Uncategorized

Siri ya Laylatul Qadr

hizi hapa Fadhila za siku 10 za Mwisho wa ramadhani

Siku kumi za mwisho wa Ra- madhani ni siku zenye fadhila kubwa kwani imepokewa Ha- dithi na mama ‘Aisha (Allah awe radhi naye) “Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa akijipin- da siku kumi za mwisho wa Ra- madhani kuliko siku nyingine” (Muslim, Na. 1175).

Kujipinda huku ni katika kufanya ibada kwa wingi na miongoni mwa ibada alizokuwa akikithirisha kuzifan- ya katika kumi la mwisho ni ibada ya Itikafu na kisimamo cha usiku. Im- eripotiwa Hadithi kwamba “ Miongo- ni mwa mambo aliyoyafanya ni ku- jitengakwaitikafunakutafutaLaylatul Qadr,” (Bukhari, Na. 1913; Muslim, Na. 1169). Naye mama ‘Aisha (Allah awe radhi naye) anasimulia: “Siku kumi za mwisho za Ramadhani zilipoingia, Mtume alikuwa akikesha usiku mzi- ma, akiwaamsha watu wa familia yake na kukaza kikoi chake,” (Bukhari, Na. 1920; Muslim, Na. 1174). Kukaza kikoi chake ni lugha ya kuashiria kwamba alikuwa akijitenga na wake zake kwa kutokufanya jimai. Kukesha usiku mzima ina maana kukesha akifanya ibada mbalimbali kwani mama Aisha (Allah awe radhi naye) anasimulia: “Sikupata kumuona Mtume akiisoma Qur’an yote au kuke- sha usiku akiswali mpaka asubuhi au akifunga mwezi mzima isipokuwa ka- tika Ramadhani” (An-Nasai, Na. 1641). Kwa hiyo tunaona jinsi Mtume wa Allah (rehema na amani ya Allah zimshukie) alivyokuwa akijihimu na ibada katika kumi la mwisho la Ram- adhani na jinsi alivyokuwa akiwaam- sha watu wa nyumba yake kwa ajili ya ibada. Hivi ndivyo tunavyopaswa ku- fanya katika kumi la mwisho la Ram- adhani. Ile kujua kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa akifanya hivi kuonesha fadhila la kumi la mwisho la Ramadhani kwani alizipa umuhimu mkubwa siku hizi kumi ki-asi cha kujipinda hivyo. Muislamu anapaswa kumfuata Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) kwani ndivyo Allah Taala alivyotuelekeza aliposema:“Na hakika mmekuwa na kiigizo chema kwa mtume wa Allah kwa yule mwenye ku- taraji kukutana na Allah na siku ya mwisho.” Hizi ni siku za mwisho wa Rmadhani na huenda tusije kukutana nazo tena maishani mwetu kwa hiyo tujipinde katika ibada kama alivy- okuwa akifanya Mtume wa Allah.

Usiku wenye Cheo

Miongoni mwa fadhila za siku kumi za mwisho za mwezi wa Ramad- hani ni usiku wenye cheo au Laylatul Qadr. Usiku huu ndiyo usiku ambao Qur’an iliteremshwa yote kutoka Lawhul Mahfuudh (Kitabu kilichoko mbingu ya saba) kuja Baytul ‘Izza kati- ka mbingu ya kwanza ya dunia na ndi- yo ten akikaanza kuteremshwa kidogo kidogo kwa Mtume kwa muda wa mi- aka ishirini na tatu (Tafsir Ibn Kathir, 4/529). Allah Taala anazungumzia tukio hili aliposema: “ Hakika sisi tumeki- teremsha (kitabu hiki) katika usiku wenye baraka, hakika tumekuwa ni wenye kuwaonya binadamu. Ndani yake hugawanya kila amri zenye huk- mu,” (Qur’an, 44:2-3). Allah ameuita usiku wenye cheo kuwa usiku wenye baraka na kwamba ndani yake hugawiwa kila amri. Mas- wahaba , akiwemo Ibn ‘Abbas, Qata- dah, Saiid ibn Jubayr, ‘Ikrimah, Mu- jaahid na wengineo wanasema usiku ambao Qur’an ilipoteremshwa ni Laylatul Qadar. Ni katika usiku huu ndipo amri mbali mbali kuhusu mambo ya vi- umbe kama vile umri, nani atakufa, nani ataokolewa, nani ataangamia, nani ataingia peponi, nani ataingia motoni, wapi ukame na njaa itatokea na kila jambo ambalo Allah anataka kwa viumbe wake hupitishwa. Ndiyo maana usiku huo unaitwa Laylatul Qadar kwani qadar mbali mbali za viumbe hupitishwa usiku huo hivyo kukutwa ukiwa unafanya ibada huvuta huruma ya Allah kama ilikuwa shari ya qadar ilikuwa ikukute na kama ni kheri ya qadar basi ikuthibi- tikie. Allah ameuita usiku huo “Laylatul Qadr” kutokana na thamani ya kile kilichotokea usiku huo kwa kush- ushwa Qur’an na kutolewa amri juu ya qadar za viumbe. Abu Hurayrah (ra- dhi za Allah ziwe juu yake) anasema Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie), alisema “Yeyote abakiae macho katika usiku wenye cheo kwa imani na kwa kutaraji malipo kwa Al- lah, madhambi yake yaliyopita yat- asamehewa,” (Bukhari, Na. 1910; Muslim, Na. 760).

Allah ameipa Laylatul Qadr Hadhi Kubwa

Allah ameupa usiku wenye cheo hadhi kubwa kiasi kwamba anasema katika Qur’an: “ Laytul Qadr ni bora kuliko siku elfu moja. Huteremka ma- laika na Jibril ndani yake kwa idhini ya mola wao na kila amri” (Qur’an, 97:3-4 ).Malaika wengi hushuka usiku huo kwa kuwa ni usiku wenye baraka ny- ingi, wakishuka kila mahali ambapo Qur’an ikisomwa na mahali panapo- fanywa dhikr (kisheria) huwafunika kwa mbawa zao wenye kufanya ibada mbalimbali (Tafsir Ibn Kathir, 4/531). Usiku huu Allah ameuita usiku wa amani mpaka Alfajiri. Ni salama na amani duniani na mbinguni. Kwa mu- jibu wa Mujaahid (Allah amrehemu), shetani hawezi kusababisha madhara yoyote kwa nafsi ya Muumini usiku huo (Tafsir Ibn Kathir, 4/531). Usiku huu kuwa bora kuliko miezi elfu moja ni kuvuta hisia zetu tujue thamani ya usiku huu. Inakuwaje usiku huu mmoja tu uwe sawa na mia- ka 83 na miezi mitatu? Hakuna ajuaye isipokuwa Allah pekee. Ukweli huu unamhamasisha Muu- mini kujipinda kwa ibada usiku ili ap- ate fadhila zake kama alivyokuwa aki- fanya Mtume wa Allah (rehma na am- ani ziwe juu yake). Kilicho sunnah ka- tika kumi la mwisho ni kufanya itikafu msikitini.

Ni siku gani Laylatul Qadr hupatikana?

Ibn Umar (Allah awe radhi naye) alisema Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) alisema: “Tafuteni Laylatul Qadr siku kumi za mwisho za Ramadhani” (Muslim, 2/823). Kuhu- su ni siku gani, Mama Aisha (Allah amridhie) alisema Mtume alisema: “Itafuteni Laylatul Qadr siku witri za kumi la mwisho,” (Bukhari, 4/259). Siku hizo ni usiku wa mwezi 21, 23, 25, 27 na 29 kwa kuzingatia kwamba siku ya Kiislamu huanza jua linapoza- ma. Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah al- isema: “Inapaswa kutafutwa usiku wa 21, 23, 25, 27 na 29 au kwa kile kili- chobakia kwani Mtume alisema pindi zikibaki siku 9, au siku 7, au siku 5 au siku 3. Kwa msingi huu, kama mwezi una siku 30 kwa hiyo Muumini ana- paswa kuitafuta Laylatul Qadr siku zote kumi za mwisho wa Ramadhani,” (Fatawa Ibn Taymiyyah, 25/284, 285) Dalili za Laylatul Qadr Wapo waislamu wanaoamini kwamba Laylatul Qadr ni kitu fulani hivi kama nyota. Wengine hudai kuwa wameiota laylatul Qadr. Kule kuota maana yake mtu huyo alikuwa amela- la wakati anatakiwa kujipinda kwa ibada. Neno ‘Laylah’ kwa Kiswahili maana yake ni usiku. Kwa hiyo ni usiku na si vinginevyo. Ama dalili zak- wamba usiku huo utakuwa umepa- tikana, ziko Hadithi kadhaa juu ya hili. Dalili ya Kwanza; Ubayy ibn Ka’ab (Allah amridhie) alisema: “Mtume ali- tangaza kwamba moja ya dalili zake (Laylatul Qadr) ni pale jua lilipocho- moza asubuhi likiwahalina miale mi- kali” (Muslim, Na. 762). Dalili ya Pili; Ibn Abbas (Allah awe radhi naye) Mtume alisema “Laylatul Qadr ni usiku tulivu, hauna joto wala baridi na asubuhi inayofuata jua linachomoza likiwa dhaifu,” (Ibn Khuzayyima, Na. 2912). Dalili ya Tatu; Imesimuliwa na A-Twabarany Mtume amesema: “Laylatul Qadr ni usiku angavu, hauna joto wala baridi na hauna vimondo vinavyoonekana,” (Al-Kabir, Majma’ al-Zawa’id, 3/179). Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Muumini ajipinde tu kwa ibadahatakamahatajuakama amei- pata Laylatul Qadr. Yawezekana kabi- sa yule anayedhani kuwa ameipata asiwe ameipata na yule anayedhani kuwa hakuipata akawa ameipata. Hii ni tawfiki ya Allah humpa anayejitahi- di namna apendavyo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close