Uncategorized

Usiwe mwanachama wa Jumuiya ya wanaoabudu Ramadhani Tanzania

Upepo huu wa Ramadhani umetulia mwisho wa tangazo linalo- wataka Waumini kuishika amri ya kufunga kama walivyowajibishwa wenzao waliopita, ‘la’allakum tat- taqoun’, (Qur’an, 2: 183). Taqwa ndilo lengo haswa la kuja kwa funga ndani ya Mwezi Mtukufu Rmadha- ni. Upepo ulipoanza kuvuma na ku- sisimua ngozi za waumini, wal- ionekana wakichangamka na ku- jiandaa na kusikika kuutaja sana mwezi huu wa kheri utadhani kwamba wanajipanga kumpokea mgeni mkubwa mheshimiwa, na ni kweli Ramadhani ni mgeni rasmi muheshimiwa. Vyombo vya habari, hasa vile vya Kiislamu, vilisikika vikiwakumbu- sha na kuwataka Waumini waji- pange kumpokea na kumuenzi mgeni huyo, huku wakitumbuizwa na ‘anaashiid’ zenye maudhui husi- ka. Redio zisizo za Kiislamu (redio ngoma) zinazosimamiwa na Wais- lamu, zilisalimu amri mbele ya upe- po huo laini, tangu kukaribia kufika Ramadhani na muda wote wa ku- wepo kwake, zikasikika zikitoa ma- tangazo na jumbe zenye mwelekeo wa dini moja kwa moja, sambamba na uendeshaji vipindi vya kuuhusu mwezi wa ibada, kama vile mawaid- ha, mahojiano na masheikh pamoja na ufafanuzi juu ya hukmu za ibada ya funga.Masheikh katika vituo vyao vya

da’awa walijipanga na kuweka utar- atibu mnasaba wa kimsimu kuhak- ikisha wanawanufaisha zaidi Wau- mini wao.

Qur’an ilipokusanya watu 60,000 dar

Mwezi wa Ramadhani – ambao ndipo Qur’an imeteremka – mwaka huu uliambatana na tukio kubwa la kihistoria lililowakutanisha maelfu ya Waislamu. Upepo wa Ramadha- ni ulipenya ndani ya nyoyo za zaidi ya Waislamu elfu sabini walioam- shwa na hisia za kukipenda na kuki- jali Kitabu chao Kitukufu, Qur’an.

Waislamu waliotoka maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam, mikoa mingine ya Tanzania bara na visiwani, na hata kutoka nje ya nchi, wakiwa pamoja na viongozi wao wa kidini na kisiasa, walijikusanya kati- ka Uwanja wa Taifa na kushuhudia mchuano mkali katika Mashindano ya Afrika ya Kuhifadhi Qur’an.

Ilikuwa ni siku ya kuamini uwezo mkubwa wa Qur’an wa kuwakusan- ya walimwengu chini ya mafunzo yake matakatifu katika nyanja zote za maisha.

Misikiti ilivyofurika

Upepo wa Ramadhani ulitembe- lea maskani za Waislamu ma – ‘ta- riku-sswalaa’ (wasioswali), ukawakuta wamelala kiroho, uka wamwagia matone ya nasaha, wa-  kashtuka na kukimbilia misikitini,

wakajiunga na wenzao katika utekelezaji wa swala za jamaa, Iju- maa na Tarawehe.

Upepo uliwan’garisha na nyuso zao zikamemetuka kwa athari ya ibada. Walibadilika kimavazi, maneno na mwenendo wao mzima.

Katika mwezi wa Ramadhani misikiti ilivumiwa na upepo huo laini na kufikia kilele cha furaha yake na kutabassam, kwa kupokea idadi kubwa ya waswaliji walioijaza kila kipindi cha swala, ingawa ilishikwa na mshangao na kujiuliza: “Wau- mini hawa hivi walikuwa wapi miezi yote kumi na moja ya mwaka?!” Hivi sasa misikiti imeshagubikwa na si- manzi na wasi wasi wa kuhamwa tena!

Hofu ya Mungu na mwezi wa Hijab

Katika maeneo mengi wanayoi- shi Waislamu, upepo wa Ramadha- ni uliziathiri nyoyo zao na kuogopa na kujisikia aibu kufanya dhambi hususan zile ya dhahiri, kama kuse- ma uongo, kubishana, kudhulumu wengine, kuwatazama wanawake/ wanaume kwa matamanio au ku- fanya utani nk.

Si hayo tu, bali ni mara nyingi –wakiwa katika marashi ya upepo wa Ramadhani – walisikika wakion- yana kwa kusema: “Jamani swau-mu, Ramadhani hiyo… kila pale mmoja wao anapojaribu kuvuka Upepo mwanana wenye manu- kato ulizigusa pia hisia za akina dada wa Kiislamu waliozowea kutoka bila ya kujisitiri kisheria. Wadada wal- ionekana katika hijab ya kutosha na kujisikia vibaya kuionyesha miila yao kwa wanaume ndani ya Ramad- hani. Upepo wa Ramadhani uliwa- kumbusha pia Waislamu suala zima la ukarimu na kuwasaidia wasioji- weza. Migao mbali mbali ya vyakula na mialiko ya futari imekuwa ikitia fora kipindi chote cha uwepo wa up- epo. Manukato ya upepo wa Ramad- hani Waislamu walipoyapata kwa mbali na kuvutiwa na burudani yake, waliinua pua zao juu juu waki- hangaika kuyatafuta. Shauku ya kuyapata na kuyanusa mpaka wa- tosheke iliwajaa, wakaenda kuyaku- ta misikitini ambako kwenye urithi aliouacha mtume (elimu). Waislamu walikaa mbele ya masheikh wao kwa utulivu sana na unyenyekevu mkubwa na kusikiliza tafsiri ya Kitabu Kitukufu kilichoter- emshwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, sanjari na kupata nasa- ha mbali mbali za wanazuoni hao! Upepo – kwa muda wote wa ku- wepo kwake – uliwakumbusha hu- ruma, na upendo pamoja na tabia laini makazini, masokoni, stendi za magari na mabarabarani. Waislamu walikumbushwa pia juu ya utama- duni wa kuombana radhi na kusameheana wanapokoseana, wa- kasikika wakisema: “Usipomsame- he aliyekuomba radhi huna swau- mu.” Kwa ujumla, Mwezi wa Ramad- hani umekuja kutuonjesha kidogo utamu wa maisha waliyoishi Mtume na Maswahaba, lakini kwa upande mwinginekutubainishiauwezekano wa kuishi Kiislamu katika zama zetu hizi kwa maeneo yote ya maisha pale ambapo upepo (taqwa) utaendelea kutuachia athari zake. Raha iliyoje kuishi maisha ya Kiislamu! Lakini… Waislamu Ramadhani na funga yake imeshatuaga na hatuna uwezo wa kuizuia na haiji tena mpaka mwakani. Ni mgeni wa siku 29 au 30 tu, lakini upepo (taqwa) ndiyo ambao tukitaka tunaweza kubaki nao tukiyanusa manukato yake hadi mwakani. Atakayekula khasara ni Muisla- mu atakayejiunga na Jumuiya ya Wanaoabudu Ramadhani Tanzania (Juwarata). Ni jumuiya hatari isiyo na usajili halali ambayo mwenyekiti wake ni Shetani mpotoshaji. Na ndio maana kazi zake za kuwasajili wanachama wapya (Waislamu wal- iojisahau) huzifanya kwa siri sana kila ufikapo mwezi wa Shaabani baada ya kubaki katika mkondo wa maasi miezi yote kumi na moja! Kwa kumalizia makala yetu, tun- apenda kuwanasihi Waislamu kwa mfano wa wasia alioutoa Khalifa wa kwanza (Abubakr); “Baada ya utata uliowakuta Waislamu juu ya uhaki- ka wa kifo cha Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie). Alisema: “Ambaye alikuwa anamuabudu Mu- hammad basi Muhammad ame- shakufa, na ambaye alikuwa ana- muabudu Allah, basi Allah yu hai, hafi. Na sisi tunasema: “Ambaye alikuwa anaiabudu Ramadhani, Ramadhani ni kiumbe huja na kutoweka, lakini aliyekuwa ana- muabudu Allah, basi Allah hafi na yupo haondoki abadan, basi aen- delee kumuabudu.” Waislamu tusirudi tena baada ya Ramadhni kuwa waasi. Muabudiwa wetu ni mjuzi kuliko tunavyomjua sisi na anayafuatilia kwa makini ma- tendo yetu hata katika miezi inayo- fuata. Tusiichezee nguvu kubwa isiyo na mfano. Zidumu kwa wote athari za upepo wa Ramadhani. Amiin. Kullu A’amin Waantum Bikhayr

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close