Uncategorized

Ubora Wa Kufunga siku zita za mwezi wa Shawwali

Kufunga siku sita za Mwezi wa Shawwali (Mfungo Mosi) baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Sunna iliyo- pendekezwa na sharia na wala si jambo la Wajibu. Hata hivyo, funga hii fadhila na malipo makubwa.

Ubora na fadhila hizi zimethibit- ishwa na Hadithi Sahihi ya Mtume (rehema na amani za Allah zimshuk- ie) iliyopokewana Swahaba Abu Ayyub al-Answari (Allah amridhie). Mtume amesema: “Mtu aliyefunga mwezi wa Ramadhani kisha akafua- tisha kufunga siku sita za mwezi wa Shawwali, malipo yake anakuwa ni kama mtu aliyefunga dahari yaani milele,” (Muslim). Faida nyingine inayopatikana ka- tika kufunga siku sita za mwezi Shawwali ni kuziba mapengo na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa kufunga Ramadhani kwani mfunga- ji haachi kuwa na mapungufu au makosa ya kibinadamu yatakay- oathiri funga. Hivyo, Sunna huhesa- biwa ndio inayoziba mapungufu na mianya inayojitokeza katika ibada ya Faradhi. Hili linabainishwa na Hadithi ya Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) iliyopokewa na Abu Daud, ambapo Mtume amenukuli- wa kusema: “Hakika jambo la kwan- za kuhesabiwa Siku ya Kiyama kati- ka amali za mja ni swala tano za fara- dhi. Mola wetu Mlezi atawaambia Malaika wake, na huku akijua unda- ni wa jambo hilo, ‘Hebu zitazameni swala alizoswali mja wangu huyu zipo kamili au zina mapungufu nda- ni yake?”

“kama zikiwa timilifu, zitaandikwa kuwa zimekamilika.Na kama zikiwa na mapungufu katika baadhi ya utekelezaji wake.Allah atasema kuwaambia malaika wake, ‘Hebu tazameni kwa mja wanguhuyu,Je,kuna amali yoyote ya sunna aliyoifanya. Kama itakuwepo, Allah atasema, ‘Yakamilisheni ma- pungufu yaliyokuwepo katika fara- dhi yake kwa kujaza amali za Sunna. Kisha baada ya hapo, amali zote zi- tahesabiwa kwa mtindo huo”. Je, ipo ruhusa ya kuchagua siku za kufunga katika Sunna ya Shaw- wali? Hizi siku sita ambazo ni Sunna kufunga katika Mwezi wa Shawwali hazikuainishwa, bali Muislamu atachagua kufunga katika siku zozo- te katika Mwezi wa Shawwali ili mradi tu siku sita hizo ziwe ndani. Akitaka atazifunga mwanzo wa mwezi, katikati au mwisho wake na pia akitaka atazitenganisha au atazi- fuatisha. Sharia imetoa uwanda mpana ka- tika ibada hii. Sifa njema ni zake Al- lah Aliyetukuka. Lakini iwapo ata- harakisha kuzifunga mwanzoni mwa Mwezi wa Shawwali – yaani baada ya sikukuu tu kumalizika – ni bora zai- di. Kufanya hivyo kunaingia katika wigo wa kuyaendea haraka mambo ya kheri. Na anapozianza kuzifunga ni ruhusa kuziacha huko mbele, katika mwaka wowote. Si kweli wanavyodai baadhi ya watu kuwa ukianza kufun- ga Sunna ya sita hauruhusiwi kuacha. Kufunga siku sita za Shaw- wal ni Sunna wala si amali ya fara- dhi. Hata hivyo, kudumu katika ku- funga sita ni jambo timilifu na bora zaidi, kwani Mtume (rehema na am- ani ya Allah zimshukie) amesema: “Amali iliyo bora kwa mtu ni ile anay- odumu nayo hata kama ni chache.” Je, inaruhusiwa kufunga sita kab- la ya kulipa Siku za Ramadhani? Wanazuoni wa Sharia ya Kiisla- mu, (Fuqahau) wana mitazamo to- fauti katika shauri hili yaani, kama inaruhusiwa kufunga sita kabla ya kulipa Siku za madeni ya funga ya Ramadhani. Na mtazamo ulio karibu na usa- hihi ni kwamba inaruhusiwa kwanza kulipa siku zilizokupita katika mwezi wa Ramadhani, kisha baada ya hapo ufunge Sunna ya sita, kwa ushahidi wa Hadithi ya Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie): ”Mtu ali- yefunga mwezi wa Ramadhani kisha akafuatishia na kufunga siku sita za Shawwali, anapata ujira wa malipo ya mtu aliyefunga milele,”(Muslimu) Na mtu aliyeanza kufunga sita kwanza na akaacha kulipa siku ali- zoziacha katika Mwezi wa Ramad- hani, anakuwa hajafuatisha Mwezi wa Ramadhani, isipokuwa amefua- tisha baadhi ya siku za Ramadhani. Na Mtume amesema: “Aliyeufunga Mwezi wa Ramadhani,” kwa maana ya kukamilisha siku zake. Sio hivyo tu, suala la kuzilipa siku za Ramad- hani ni la wajibu, na kufunga sita ni jambo la Sunna. Ilivyo ni kuwa, fara- dhi ni bora zaidi kuitilia maanani na kuipa kiapaumbele kuliko Sunna. Allah ndiye mjuzi zaidi wa hili.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close