusi kuwa ni jambo lililo nje ya uwezo wa Trump, naamini hali ni hiyo hiyo kwa suala la Palestina.

Mgogoro wa Palestina

Baadhi ya wachambuzi wamesema, Trump hapendelei kuendelea na mgogoro huu, lakini mimi nina mashaka yangu. Hata kama akisukuma mapatano ya amani, ni dhahiri kwamba mapatano hayo hayatakuwa kwa manufaa ya Wapalestina hata kidogo.

Tusisahau kwamba Trump ndiye aliyehamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem Mashariki, na msisahau pia mchango wake katika ‘Makubaliano ya Abraham Accords’ na nchi mbalimbali za Kiarabu.

Athari kwa Iran na Uturuki

Iran haifurahishwi na ushindi wa Trump, kwa sababu awamu ya pili ya utawala wake nchini Marekani ilijiondoa kwenye mpango wa ‘Iran deal,’ na vikwazo vilivyofuatia vinaendelea kuathiri uchumi wa Iran.

Uturuki inaonekana kufurahishwa na ushindi wa Trump kwa sababu viongozi wake hawakuwa na maelewano mazuri na Biden, ambaye alikuwa zaidi upande wa chama cha mrengo wa kushoto.

Mtazamo wa Uislamu kuhusu upandikizaji mimba

Islamic Perspective on Surrogacy

Utangulizi

Wanandoa waliomtuma awazalie mtoto. Katika hali hii, wazazi halisi kibaiolojia ndiyo watakaomlea mtoto huyu, na mwanamke huyu aliyebeba mimba na kuzaa mtoto kwa ajili ya wanandoa wengine (Surrogate) anakuwa kama chombo tu cha kumzaa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu, imekatazwa kabisa mwanamke asiyehusika katika ndoa kubeba mimba na kuzaa kwa ajili ya wanandoa wengine.

Maelezo

Fatwa ya Baraza la Fiqhi ya Kiislamu la Makkah ya mwaka 1984 iliruhusu ‘surrogacy’ kwa kupandikiza mimba ndani ya mfuko wa uzazi wa mke wa pili wa mume yule yule aliyetoa mbegu za kiume. Lakini mwaka 1985, baraza hilo lilifuta fatwa yake hiyo.

Kilugha na kidini, kuzaa, kwa neno la Kiarabu ni ‘Walad’ (to give birth), na kwa mama ni ‘Walidah’ yaani yule anayezaa. Qur’an inasema kwamba: “…hawawezi kuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa.” [Qur’an, 58:2].

Mwendelezo

Hata kama kuna makubaliano kati ya watu hao, mkorogeko wa ukoo, jambo ambalo linawezekana kabisa kutokea katika mipangilio hii ya ‘surrogacy’ na ambalo ni muhimu sana katika Uislamu, sheria ya Kiislamu imekataza kabisa ‘surrogacy’.

Katika makala ya leo tutaangazia aina nyingine ya teknolojia saidizi ya uzazi inayotambulika kwa lugha ya kisayansi kama ‘surrogacy’. Mwanamke asiye katika ndoa husika anabeba mimba na kuzaa mtoto kwa ajili ya wanandoa wengine.

Kipengele cha Stadi za Maisha

Kipengele cha Stadi za Maisha

Usafi binafsi

Usafi binafsi ni kipengele muhimu cha stadi za maisha. Kujua namna ya kujifanyia usafi binafsi kutamfanya mtoto avutie mbele za watu na ajiamini zaidi.

Mavazi

Kijana anatakiwa ajue namna ya kuvaa nguo sahihi kwa mujibu wa wakati, mahali na hafla husika. Kujifunza kuvaa kwa usahihi kutamuandaa kwa maisha ya baadaye.

Huduma ya Kwanza

Ufahamu juu ya namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu wanaokabiliana na majanga mbalimbali ni muhimu sana kwa vijana. Ujuzi huu unaweza kuokoa maisha yake au ya watu wengine.

Huduma ya Kwanza

Ustawi binafsi

Ustawi binafsi unajumuisha suala la kijana kujali afya yake kimwili na kiakili. Hili linajumuisha kujua namna ya kukabiliana na huzuni na msongo wa mawazo.

Somo la fedha

Vijana wanatakiwa wafunzwe namna ya kubajeti fedha zao na kuweka malengo ya muda mfupi na mrefu. Kujifunza bajeti ni hatua ya kuokoa fedha.

Kutumia muda vema

Vijana wanapaswa kujifunza namna ya kupanga na kutumia muda kwa busara, kuepuka kuahirisha mambo na kujifunza kuzingatia masuala ya msingi kama vile kusoma.

Ujasiriamali

Ujasiriamali ni ule ujasiri wa kuleta wazo jipya la biashara kwa lengo la kupata faida, na katika mchakato huo, kukubali kubeba hatari na wasiwasi wote wa biashara hiyo kushindwa, kwa mujibu wa kamusi mbalimbali ikiwemo Oxford.

Inaelezwa kuwa wajasiriamali wana mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa nchi yoyote. Wao hugundua mahitaji sokoni (ya bidhaa au huduma) na kubuni njia ya kukidhi mahitaji hayo, kiubunifu, na wao kupata faida na kukuza uchumi wao.

Wachumi wanasema wajasiriamali ni moja ya rasilimali nne zinazohitajika kukuza uchumi wowote: ardhi, wafanyakazi, mtaji, na ujasiriamali.

Mchakato wa Mjasiriamali

  • Hufanya utafiti wa kina.
  • Huandaa mpango wa biashara.
  • Hutafuta fedha – binafsi au kupitia mikopo.
  • Huajiri wafanyakazi na kusimamia biashara kwa ufanisi.

Tofauti kati ya Mjasiriamali na Mfanyabiashara: Mjasiriamali anatumia wazo la kipekee kuanzisha biashara mpya, wakati mfanyabiashara anafuata mkumbo kwa kutumia wazo lililokwisha jaribiwa.

Mjasiriamali mara nyingi huwa kiongozi sokoni kwa sababu anajibu mahitaji sokoni kwa njia za kipekee na za kiubunifu, hivyo kuleta mapinduzi makubwa. Hata hivyo, kwa sababu analeta ubunifu mpya, hatari ya kupoteza huwa kubwa – lakini akifaulu, faida huwa kubwa zaidi.

Kinachomsukuma mjasiriamali siyo faida tu, bali kutatua shida za watu sokoni.

Ujasiriamali

Ujasiriamali ni ule ujasiri wa kuleta wazo jipya la biashara kwa lengo la kupata faida, na katika mchakato huo, kukubali kubeba hatari na wasiwasi wote wa biashara hiyo kushindwa, kwa mujibu wa kamusi mbalimbali ikiwemo Oxford. Inaelezwa kuwa wajasiriamali wana mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa nchi yoyote. Wao hugundua mahitaji sokoni (ya bidhaa au huduma) na kubuni njia ya kukidhi mahitaji hayo, kiubunifu, na wao kupata faida na kukuza uchumi wao.

Wachumi wanasema wajasiriamali ni moja ya rasilimali nne zinazohitajika kukuza uchumi wowote, nyingine tatu za mwanzo ni ardhi, wafanyakazi na mtaji. Wajasirimali hutumia rasilimali hizo nyingine tatu kuzalisha bidhaa na huduma na hivyo kuunda sekta binafsi imara.

Mchakato wa Mjasiriamali

Hivyo basi, mjasiriamali akiona fursa atafanya utafiti, ataandaa mpango wa biashara, atatafuta fedha (zake mwenyewe au akope), ataajiri wafanyakazi na kusimamia hiyo biashara ili ilete tija.

Wasomi wanatofautisha kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara: Mjasiriamali anatumia wazo la kipekee kuanzisha biashara mpya wakati mfanyabiashara anaanzisha biashara kwa wazo la zamani ambalo lilishajaribiwa, yaani anafuata mkumbo.

Mjasiriamali mara nyingi huwa kiongozi sokoni kwa sababu anajibu mahitaji sokoni kwa njia za kipekee za kiubunifu na hivyo kuleta mapinduzi. Kwa sababu analeta ubunifu mpya, hatari ya kupoteza huwa kubwa lakini akishinda faida nayo ni kubwa.

Kinachomsukuma mjasiriamali siyo faida tu bali kutatua shida za watu sokoni.

Dondoo za Malezi ya Mtoto Tumboni

“Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima.” [Qur’an, 17:23]

Aya hii ya Qur’an inaonesha namna Uislamu unavyowapa kipaumbele wazazi. Amri ya kuwatendea wema wazazi wawili, imefuatanishwa na ile ya Tawhid, yaani kumuabudu Yeye Mwenyezi Mungu Mmoja na wa Pekee bila kumshirikisha na chochote. Hata hivyo, kati ya wazazi wawili, mama ana uzito wa kipekee kwa sababu ya jukumu lake la kuleta uhai mpya duniani kupitia ujauzito na malezi ya mwanzo ya mtoto.

Mama na Mtoto

 

“Umama unaanza pale ujauzito unapotunga na mabadiliko mengi hujitokeza kwa mama.”

Kliniki ni muhimu kwa mama mjamzito ili kufuatilia maendeleo ya mtoto tumboni. Wataalamu wanashauri mama kuhudhuria kliniki walau wiki ya 10 baada ya ujauzito kutambulika. Hii ni fursa ya kufahamu afya ya mama na mtoto pamoja na kupata elimu muhimu kuhusu lishe na mwenendo wa maisha bora wakati wa ujauzito.

  • Epuka matumizi holela ya dawa.
  • Chunga lishe yako kwa kuhakikisha mlo una virutubisho sahihi.
  • Muombe dua mtoto anayekua tumboni.
  • Hudhuria kliniki mara kwa mara kwa ushauri wa wataalamu.
  • Pumzika vya kutosha na epuka msongo wa mawazo.
  • Fanya mazoezi mepesi yanayoshauriwa na daktari.

“Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia maombi.” [Qur’an 3:38]

Tatizo Kubwa la Jamii Zetu

Tatizo kubwa la jamii zetu, hususan katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, tunasubiri mtu aokote makopo, apige watu ndiyo tujue huyu anaumwa akili! Hii si sahihi. Matokeo ya kushindwa kung’amua mapema dalili za maradhi ya akili ni kuchelewa kupata matibabu kwa sababu mhusika anakuwa amefikia hatua mbaya tayari, pengine kuokota makopo, kupiga watu na kadhalika. Kwa msingi huu, ni muhimu sana kujua viashiria vya maradhi ya akili ili tuweze kusaidiana kabla mambo hayajaharibika. Waswahili wanasema, mdharau mwiba guu huota tende.

Hutokea sana katika jamii zetu mtu ghafla anaanza kuwa na tabia zisizo za kawaida. Pengine anakuwa mnyonge na mwenye kujitenga na watu, mcheshi kupitilia hadi anajichekea mwenyewe akiwa pale yake! Pengina mtu anaonekana ana mawazo mengi muda wote. Tusichojua ni kuwa kumbe mwenzetu anapitia kipindi kigumu, anakabiliwa na matatizo lukuki ambayo yanampa msongo wa mawazo!

Niliwahi kuandika katika makala moja huko nyuma kuwa kukaa na tatizo bila kushirikisha wengine ni hatari. Wengine, kutokana na aina ya matatizo yanayowakabili, wanaamua kukaa nayo wenyewe na hatimaye huzidi kuumia kwa msongo wa mawazo, sonona na huishia kuchukua maamuzi mabaya. Ni jukumu la watu wa karibu kumkabili muhusika wanapoona dalili tu za mabadiliko fulani fulani kumuuliza kulikoni na kujaribu kumsaidia.

Wanaume ni wahanga wakubwa wa maradhi ya akili kwa sababu wamefundishwa kuwa ni aibu mtoto wa kiume kuliakulia, au hata kulalamikalalamika. “Pambana na matatizo yako mwenyewe,” ndivyo tunavyowaambia. Somo hili limeponza wengi. Pengine hata tukiona hitilafu za kitabia zenye kutia wasiwasi kwa wanaume, pengine kujitenga, kuingia kwenye lindi la mawazo, tunasema: “Mwacheni kijana wa kiume huyo ana mambo mengi, atatatua shida zake. Siyo kila kila kitu alielee kama mtoto wa kike.”

Matokeo ya mtu kutoshirikisha wengine shida anazopitia ni tatizo kuongezeka na hatimaye muhusika anafanya tukio linalotuacha wote kinywa wazi. Utasikia fulani kajiua, kamchomoza visu mkewe, kampiga bosi wake, kachanganyikiwa anaokota makopo sasa. Dalili mbaya zilikuwepo lakini sisi watu wa karibu tulizipuuza!

Bahati mbaya sana katika ulimwengu wa sasa vichocheo vya maradhi ya akili ni vingi. Maisha ni magumu. Mahusiano haramu ni jambo la kawaida kwa vijana. Shule kuna mitihani ambayo mzazi haelewi mrejesho mwingine zaidi ya alama nzuri. Ulevi umetapakaa sambamba wakati kamari tumeifanya kazi.

Nyuma ya yote haya kuna uchumi huria unaoongozwa na ushindani wa kibiashara na matangazo yanayocheza na akili za watu wajione wameungukiwa kwa kutokuwa na kitu fulani ambacho kimsingi si katika mahitaji ya lazima. Uchumi huu umewaingiza watu kwenye pupa za kutaka kumiliki ili waonekane wa kisasa. Wakikosa, shida inaanza na kuambukiza wanaowategemea kwa kuwapa shinikizo!

Mbaya zaidi elimu ya dini ambayo ingetukinga na shida za akili kwa kutufunza kukinai, kuikubali qadari ya Allah, kujikinga na njia mbaya wengi hatuna.

Vijue Viashiria vya Maradhi ya Akili

Tatizo kubwa la jamii zetu, hususan katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, tunasubiri mtu aokote makopo, apige watu ndiyo tujue huyu anaumwa akili! Hii si sahihi. Matokeo ya kushindwa kung’amua mapema dalili za maradhi ya akili ni kuchelewa kupata matibabu kwa sababu mhusika anakuwa amefikia hatua mbaya tayari, pengine kuokota makopo, kupiga watu na kadhalika. Kwa msingi huu, ni muhimu sana kujua viashiria vya maradhi ya akili ili tuweze kusaidiana kabla mambo hayajaharibika. Waswahili wanasema, mdharau mwiba guu huota tende.

Dalili za Maradhi ya Akili

Hebu tuone baadhi ya dalili zinazoweza kukujulisha kuwa huenda wewe mwenyewe au mtu wako wa karibu ana maradhi ya akili. Kiashiria kikubwa ambacho kinapaswa kukushtua unapokiona kwa mtu ni mabadiliko ya ghafla ya tabia na mitazamo. Miongoni mwa mabadiliko haya ya kitabia ni kupenda kulala sana, kujitenga na watu, kupoteza hamu ya kula, kutojijali, mawazo yasiyo na mantiki na kadhalika.

Sisemi kuwa mtu mwenye tabia hizi moja kwa moja ana maradhi ya akili. Inaweza kuwa ni dalili ya matatizo mengine. Pengine anaumwa tu homa, lakini pengine pia ni tatizo la kiakili. Ukiwa kama ndugu au rafiki, si vibaya kufuatilia ili kujiridhisha.

Mental Health Awareness

Baadhi ya tabia nyingine ni pamoja na kuwa na wasiwasi muda mwingi na kushtukashtuka, kutofurahia mambo ambayo zamani mtu alikuwa akiyapenda, ambavyo mabadiliko ya mara kwa mara na ya ghafla ya kihisia kama hasira, kipawa na karama maalumu ya kuona vitu vya ghaibu au watu.

Dalili nyingine ya hatari ni msongo wa mawazo unaopelekea mtu kukumbwa na huzuni ya kupitiliza na wakati mwingine kuingiwa na mawazo ya kutaka kujiua. Dalili nyingine inayoweza kuashiria maradhi ya akili ni pamoja na kuchokozeka na kukasirika haraka kwa mambo yasiyo na msingi.

Yupo ndugu yetu mmoja alikuwa na hali hii. Baadhi ya ndugu zake wa karibu waliamini kuwa ule alirogwa hivyo wakaamua kumpeleka kwa waganga. Baada ya kuhangaika sana, mgonjwa alirejeshwa akiwa hajapona wala hajapata nafuu yoyote. Alitokea mtu mwenye busara na kumpeleka hospitali ambako alikutwa na malaria iliyopanda kichwani.

Dalili moja au mbili kati ya hizi nilizozitaja zinaweza zisiwe kigezo tosha cha kusema mtu anaweza kuwa na maradhi ya akili, lakini bila shaka hapo mtu atahitaji uchunguzi.

Sauda bint Zum’at: Mke wa Pili wa Mtume (Rehema za Allah na Amani Zimshukie)

Kupitia Machungu ya Kifo cha Khadija (Allah Amridhie)
Baada ya kifo cha mke wake wa kwanza, Bi Khadija (Allah amridhie), Mtume Muhammad (Rehema za Allah na Amani zimshukie) alipitia kipindi kigumu cha huzuni na upweke. Khadija alikuwa kipenzi chake wa pekee na mchango wake katika ulinganiaji wa Uislamu ulikuwa mkubwa. Maswahaba walifahamu nafasi ya Khadija maishani mwa Mtume, lakini walimshauri aingie tena kwenye ndoa ili kupata mwenza wa kumsaidia kuendeleza ujumbe wa Uislamu.

Jina na Nasabu ya Sauda

Sauda bint Zum’at bin Qays bin Abdi Shams bin Abdi Uddi bin Nasr bin Malik, alikuwa mwanamke wa nasaba heshimika. Kabla ya kuolewa na Mtume, alikuwa mke wa Sukran bin Amr, mtoto wa ami yake, ambaye pia alikuwa miongoni mwa Waislamu wa mwanzo.

Ndoa ya Mtume na Sauda

Maswahaba walijadili kuhusu nani angemfaa Mtume baada ya kifo cha Khadija. Bi Khawla bint Hakim alimpendekeza Sauda, mjane wa Sukran, pamoja na Aisha bint Abubakr (Allah awaridhie). Khawla alimfuata Sauda na kumueleza pendekezo la Mtume, jambo lililomfurahisha sana Sauda. Hata hivyo, aliomba suala hilo liwasilishwe kwa baba yake, Mzee Zum’at, kwa ridhaa yake. Baada ya kushauriana, baba yake aliridhia na Mtume akamuoa Sauda.

Sauda bint Zum'at

Tabia na Wasifu wa Sauda

Sauda alikuwa mwanamke wa kipekee, mwenye mwonekano wa kuvutia na wa kupendeza. Alijulikana kwa ucheshi wake na uwezo wa kumchekesha Mtume wakati wa huzuni. Siku moja alimsimulia Mtume hadithi kuhusu jinsi alivyoshikilia pua yake aliporukuu akihofia isidondoshe damu. Hadithi hiyo ilimchekesha sana Mtume (Rehema za Allah na Amani zimshukie).

Pia, Sauda alikuwa na moyo wa ukarimu. Siku moja, Umar bin Khattab alimpelekea mfuko wa pesa, lakini Sauda alichukua pesa hizo na kuzitoa kwa wahitaji. Hili liliashiria moyo wake wa kujali na kusaidia wengine.

Safari ya Uhabeshi na Maisha Yake Kama Muislamu

Sauda na mume wake wa kwanza, Sukran, walikuwa miongoni mwa Waislamu wa mwanzo waliokubali Uislamu. Walishiriki safari ya Hijra kwenda Habbash (Ethiopia) kutafuta hifadhi kutokana na mateso ya makafiri wa Makka. Hata hivyo, baada ya kurudi Makka, mume wake alifariki dunia, na Sauda akawa mjane hadi alipooana na Mtume.

Ndoa Yake na Mtume

Baada ya ndoa yao, Sauda aliishi na Mtume kwa zaidi ya miaka mitatu. Hakuwa tu mke, bali pia Mama wa Waumini na kipenzi cha Mtume kwa utu wake wa kipekee na uaminifu.

Sauda na Ukarimu wa Dini

Sauda alijulikana kwa kipawa cha kusimulia hadithi na kuwatia moyo watu wa karibu yake. Alikuwa msaidizi wa kweli wa Uislamu, akiishi maisha yenye subira na radhi ya Allah baada ya majaribu ya kufiwa na mume wake wa kwanza.

Utii wa Maswahaba kwa Allah na Mtume

Maswahaba walikuwa wepesi kumtii Allah na kujisalimisha kwake haraka, na walikuwa wakikimbilia kutekeleza amri za Allah bila kuchelewa. Wakiwa wamesikia katazo au kemeo lolote, walikwepa mara moja. Huu ndio ukweli wa kujisalimu na utiifu wa halisi kwa Allah.

Hata ingawa Allah ‘Azza Wajallah’ ametuwekea amri nyingi, utekelezaji wetu unakumbwa na upungufu na wakati mwingine, tunazembea.

“Mtume (rehema na amani zimshukie) alikumbana na vishindo vingi, lakini alitufundisha kuwa mtumishi mtiifu kwa Allah ni yule anayekubali kutii amri zake bila kuhoji. Maswahaba walijidhihirisha kwa vitendo kuwa wao ni watumishi wa Allah kwa kujisalimisha kwake katika kila jambo.”

Katika zama za Mtume (rehema na amani zimshukie), wanawake walionesha mfano mzuri wa kujisalimisha kwa Allah Ta’ala, kumtii na kumnyenyekea bila masharti yoyote. Huu ni mfano bora wa wanawake wa Kiislamu, ambao walikuwa wakikimbilia kutekeleza amri za Allah na Mtume wake.

Mfano wa Abu Sa’id Al-Khudry (Allah amridhie)

Abu Sa’id Al-Khudry (Allah amridhie) anasema:

“Mtume alimuuliza, ‘Hawa ni punda au viongwe?’ Tukamjibu, ‘Ni viongwe.’ Akasema, ‘Mwakilishi wa Allah ni mtiifu.’”

Huu ni mfano wa maswahaba walivyokuwa wakijisalimisha kwa Allah kwa vitendo.

Wanawake wa Ki-Ansar Walivyojidhirisha kwa Utii

Katika wakati mmoja, wanawake wa Ki-Ansar walijitokeza haraka waliposhuka kauli ya Allah kuwa wavaa shungi zao ili kuonyesha utii na kujitolea kwa utukufu wa Allah. Aisha (Allah amuwie radhi) alisema:

“Wanawake wa Ki-Ansar walionekana kama kunguru kwa vile walijifunga shungi zao kwa haraka baada ya kushuka kwa aya hii.”

Utii wa Kweli ni Kutekeleza Bila Mashaka

Utii wa kweli ni ule unaotekelezwa bila mashaka au kujiuliza, na Maswahaba walikubali kutii amri za Allah bila kujali mazingira au changamoto walizokutana nazo. Huu ni mfano wa utii wa kiwango cha juu, na ni wa kuigwa na Waislamu wa sasa. Maswahaba walikuwa mfano bora wa kujitolea kwa Allah katika kila hali.

Tukio la Anas bin Malik (Allah amridhie)

Hali hii inajidhirisha pia katika tukio la Anas bin Malik (Allah amridhie), ambapo alikumbwa na swali kuhusu kula nyama ya punda. Aliishi katika mazingira ya kipekee ya utii wa Allah, akifuata sheria na maadili yaliyowekwa na Mtume. Hii inatuonyesha umuhimu wa kufuata maagizo ya Allah na Mtume bila kushukiwa na hisia au shaka.

Maswahaba walijisalimisha kwa Allah katika kila jambo, kama inavyoshuhudiwa na hadithi kutoka kwa Anas bin Malik, ambaye aliona kuwa utekelezaji wa amri za Allah ni jambo la muhimu zaidi. Walijitolea na walikuwa tayari kutekeleza amri za Allah, bila kujali majaribu waliyokutana nayo.

Hitimisho

Utii wa Maswahaba kwa Allah na Mtume ni mfano wa kuigwa, na ni lazima sisi Waislamu tuonyeshe utayari wa kujisalimisha kwa Allah na kutii amri zake kwa bidii na moyo safi, kama walivyofanya Maswahaba.

Kinyonga: Mjusi anayevutia kumtazama

KINYONGA: Mjusi anayevutia kumtazama

Kinyonga Image
Wengi wao hupenda kupumzika kwenye miti, ingawa wapo wanaotambaa wakiwamo panzi, nzige, kumbikumbi, nzi, kore, siafu na wengineo. Pia kuna aina ya vinyonga wanaokula majani ya mimea. Vinyonga wakubwa, wao hupendelea kula ndege, baadhi wanaopendelea kukaa kwenye nyasi au vichaka vidogo, majani yaliyoanguka au kwenye matawi yaliyokauka.
Vinyonga wanapatikana barani Afrika, Asia na Ulaya, ila wengi wadogo na aina nyingine ya mijusi. Wachunguzi wa masuala ya wapo Afrika hususani nchini Madagascar. Vilevile kuna aina ya viumbe hai wanasema, vinyonga wanakula sana wakati wa baridi. Vinyonga wanaopatikana Mashariki ya Kati, aina moja wanapatikana nchini India, Pakistan na Sri Lanka, na wachache wanapatikana katika visiwa vilivyopo kwenye bahari ya Hindi. Na katika msimu wa joto wanapunguza kula.
Mambo 10 Usiyoyafahamu Kuhusu Kinyonga
Jicho la Kinyonga: Kinyonga ana uwezo wa kipekee wa kuona kwa namna ambayo ni tofauti na wanyama wengi. Jicho moja lina uwezo wa kutazama vitu vilivyopo mbele yake kwa mzunguko wa digrii 360, wakati jicho jingine lina uwezo wa kutazama vitu vilivyopo nyuma yake. Hii ina maana kwamba kinyonga ana uwezo wa kuona kila kitu kinachomzunguka kwa wakati mmoja. Hii inamwezesha kuwa macho yake yachukue taswira ya kila kitu anachokiona na kupeleka taarifa kwenye ubongo wake.
Mate ya Kinyonga: Mate ya kinyonga yananata sana kiasi kwamba, ikiwa mdudu atakwepa kutoroka, hakika hatakuwa na njia ya kutoroka. Kinyonga pia amejaliwa ulimi mrefu ulio na uwezo wa kufikia mara mbili ya urefu wa mwili wake. Ulimi huu ni sehemu muhimu kwa kinyonga kwani humsaidia kumkamata mawindo kwa urahisi. Aidha, ana mkia mrefu uliojikunja na macho makubwa ambayo anaweza kuyazungusha katika mwelekeo wowote – juu, chini, kulia au kushoto – ili kufuatilia mazingira yake.
Rangi ya Kinyonga: Ingawa kinyonga ana uwezo wa kubadilisha muonekano wa rangi yake, rangi yake halisi ni kijani na kahawia. Rangi hii hubadilika kulingana na mazingira, mwanga, joto, hofu ya adui au hali ya hisia. Kwa mfano, anapokuwa katika mazingira hatarishi, kinyonga anaweza kubadilisha rangi yake ili kuendana na mazingira yake na kuwa ngumu kugundulika na wanyama wanaomwinda.
Wakati wa Utafutaji wa Chakula: Vinyonga ni viumbe wa mchana, ambapo hufanya shughuli zao za utafutaji wa chakula wakati wa mchana. Wanapokuwa wamejishughulisha kutafuta chakula, ni kawaida yao kuwa na shughuli nyingi na shughuli zao zinafanyika kwa haraka. Wakati wa usiku, vinyonga hupumzika na hutumia usiku kama kipindi cha kupumzika.
Maji ya Kunywa: Vinyonga hawapendi kunywa maji kama wanyama wengine. Badala yake, wanapata maji kwa kutumia umande (unyevu) wa asubuhi au kwa kumeza majani yaliyojaa unyevu. Hii inawawezesha kuishi katika maeneo ambayo upatikanaji wa maji unaweza kuwa mgumu, kama vile milimani na jangwa.
Hadhari Kabla ya Kudhurika: Ingawa kinyonga anaweza kumdhuru binadamu, kabla ya kufanya hivyo, hutoa tahadhari. Ana tabia ya kubadilisha rangi au kuonyesha ishara nyingine ya kuonyeshea hatari inayojiandaa. Kinyonga hutumia mbinu hizi za tahadhari kuzuia kuwa na mgongano na viumbe wengine, ikiwa ni pamoja na binadamu.
Rangi ya Kinyonga Iwapo Mnyonge: Watu wengi wanaamini kuwa kinyonga akiwa katika eneo lenye rangi ya kijani lazima awe wa kijani. Hata hivyo, kinyonga ana uwezo wa kubadilisha rangi kulingana na mazingira, na anaweza kuwa na rangi tofauti na ile ya eneo analoishi. Hii inampa uwezo wa kujificha kwa ustadi mkubwa, lakini pia inamruhusu kubadilisha rangi kulingana na hali yake ya kihembe.
Rangi ya Kinyonga Iwapo Mnyonge: Ikiwa kinyonga anakosa chakula au kitu muhimu katika mazingira yake, rangi yake inaweza kufifia. Hii ni ishara kwamba kinyonga amekosa kitu cha muhimu kama chakula, hali ya hewa, au mazingira bora ya kuishi, na inamaanisha kuwa yupo katika hali ya dhiki.
Ulimi wa Kinyonga: Kinyonga ana ulimi wa kipekee ambao una sifa ya kuwa na gundi. Ulimi huu ni muhimu kwa kinyonga kwa sababu humuwezesha kumkamata mawindo kwa haraka na kwa urahisi. Hii ni sehemu muhimu ya maisha yake, na ulimi huu unaweza kufikia hadi mara mbili urefu wa mwili wake.
Vinyonga Wanapokutana: Wakati vinyonga wawili au zaidi wanapokutana, rangi zao hugundulika kuwa angavu zaidi. Hii ni kwa sababu kila mmoja hutaka kumwonyesha mwingine kuwa yeye ni bora kwa kumwangazia rangi zaidi ili kuonyesha nguvu au mng’ao wa kimwili. Vinyonga hutumia rangi zao kuonesha hali ya kujivunia au kukubalika katika jamii yao.
Chakula cha Kinyonga: Kinyonga anakula wadudu warukao, na hao ndiyo chakula chake bora zaidi. Kinyonga pia anakula aina nyingine ya mamba na minyoo inayopatikana katika mazingira anayokaa.
Kuhusu Kinyonga na Mazingira Yake
Naam ndugu yangu msomaji na mfuatiliaji wa safu hii ya ‘Fahamu usiyoyajua’, karibu tena katika mfululizo wa makala hizi zinazohusu tabia na maisha ya viumbe mbalimbali wa Allah, Mbora wa Uumbaji. Juma hili nimekuletea habari kemkem kuhusu kinyonga, kiumbe jamii ya mijusi, ambaye ana tabia nyingi zinazomtofautisha na mijusi wengine. Kinyonga yupo kundi moja na kenge na mamba, na hupendelea kuishi kwenye misitu ya mvua, jangwani, ukanda wa Savanna na kwenye milima.
Hitimisho
Inasikitisha kuona kuwa karibu nusu ya vinyonga wameshatoweka duniani kwa mujibu wa sensa mbalimbali zinazofanyika kwa njia ya uratibu. Inasemekana, hivi sasa Madagascar ndiyo nchi pekee yenye karibu aina (species) zote za vinyonga waliosalia duniani, ikikadiriwa kuwa na aina 160 za vinyonga.
Kinyonga Image 2
Back to top button