Uncategorized

Mauaji ya Manchester, Waislamu wajibu vipi!

Ukweli ni kwamba mauaji ya kutisha yaliyotokea kwenye mji wa Manchester nchini Uingereza wiki iliyopita, yana- paswa kutukumbusha kwamba umwagaji damu na ukosefu wa usalama duniani, unatokea kati- ka kipindi hiki ambacho ulim- wengu umedhibitiwa na madola ya kibeberu. Kile kilichoonekana kuusibu ulimwengu wa Waislamu kila siku, kwa kipindi cha miaka 17 il- iyopita, sasa kwa huzuni kubwa, kinaonekana kutokea mara moja moja nchini Uingereza na barani Ulaya. Idadi ya wanaouawa inaweza isiwe kubwa sana, lakini bila sha- ka hofu imetawala na hilo linaonekana wazi. Wanasiasa wa Ulaya wanawe- za kuzidisha hatua za usalama, lakini kwa huzuni kubwa, haku- na kitakachobadilika kwa kuwa hawako tayari kukubali visababi- shi halisi vya ‘ugaidi’ duniani, ambavyo ni ukandamizaji wa watawala dhidi ya raia wao wa- naopigania haki. Sera za mabeberu katika nchi nyingine, nazo zimevuruga ama- ni ya dunia kwa miongo kadhaa. Waislamu nchini Uingereza na maeneo mengine ya dunia wa- naweza kulaani vikali matukio ya kikatili kama hayo, lakini hilo lisitufanye kubadili mfumo wetu wa maisha ya Kiislamu ambao unapigwa vita na wanasiasa wa Ulaya, kila matukio kama hayo yanapotokea. Wanapiga kelele kwa nguvu sana wakifichua migongano ya njia za maisha za mabeberu katika haki na maadili wanayojifanya kuyasimamia.

Waislamu wanapaswa kuuwasilisha Uislamu kama ufumbuzi na siyo kuruhusu dini hii nzuri ya Mwenyezi Mungu kushambuli- wa. Wakati Uislamu ulipokuwa ndiyo msingi wa kitaaluma na maisha ya kisiasa katika ulim- wengu wa Waislamu, dunia ili- shuhudia ustaarabu ulioweza ku- jenga jamii njema, ambapo haki na usalama ilikuwa ni kwa raia wote. Teknolojia na elimu vili- shamiri kwa kiasi kikubwa na historia ni shahidi wa hilo. Na tangu eneo hilo la ulimwengu lilipokaliwa na wakoloni, basi matokeo yake yamekuwa ukosefu wa utulivu, usalama na kuwepo hali ya kukata tamaa. Waislamu wanapaswa kuishi- ka kikamilifu dini yao (mfumo wa maisha) na mara zote kuzun- gumza lile lililo sawa na dhidi ya ugaidi wote duniani – siyo kucha- gua matukio maalumu ya kigaidi, kama yanavyoangaziwa na vyo- mbo vya habari vya Magharibi. maye utavunjilia mbali mitazamo ya kisiasa mingine kama uiivyo duniani hivi sasa. Mtazamo huo wa haki unahi- tajika sana, na unapokosekana, basi vurugu, dhulma na umwa- gaji damu havitakoma. Ujumbe muhimu kwa Waisla- mu ni kwamba ingawa wanach- ukizwa na dhulma na umwagaji damu unaofanywa na mataifa ya Magharibi katika nchi zao ni kwamba, tofauti na nchi za Ma- gharibi, Waislamu kamwe hawa- chukui maisha ya wasio na hatia ili kufikia malengo ya kisiasa. Mauaji yanayofanywa na mataifa ya Magharibi yanawau- dhi Waislamu na wasio Waisla- mu duniani kote. Hata hivyo, kitendo chochote ambacho Muislamu anakifanya lazima kiwe katika Sharia – Uislamu Uislamu hausemi kwamba mauaji ya kutisha ndiyo njia ya kubadilisha hali. Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ya Allah im- shukie) ameleta methodolojia ya mabadiliko ambayo ni harakati za kisiasa na kifkra kwa kuzinga- Waislamu wanapaswa ku- jichanganya kwenye jamii pana zaidi na kufafanua kwa usahihi Uislamu kuanzia imani, maadili na mtazamo wake kama mbadala tia muundo aliouweka. Njia nyingine zote hazina tija na hati- maye zitatuingiza motoni. Ni jambo la kushangaza sana, baada ya mashambulizi ya kuti- sha kama ya Manchester, Uisla- mu ndiyo unaolaumiwa kama sababu ya mashambulizi hayo. Wale wanaohojiwa kwenye vyo- mbo vya habari wanalazimisha kwamba viongozi wa Waislamu Uingereza wanapaswa kufanya zaidi katika ‘ kulaani’ matukio haya! Kwanza, hata kuwataka tu Waislamu kulaani matukio kama hayo ni kuwatukana kwa sababu ni sawa na kuhoji hisia zao za kib- inadamu dhidi ya wengine, uki- watarajia kuzithibitisha zaidi ku- liko watu wengine. Waislamu hawahitaji kujiun- ga katika namna hiyo ya kulaani. Hiyo ni sehemu ya ajenda ya ki- siasa ya kuipaka matope jamii ya Waislamu, dini yao na kuondoa mazingatio ya watu kwenye uk- weli halisi wa kinachotokea. Dini ya Kiislamu inawataka Waislamu kufuata kile tu Allah ‘Azza wa Jalla’ na Mtume wake (rehema na amani ya Allah im- shukie) walichoamrisha. Ni har- uhai wa asiye na hatia. Hakuna jamii inayopaswa kuhisi inahitaji kuomba msama- ha kwa majanga ambayo hawakuyaanzisha, kushawishi wala kuyatekeleza. Kutarajia fa- milia za Waislamu, ndugu na jamaa zao, kuomba msamaha kwa vitendo kama hivyo, siyo haki na ni hatua inayolenga ku- leta lawama za jumla. Wakati Mbunge wa Batley nchini Uingereza, Jo Cox alip- ouawa na kijana wa kizungu ali- yehamasishwa na mawazo ya ki- fashisti yenye msimamo mkali, vyombo vya habari nchini humo havikuwataka Waingereza wote weupe kuomba msamaha. Mwa- namke anaposhambuliwa na mwanaume, hakuna anayetarajia wanaume wote waombe msama- ha kwa uhalifu huo! Wakati nchi za Magharibi zi- napoendesha vita katika eneo la Mashariki ya Kati, zikiangamiza maisha ya maelfu ya watu na ku- wafanya wengine kuwa wakim- bizi, hakuna serikali hata moja ya nchi hizo iliyoomba radhi kwa unyama huo – ingawa unawagusa moja kwa moja. Kwa hiyo, ni wazimu kuwata- ka Waislamu waombe radhi kwa kile kilichotokea Manchester. Ki- nachohitaji kuchunguzwa ni sababu halisi ya maangamizi haya na umwagaji damu unaoen- delea kutokea duniani. Uislamu siyo unaotawala dunia hivi sasa isipokuwa itikadi ya mabeberu wa Magharibi ndiyo inayotawala. Wao ndiyo wanaosababisha maa- fa hayo na mjadala unapaswa kuanzia na kuishia hapo, badala ya kuhamisha ajenda na kuondoa mazingatio ya walimwengukwenye ukweli halisi.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close