Uncategorized

Udhuru unaoruhusiwa na sharia kuacha

SEIF RUGA Wepesi wa Uislamu katika ibada ya funga. Hakika tofauti baina ya kanuni zilizotungwa na binadamu, na sharia zaaliyemuumbabinadamu,nikamaviletofautikatiyabinadamunaMuumbawao. Kwasababuhiyo,ndiyo maana hutokea wakati kanuni na miongozo iliyotungwa na binadamu hufeli na kuonesha udhaifu, kasoro na mapungufu, ima kwa kutolipa uzito shauri husika au kupitiliza mpaka

Aidha, hutokea kanuni za kibin-amu zikapatia mara moja na ku- kosea mara chungu nzima.

Ama sharia iliyotoka kwa Mwenye Hekima na Mjuzi wa vi- umbe wote, imekuja kukamilisha mahitaji ya mwanadamu, yenye kutengeneza na kusuluhisha mwenendo mzima wa maisha yake ya kila siku, ipo sawasawa haina kupindisha ndani yake.

Zaidi ya hayo, Sharia ya Mwenye- zi Mungu inachunga udhaifu aliy- okuwa nao mwanadamu, pamoja na hali zinazomzukia mwanadamu kutokana na mazingira husika. Kwa kuzingatia yote hayo, sharia ya mbin- guni inatofautiana na kanuni za ar- dhini zilizotungwa na wanadamu kwa utashi wao kwa tofauti kubwa mno, kamavilembingunaardhi.

Sharia iliyokuja kutoka mbinguni haiwalazimishi wafuasi wake kutekeleza hukumu wasiyoiweza. Sharia hiyo imejengwa katika msingi wa kuwafanyia watu wepesi na ta- hafifu pamoja na kuwaondolea mashaka na taabu.

Maandiko yanayobainisha wepesi wa Uislamu

Maandiko ya Qur’an Takatifu, ambayondiyomhimiliwakwanza unaozingatiwa katika kutoa huku- mu, sharia na muongozo yamebain- isha hilo. Aidha, Hadithi za Mtume (rehema na amani ya Allah imshuk- ie), ambazo huzingatiwa kama mhi- mili wa pili katika kutoa hukumu na muongozo, zimezingatia udhaifu huo wa kibinadamu.Kwa kuzingatia mihimili hii mik-uu miwili, unakuta Sharia ya Kiisla- mu imeugawa wepesi huu katika se- hemu tano. Kwanza, maandiko ya- nayobainisha uondoshwaji wa tabu na shida. Allah Aliyetuka amesema: “Hapendi Mwenyezi Mungu kuku- tieni katika taabu” (Qur’an, 6:5). “Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim, ” (Qur’an, 22 78). Pili, maandiko yanayofahamisha juu ya wepesi na utahafifu. Na wala hakubainisha suala la taabu ndani yake. “Mwenyezi Mungu anakutak- ieni yaliyo mapesi wala hakutakieni yaliyo mazito,” (Qur’an, 2:185). “Mwenyezi Mungu anataka kuku- punguzieni tabu, na mwanadamu ameumbwa dhaifu, ” (Qur’an, 4;28). Tatu, ubainifu wa usamehevu uli- opo katika dini ya Uislamu pamoja na wepesi wake na kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah imshuk- ie) ni mpole mno na mwenye huru- ma kwa umma wake. Allah Aliyetuka amesema: “Hakika amekwisha kujieni mtume kutokana na nyinyi wenyewe, yana-muhuzunisha yanayokutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Wau- mini ni Mpole na mwenye huruma, ” (Qur’an, 9:128). Nne, Mtume (amani na rehema za Allah zimeshukie) huogopea mashaka yasiwapate umma wake. Hayo yanabainishwa na Hadithi aliyoipokea Swahaba Mtukufu Abu Huraira (Allah amrehemu): “Lau kama si kuchelea uzito juu ya umma wangu ningeliwaamuru wao kupiga mswaki…. ” (Muslim). Tano, Mtume aliwaamuru Maswahaba wake kufanya tahafifu na kuwakata- za kushadidia katika mambo. Mfano ni kauli yake Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie): “Ewe, Muadhi unataka kuwafitinisha watu na Mola wao! Iwapo unaswalisha watu, soma, ‘Sabbihisma Rabbikaa- laa’, ‘Wallaili idhaa yaghshaa’, ‘Wad- huhaa, ’ (Muslim). Mtume alimtahadharisha Swa- haba wake Mtukufu, Muadhi bin Jabali (Allah amridhie), asije ku- wafitini watu na Mola wao kwani alikuwa akisalisha husoma sura ndefu katika swala hali ya kuwa katika ibada kuna wazee, vikongwe, wenye shida na haja mbalimbali.Hivyo, inabidi kuzingatia nyudhuru za watu.

Udhuru anaoruhusiwa mtu kuacha kufunga

Funga ni katika ibada nzito yenye mashaka na tabu ndani yake na ina- hitaji uvumilivu na subira ya hali ya juu. Hutokea baadhi ya watu katika jamii wasiweze kufunga. Kwa kuz- ingatia desturi ya Uislamu ambayo hufanya wepesi na kuondosha taabu kwawatu, AllahAliyetukaameruhu- su kwa baadhi ya waja wake kuacha kufunga, na amewapa ruhusa ya kula mchana katika Mwezi wa Ram- adhani, kwa kuwahurumia na ku- wafanyia wepesi. Allah Aliyetuka anasema: “Basi atakaye kuwa mjini katika mwezi huu na aafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu katika siku ny- ingine. Mwenyezi Mungu anakutak- ieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, ” (Qur’an, 2:185). Wafuatao ni watu waliyoruhusi- wa kufungua katika mchana wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wapowatakaozilipasikuwalizofun- gua, na wapo ambao hawatakiwi wazilipe siku hizo.

Mtu aliyekula au kunywa kwa kusahau

Iwapo Muislamu aliyefunga akila au kunywa kwa kusahau, kwa maa-na bila ya kukusudia, hatakiwi ku- fanya jambo lolote, na funga yake ipo sahihi, kwa maana anaendelea na funga yake kama kawaida. Na wala siku hii hatoilipa. Hii ni kwa mujibu wa kauli yake Allah Aliyetuka: “(Ombeni) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisa- hau au tukikosea,” (Qur’an, 2:286). Na katika Hadithi, Mtume (ama- ni na rehema ya Allah zimshukie) ili- yopokewa na Abu Huraira (Allah amridhie): “Mtu yeyote aliyekula au kunywa kwa kusahau katika Mwezi wa Ramadhani, aiendeleze Funga yake, kwanisivingineAllahAliyetu- ka ndiye aliyemlisha yeye na kumny- wesha,” (Bukhari na Muslim). Amri ya Mtume(amani na rehe- ma ya Allah zimshukie) kumtaka mtuhuyoakamilishefungayake, ni ushahidi ya kuwa funga yake ni sa- hihi. Na Mtume, kukihusisha ki- tendo cha kulishwa au kunyweshwa na Allah Aliyetuka kwa mtu aliyesa- hau, niushahidimwinginewamtu huyo kutoadhibiwa juu ya suala hilo. Lakini atakapokumbuka kuwa yupo katika funga atajizuia na wala hatoendelea kula, na atakitema chakula kilichomo ndani ya mdomo wake wakati huo. Na, ni wajibu kwa mtu aliyem- uona mwenzake ambaye amefunga akila au kunywa mchana wa Mwezi wa Ramadhani kumtahadharisha, kwa kauli yake Allah Aliyetuka: “Na saidianeni katika wema na ucha- mungu,” (Qur’an, 2:2). Ibn Qayyim (Allah amrehemu) anasema: “Na katika muongozo wake Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie) ni kuondoa suala la kulipa swaumu kwa mtu aliyekula au kunywa kwa njia ya kusahau. Kwa kula na kunywa huku hakuege- mezwi kwa mhusika wa jambo hilo. Hivyo hakihesabiki kitendo hicho kuwa ni kufungua. Suala hili ni sawa na mtu aliyeku- la au kunywa akiwa amelala using- izini kwani hakuna ukalifishaji wa hukumu yoyote kwa kitendo kina- chofanyika kwa njia ya kulala using- izini au kwa kusahau, ” (Taz: ‘ Zaadulma’ad’ 1/338). Msafiri Sharia ya Kiislamu inampa ruhusa ya kula mchana wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani msafiri ambaye Mwezi wa Ramadhani umemjia akiwa safarini, au mtu ambaye safari ilimzukia katikati ya mweziwaRamadhani. Mandiko ya kisharia yaliyotoa ruhusa hiyo, kwanza, Kitabu Ki- takatifu cha Qur’an: ”Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyingine,” (Qur’an, 2:184). Hili ni andiko la wazi linalobainisha ruhusa ya ku-

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close