Uncategorized

masheikh walivyoumizwa na kifo cha Kitwana Kondo

Masheikh, maimamu na wa- nazuoni wa Kiislamu wameelezea walivyoguswa na watakavyomkumbuka Meya wa zamani wa Dar es Salaam, Kit- wana Selemani Kondo, maarufu kama KK, aliyefariki hivi karibuni.

Viongozi hao wa Kiislamu wamesema kifo cha KK ni pigo kubwa kwa Waislamu na Watan- zania ambao aliwatumikia vema enzi za uhai wake.

Amiri wa Baraza Kuu na Ju- muiya na Taasisi za Kiislamu nchi- ni, Sheikh Mussa Kundecha alise- ma ameelezea kifo cha KK kuwa ni msiba mzito kwa Waislamu, kwani alikuwa mtetezi mkubwa wa haki za wanyonge, hususan Waislamu

“Nilipokamatwa, Kitwana Kondo alisimama kidete kutaka kujua kwa nini na kuhakikisha haki inafuatwa,” alisema Sheikh Kundecha. Pia, Sheikh Kundecha aliwataka viongozi wengine Wais- lamu walioko Serikalini waige mfano wa Kitwana Kondo katika kuitetea dini yao, pale inapotakiwa kufanya hivyo.

Naye, Mwenyekiti wa The Is- lamic Foundation (TIF) Aref Nah- di, alisema Kitwana Kondo ameacha pengo kubwa katika jamii ya Kiislamu. “Kifo chake kimeleta mshtuko mkubwa sana kwa jamii ya Kiislamu, ameacha pengo kubwa na sioni wa kuliziba haraka,” alisema Nahdi.

Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda alimuelezea Kitwana Kondo kama mtu aliyesimama imara kupigania haki za Waislamu, ikiwemo ya yeye mwenyewe Ponda.

“Nakumbuka enzi za Mwem- bechai, Makamu wa Rais wakati huo aliagiza nikamatwe nikiwa hai au mfu, Kitwana Kondo alinionge- lea Bungeni kwa ujasiri mkubwa licha ya mazingira magumu ya wakati huo,” alisema Sheikh Pon- da.

Naye Imamu wa msikiti wa Mtambani, Sheikh Selemani Ab- dallah alisema kuwa Kitwana Kondo hakuuficha Uislamu wake akiwa serikali.

“Nimepokea taarifa za kifo chake kwa huzuni na masikitiko makubwa…Kitwana Kondo ni miongoni mwa viongozi wa Seri- kali ambao waliuweka mbele Uis- lamu wao,” alisema Sheikh Abdal- lah.

Kwa upande wa Profesa Ibra- him Haruna Lipumba, anamuan- galia Kitwana Kondo kama mtete- zi wa maslahi ya Uislamu ndani na nje ya Bunge.

“Kitwana Kondo alikuwa akisi- mama bungeni kutoa hoja, wabunge wote wanamsikiliza. Ali- pigania haki za Waislamu ikiwemo kuanzishwa kwa Chuo cha Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM),” alisema Profesa Lipumba.

Licha ya kupigania dini, pia kwa mujibu wa Profesa Lipumba vilev- ile Kitwana Kondo alijitoa kwa hali na mali kupigania uhuru wa Tanganyika.

“Kitwana Kondo alikuwa polisi enzi za ukoloni na alitoa mchango mkubwa kwa chama cha TANU enzi za kupigania uhuru,” alisema Profesa Lipumba. na kuongeza:

“Enzi za uasi wa kijeshi mwaka1964,Marehemu Kitwana Kondo ndiye al- iweka ulinzi ili kuhakiki- sha Nyerere hadhuriki.”

Mratibu wa Hijab Taifa, Shabani Ali Shaba- ni kwa upande wake al- isema kuwa Kitwana Kondo alikuwa Mbunge pekee wa kwanza Tanza- nia kupigania wanawake wa Kiislamu waruhusiwe kuvaa hijab serikalini, shuleni na ofisi zingine.

Shabani alisema: “Jitihada za Kitwana Kondo hatimaye zilipele- kea Rais Ali Hassan Mwinyi kutoa waraka mwaka 1995 na ul- ioruhusu wanafunzi wa shule na vyuo kuvaa hi- jab.”

Kwa upande wake Dk Ramadhani Dau aki-
andika kwenye mitandao ya kijamii alimsifu Kitwana Kondo kama mtu jasiri na aliyepigania mambo aliyoamini kuwa ni sahihi na yenye manufaa.

“Moja kati ya sifa zake nyingi ni ujasiri. Mzee Kitwana Kondo hakuwa mwoga na alisimamia jambo ambalo anaamini ni sahihi na lina manufaa kwa nchi yetu. Mifano iko mingi…alisimamia su- ala la upatikanaji wa chuo cha MUM Morogoro kwa kujenga hoja kwa Rais wa wakati huo Ben- jamin William Mkapa mpaka Rais akashawishika kuwa ni jambo jema kuanzishwa kwa chuo hicho kwenye majengo ya kilichokuwa Chuo cha Mafunzo cha TANESCO,” aliandika Dkt Dau.

Dkt. Dau aliendelea kuandika: “Kama kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango wa kipekee uli- opelekea upatikanaji wa chuo MUM mtu huyo ni Mzee Kitwana Kondo. Kwa kuenzi jitihada zake hizo, na kwa kuzingatia mzee Kon- do ni Mwenyekiti mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF), taasisi ambayo ndiyo mmiliki wa MUM, nashauri uon- gozi wa chuo utafute jengo lenye hadhi pale chuoni lipewe jina lake.”

Hotuba ya Mzee Kitwana Kon- do

Mwaka 1999, akiwa Bungeni Dodoma, Mzee Kitwana Kondo ambaye alikuwa Mbunge wa Kig- amboni aliainisha changamoto kadhaa zilizokuwa zinawakabili Waislamu na kutaka mamlaka husika zichukue hatua ili kuepu- sha mifarakano.

Ifuatayo ni sehemu ya hotuba yake hiyo aliyo- itoa bungeni.

“Mheshimiwa Spika, ninacho- taka kusema ni hiki cha umoja un- aotadhari sera, kauli, tabia na vi- tendo vinavyoweza kupanda mbe- gu za mfarakano. Nimesema mara

nyingi hapa kwako. Mheshimiwa Rais, hivi karibuni aliwahutubia Waislamu kwenye Baraza la Idd, akawaambia kwamba manung’uniko yao na malalamiko yao yote atayatazama na atayashu- ghulikia akishirikiana na baraza lake la mawaziri.

Sasa nina mambo mawili au matatu ambayo nataka kuyasema ambayo yanaweza kuleta mfar- akano. Yanapandwa na serikali. Moja, karibuni hivi katika Mwezi wa Ramadhani, mwezi wa Ram- adhani kwa Waislamu ni mwezi mtukufu, ni mwezi wa toba.

Wale jamaa zangu wasiojua toba ni mwezi wa kurudi kwa Mungu. Wakati wa ukoloni na mimi nilisoma wakati wa ukoloni mwezi wa Ramadhani shughuli zote zinafungwa, baadaye kwenye serikali yetu wenyewe shule hazi- fungwi. Lakini baada ya muda wa- naachiwa watoto kurudi majum- bani kwao au kwenda kwenye ma- bweni. Lakini mwaka jana na mwaka huu serikali ikaamua kuwa mitihani ya watoto wa kidato cha nne ifanywe Mwezi wa Ramadha- ni na iendelee mpaka siku za Idd. Hiyo ni moja ya cheche za mifar- akano.

Kwa rehema ya Mungu Alham- dulillah, baada ya kunung’unika Waislamu, Waziri wa Elimu na Utamaduni alitoa maelezo. Mael- ezo yale yakawaridhisha Waislamu na Mheshimiwa Rais akakubali kwa siku za Iddi, watoto wasifanye mitihani na haikufanywa mitihani. (Makofi)

Lakini mimi ninalouliza ile sababu ya kuamua Mwezi wa Ra- madhani ifanywe mitihani ni nini? Ni Insensitivity, ni jeuri, ni kiburi, kwa sababu kuna wengine ambao ni wazito tuliwasikia wakisema, wakitaka kufanya mtihani na wa- fanye hawataki basi. Mimi nasema watu kama hao ndiyo watu wasioi-

takia kheri nchi hii. Siyo sisi tunakuja kusema hapa hadharani. Hao wanaose- ma wakitaka kufanya na wafanye na hawataki ku- fanya basi. Hao ndiyo wa- sioitakia kheri nchi hii. (Makofi)

La pili, linaloweza ku- leta mfarakano ni tabia ya serikali ya kuchelewesha makusudi kuandikisha taasisi za Kiislamu. Taasisi yoyote ya Kiislamu ikitaka kuandikishwa serikalini it- achukua miaka miwili au mitatu. Sababu hazitolewi, hata kama kuna uchungu- zi,watuwaendewakatafute habari kwa nini inachukua miaka miwili, miaka mi- tatu?

Mheshimiwa Spika, nilipata kusema hapa kwamba mimi ni mlezi wa Baraza la Maimamu Tan- zania. Tumeomba Baraza la Maimamu kuandikish-

wa, sasa ni miaka mitatu, sababu haijulikani. Wengine kila wakiom- ba wanasema lazima kipatikane kibali toka BAKWATA. Leo nin- gependa nijue ipo sheria inayose- ma hivyo? Au ni matakwa tu ya wakubwa? Hilo la pili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu, Suraya33Ayaya30naya31ya Qur’an inamtaka mwanamke aki- fika umri wa miaka 9 avae hijab. Hijab maana yake avae nguo ya mikono mirefu, avae shungi, avae gwanda zuri na avae suruali inay- oficha mapaja na mpaka magoti. Mimi najua ya kwamba serikali imetoa agizo kwa watoto wa shule kwamba wafanyiwe hivyo wale wa Kiislamu wanaotaka, sheria zote zinavunjwa. Dini ya Kiislamu in- akataza pombe, Waislamu wana- kunywa pombe. Sasa hilo anafanya mwenyewe.

Lakini ninajua pia ya kwamba kuna shule nchini huku, kuna vi- ongozi wa Idara ya Elimu ambao wanakataa kutekeleza sheria hii au agizo hili na serikali imekaa kimya, nataka nijue ni kwa sababu gani? Tujue ni kwa nini. Hii ni amri ya Mwenyezi Mungu na serikali, Rais anasema tusifanye chochote kina- choweza kuleta mifarakano.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kwamba huu mwaka wa 30 wa uhuru. Siku ya Ijumaa ni siku muhimu kwa Waislamu kama ili- vyo kwa siku ya Jumamosi ni siku muhimu kwa Wasabato kama ili- vyokuwa siku ya Jumapili ni siku muhimu kwa Wakristo wengine.

Lakini siku ya Ijumaa ingawa kuna agizo la serikali kwamba Waislamu waachiwe waende wa- kasali. Kuna viongozi siku ile ndiyo siku ya kufanya ‘Board Meeting’, ili kumzuia Mkurugenzi ambaye ni Muislamu ambaye anapenda kazi yake aogope. Shule zinafungwa saa 7. Jumapili vitoto vidogo vidogo

vya Kikristo vinakwenda kusali. Jumamosi vitoto vidogo vidogo vya Kikristo vinakwenda kusali.

Siku hizi vitoto vidogo vidogo vya Kiislamu vinataka kwenda na wazazi wao. Naomba utaratibu ufanywe wa dhamiri kabisa kwamba Ijumaa saa 6 kazi basi kwa Waislamu. Wale wanaofanya ‘Board Meeting’ waache wafanye saa 8, wafanye saa 9 na shule zote za Primary na Sekondari zifungwe saa 6 ili kuwapa nafasi watoto wa Kiislamu waende wakasali.

Mheshimiwa Spika, nina men- gi lakini nitakuambia mwisho. La mwisho, Rais aliwaambia Waisla- mu wote pale Dar es Salaam kwamba atalishughulikia suala la elimu. Lakini akawashauri kwamba wale wafadhili ambao hivi sasa wanatujengea misikiti wajenge pia shule. Hilo jambo zuri, na Waislamu wamelisikia na nina- jua ya kwamba Waislamu wanata- ka hivi karibuni kumwendea Rais kwenda kumshukuru. Ila nina jambo moja, natoa mfano wa Dar es Salaam, Waislamu wanafikia asilimia 70 au zaidi. Kwenye mage- reza Dar es Salaam wengi kuliko Wakristo au watu wengine. Hawa wengi, hawana kazi, jela watakuwa wengi. (Kicheko)

Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waisla- mu. Asilimia 29 ni wengine. Wal- ioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 wal- ioshinda tena sema mwenyewe. Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asil- imia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21. Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu. Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga. Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwan- yanyua waliokuwa chini. Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua wal- iokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.

Mheshimiwa Spika, Rais Mka- pa anawasaidia Waislamu. Tulim- wendea, mimi mmojawapo kwa mambo mengi ambayo ameyashu- ghulikia. Nina hakika ya kwamba mambo haya tuliyoyasema na aliy- oambiwa na viongozi wa Kiislamu kule bungeni atayashughulikia. Lakini ninaamini kabisa ya kwamba hataweza peke yake bila ya msaada wa viongozi wangu hao walioko hapa. Wakisema hawa kwamba ndiyo kawaida yao hiyo. Atapata tabu Rais wangu.

Mheshimiwa Spika, kengele ya pili imelia. Nashukuru sana.

Lakini nataka niseme kwamba haya niliyoyasema, nasema kwa sababu najua mimi kwamba suala hili la mfarakano ni suala kubwa. Penye mfarakano hakuna maen- deleo. Penye mfarakano hakuna cha uchumi. Kwenye mfarakano kuna ghasia. Kwa kuwa Rais ame- omba tufanye kila jambo mfar- akano usiwepo, basi serikali imsai- die Rais katika kutekeleza wajibu wake kwa makundi yote ili pawepo na usawa. (Makofi).”

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close