Uncategorized

ramadhan, mwezi wa mashujaa

“Ewe Mwenyezi Mungu! Kikundi hiki leo kikishindwa, basi hutaabudiwa tena.” Hayo yalikuwa maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ya Allah imshukie) , wakati aliposimama mbele ya Mola wake, usiku wa Ijumaa moja huku akiinua mikono yake juu, akilia, akiomba dua ya ushindi kwa umma huu!

Mtume wa Mwenyezi Mungu al- ihangaika sana, machozi yake hay- akusimama, dua zake hazikukoma, mpaka joho lake likaangukia mabe- gani na Abubakar (radhi za Allah zimshukie), Swahaba wake wa kari- bu zaidi, akimpa matumaini kwamba Allah ‘Azza wa Jalla’ hawezi kukataa dua zake. Lakini huo haukuwa usiku wa kawaida na hapo pia hapakuwa ma- hali pa kawaida. Huo ulikuwa ni usiku wa mwezi 17 wa Ramadhan na dua hiyo ilikuwa ikiombwa kwenye Bonde la Badr, usiku wa kuamkia Vita vya Badr, moja ya vita muhimu sana kuwahi kupiganwa na Waislamu. Wakizidiwa idadi kwa kiasi kikubwa na jeshi lenye silaha bora, Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie) na Waislamu walifanya kila walichoweza, ikiwa ni pamoja na kuomba dua kabla, wakati na baada ya vita hiyo. Kutokana na re- hema zake zisizo na kikomo, Allah ‘Azza wa Jalla’ akawapa ushindi am- bao hautasahaulika. Waislamu 313, farasi wawili na ngamia 70 wamelishinda jeshi la watu 1000, likiwa na farasi 100 na ngamia 700! Hicho ndiyo kipimo cha ushindi ambapo vivumo vya ‘Allahu Akbar’ na ‘Ahad’, ‘Ahad’ (Mwenyezi Mungu ni Mmoja) vimeendelea kuvuma mpaka leo, na athari za ushindi ule zinaendelea kutikisa dunia. Ukumbusho wa kudumu wa ushindi huu umehifadhiwa kwa ajili yetu ndani ya Qur’an Tukufu, pale Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ali- posema: “Na hakika Mwenyezi Mungu alikunusuruni katika Badr hali ninyi mlikuwa dhaifu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru. Ulipowaambia Wau- mini, ‘Je? haitakutosheni ikiwa Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa’”? (Qur’an, 3:123-124) . Vita vya Badr viliimarisha zaidi imani ya Waislamu na ilikuwa ni ‘ushindi wenye kuamua’, ambao ul- isambaratisha kabisa majeshi ya adui na kusimamisha Dola mpya Madina, kama nguvu ya kiroho, ki- siasa na kijeshi ya Waislamu. Isisa- haulike kwamba huo ndiyo umuhimu wa vita ile ‘yenye kuamua’ (decisive battle) . Kama isingekuwa ujasiri, kujitoa muhanga, kupoteza viungo na mai- sha ya wale Maswahaba Watukufu waliobarikiwa siku ile, basi leo tus- ingekuwa hapa kama Waislamu. Huo ndiyo Mwezi wa Ramadhani wakati wa Mtume (rehema na ama- ni ya Allah imshukie) . Ilikuwa ni kipindi cha utakaso, kuamrisha mema, kukataza maovu na kujitolea kwa hali na mali kuli- fanya neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu. Mtume (rehema na ama- ni ya Allah imshukie) na Maswa- haba wake (Allah awaridhie) wamepita pamoja Ramadhan tisa baada ya Hijra. Ramadhan hizo zili- jawa na matukio mengi yenye kua- mua, ambayo yamefinyanga mwele- keo wa historia ya dunia.

Kukombolewa Makka

Tunapaswa kujua kwamba ili- kuwa ni katika mwezi huu mtukufu wenye malipo mengi, ilipofika Ram- adhan 20 mwaka wa 8 AH, kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah imshukie) alirejea Makka akiwa siyo mtawaliwa tena, bali kama mtawala katika tukio la kuikomboa Makka (Fat’hu Makkah). Mtume (rehema na amani ya Al- lah imshukie) aliiweka Makka chini ya Mamlaka ya Uislamu kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Uislamu, bila mapigano. Aliingia Makka na kuwahudu- mia watu kwa haki. Alikwenda yeye mwenyewe mpaka kwenye Kaaba, akayanyooshea masanamu fimbo yake huku akisoma Aya hii ya Mwenyezi Mungu: “ . . Ukweli ume- fika, na uongo umetoweka. Hakika uongo ni wenye kutoweka tu!” (Qur’an, 17:81) Baada ya hapo, masanamu yote likiongozwa na Sa’ad bin Abi ambayo Makureishi walikuwa waki- yaabudu yakaanguka moja baada ya jingine, na kisha yakatiwa moto na kuvunjiliwa mbali. Kwa hiyo, Makka yote ikakombolewa na zama za kuabudu masanamu kama Uzza, Suwa na Mannata zikafutika rasmi siku ile. Baada ya kifo cha Mtume (rehe- ma na amani ya Allah imshukie), Waislamu waliendeleza sunna hii na Allah ‘Azza wa Jalla’ aliwatumia Waumini kuathiri mkondo wa his- toria. Mantiki inaweza kukwambia kwamba kupigana wakati umefun- ga inaleta hasara, lakini imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu ku- navuka mantiki hiyo mbovu.Utaona kwamba, hakuna mwezi ambao umeshuhudia mapigano mengi zaidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kupata mafanikio makubwa na ushindi wa Uislamu kama mwezi wa Raamadhani.

Vita vya Al-Qadisiyyah

Katika mwaka wa 636CE, sawa na mwaka 15AH, ndani ya mwezi wa Ramadhani,jeshi la waislamu

likiongozwa na Sa’ad bin Abi

Waqqas (Allah amridhie) , akiwa na askari 30,000 miongoni mwao wakiwemo zaidi ya Maswahaba 700 na zaidi ya maveterani 70 wa Vita vya Badr, walikwenda kukabiliana na jeshi la Waajemi (Persian) katika eneo la Qadisiyyah.

Waislamu walikuwa wameingia sehemu kubwa ya himaya ya Waaje- mi. Vita hii ndiyo iliyofungua milan- go ya kuanguka kwa dola kubwa ya Waajemi. Jeshi la Waajemi lilikuwa kubwa na lenye nguvu, likiwa na idadi ya askari wanaofikia 100,000, wakisaidiwa na tembo wakubwa waliovishwa makoti na meno yao yakivishwa vitambaa vya hariri.

Jeshi la Waislamu lilionekana kuwa duni lakini kile walichokosa katika rasilimali, walikifidia kwenye imani yao madhubuti na dhamira isiyoyumba.

Kwa hiyo, uwanja wa mapambano ukaandaliwa kwa ajili ya majeshi haya mawili yanayotisha.Baada ya waislamu kuzidiwa, swahaba mkubwa Qa’qa bin Amr (Allah amridhie), ambaye awali alipelekwa Syria, akaingia kwenye uwanja wa mapambano. Shujaa huyu wa Kiislamu aliingia kwenye uwanja wa mapambano kwa sauti kubwa ya “Allahu Akbar” ambayo kwa haraka sana ikainua morali ya Waislamu. Wapiganaji wa Kiislamu walimjua vizuri sana Qa’qa ( Allah amridhie). Yeye peke yake alikuwa sawa na jeshi zima. Abubakr (Allah amridhie) alipata kuzungumza maneno haya kuhusu Swahaba huyu: “Hakuna jeshi li- naloweza kushindwa kama litakuwa na watu kama huyu.” Qa’qa bin Amr (Allah amridhie) aliwaangusha tembo wale wakubwa kama vile kumbikumbi na kufuatia hali hiyo, kamanda mkubwa wa Kiajemi Rustum akafutika kutoka kwenye kurasa za historia. Kabla hata damu haijakauka kwenye mabonde ya Qadissiyyah, Kamanda Sa’ad bin Abi Waqqas (Al- lah amridhie) akamuandikia barua Khalifa, Umar al Khattab (Allah amridhie) akisema: “Lo, Allah amet- upa ushindi dhidi ya Waajemi. Wais- lamu wamekutana na idadi ambayo wasimuliaji hawajawahi kusikia, la- kini idadi yao haikuwa na maana kwao na Allah akawapa Waislamu vile walivyomiliki.” (Tabari) .

Ugiriki

Katika Ramadhan ya mwaka 31AH, Waislamu wakiongozwa na SwahabaMu’awiya(Allahamridhie) walikishinda kisiwa cha Wakristo cha Rhodes, wakivunjilia mbali san- amu kubwa zaidi wakati ule duniani ‘The Colossus of Rhodes’ ambalo lili- pewa jina la Mungu wa Kigiriki ali- yeitwa Helios. Hilo lilikuwa ni sanamu lenye urefu wa futi 110 lililowekwa kwenye kitako cha urefu wa futi 50 za ‘mar- ble’ nyeupe karibu na lango la kuin- gilia bandari ya mji huo. Vita hii ilikuwa kali sana ambapo imeelezwa kwamba hata kama ndege angetaka kukatiza juu ya uwanja wa mapambano kwenda upande wa pili, asingeweza kutoka- na na jinsi mapanga yalivyokuwa yakiunguruma na mishale ilivyoru- ka. Lazima angekatwa vipande vi- pande.

Uhispania

Mpaka mwaka 92 AH, Uislamu ulishaenea mpaka Afrika ya Kaska- zini, Uajemi na Sham. Uhispania au Andalusia kama ilivyojulikana wakati ule ilikuwa chini ya utawala dhalimu wa Mfalme Roderic wa Visigoths ambaye aliwakandamiza, kuwanyanyasanakuwafungaMaya- hudi na Wakristo. Kwa mujibu wa wasimuliaji wa historia, Mkuu wa Wakristo aliyeit- wa Julian ambaye aliikimbia Uhis- pania, aliwaomba Waislamu wam- saidie wakati akiwa mwambao

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close