MATUKIO MATATU NDANI SIKU MOJA

Alipoanza safari ya utumishi uliotukuka kwa Taifa mwaka 2021,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia
Suluhu Hassan alikuja na kauli mbinu yake kwa taifa ya “ Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania -Kazi Iendelee” huenda kauli hii
haikuwa imeeleweka vyema kwa wengi wakati ananza utumishi
huu wa juu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama
walivyosema wahenga wakati ni msema kweli, ni Dhahiri sasa
kauli inaeleweka kwa watanzania wengi. Kasi na juhudi za Rais
Samia kuwaletea watanzania maendeleo katika kipindi kifupi
kinaridhisha sana. Juzi tarehe 30 Julai 2025 alikuwa mikoa ya
kusini kuzindua kiwanda cha majaribio cha uchenjuaji wa
madini ya urani katika mkoa wa Ruvuma, na jana tarehe 31 Julai
2025, anazindua matukio matatu kwa mara moja (katika lugha
ya vijana ungeweza kusema ni matukio matatu ndani ya track
moja).
Ninachokusudia kueleza hapa ni kuwa Rais Samia ni kiongozi
anayewaza, na kutenda maendeleo ya wananchi nyakati zote.
Uzinduzi wa miradi mitatu kwa wakati moja leo ni udhihirisho wa
mapenzi makubwa aliyonayo kwa Taifa. Mhe Rais Samia leo
amezindua rasmi shughuli za usafirishaji wa mizigo kwa reli ya
kisasi ya Dar es salam -Dodoma (SGR), Uzinduzi wa kituo cha
ushafirishaji wa Bandari kavu ya Kwala sambamba na uwekeji
wa jiwe la msingi msingi wa eneo la Viwanda ya Kwala, kwa
hakika Rais Samia amebeba maono sahihi ya safari ya
maendeleo ya taifa letu.

