Uncategorized

Makosa mbalimbali kwa wenye kufunga

Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wenye utukufu, mwezi ambao kheri zake zinakithiri kutokana na sifa zake za kipekee. Pamoja na hayo, kuna makosa ambayo baadhi ya watu huyafanya na kupelekea kutia dosari na kupunguza thamani ya funga zao. Ni vema kunasihiana ili tusitumbukie ndani ya dimbwi la makosa.

Imepokewa Hadithi kutoka kwa

Hudhaifa bin Yamaaniy (Allah amri- dhie) ambaye amesema: “Watu wa- likuwa wakimuuliza Mtume kuhusi- ana na kheri nami nilikuwa nikimu- uliza kuhusiana na shari kwa ajili ya kuogopa isinipate,” (Bukhari na Mus- lim).

Kwa hivyo ni vizuri kulijua jambo baya ili kuliepuka. Kwa sababu hiyo tunayazungumzia baadhi ya makosa wanayoyafanya watu ndani ya Ram- adhani, yakiwemo yale yaliyofunga- mana na funga yenyewe, swala ya Tarawehe, chakula na mengineyo ili tuweze kuyaepuka, yasipunguze tha- mani ya funga zetu au kuziharibu.

1. Kukosa Ikhlas

Katika muhimu na ya lazima katika dini ni Ikhlas (utakasifu wa nia). Hakuna jambo lolote la litakalokuwa sahihi pasi na masharti mawili kutim- ia, Ikhlas (utakasifu wa nia) na Mutaaba’a (kufuata utaratibu ulio- wekwa kisharia).

Kukosekana moja kati ya mawili hayo kunapelekea ibada kuharibika. Ikiwa ibada itafanywa kwa ikhlas bila kufuata muongozo wa kisharia, ibada hiyo haitasihi. Na iwapo itafanywa kwa mujibu wa sharia lakini ikakosa ikhlas, vilevile ibada hiyo itaharibika.

Kinyume cha Ikhlas ni ria. Ikhlas hukosekana katika ibada ya funga kwa namna mbalimbali ikiwemo kufunga kwa mazoea, kuogopea kuwa watu watakusema vibaya au kuwaridhisha watu kutokana na maslahi fulani ya kilimwengu.

Allah Aliyetuka anahimiza Ikhlas katika ibada aliposema: “Nao hawak- uamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike sala,na watoe zaka. Na hiyo ndiyo

madhubuti,” (Qur’an, 95:5).
Mtume (rehema na amani za Allah

zimshukie) amehimiza Ikhlas katika funga aliposema: “Atakayefunga Ra- madhani kwa Imani na kwa kutegem- ea malipo kutoka kwa Allah, basi mtu huyo atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia,” (Bukhari na Muslim).

Pia Mtume amesema: “Huenda mfungaji akawa hakupata chochote katika funga yake isipokuwa njaa na kiu na huenda mwenye kusimama usiku akawa hakupata kitu zaidi ya kukesha na kujitaabisha,” (An Nasai)

Maneno ya Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) yanaone- sha kuwa hawa ni watu ambao maten- do yao yamekosa ikhlas au utendaji unaokwenda sambamba na muktad- ha wa sharia, bali wanafanya matendo yao kimazoea na kufuata mkumbo.

Ni muhimu sana kutambua nafasi ya ikhlas katika matendo ili yaweze kuwa na thamani mbele ya Allah.

2. Kufunga siku ya shaka

Miongoni mwa makosa wanayoya- fanya watu ni kufunga siku ya shaka (siku ya mwezi 30 Shaaban). Hutokea baadhi ya watu wakaifunga siku hii kutokana na hatihati ya kuwa ndani ya Ramadhani, na hili ni kosa kwa mael- ezo ya wanazuoni, kutokana na maka- tazo ya Mtume.

Ibnu Umar (Allah amridhie yeye na baba yake) amesema, Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) amese- ma: “Mwezi ni siku 29 msifunge mpa- ka muuone (mwandamo) pakiwa na mawingu juu yenu basi kamilisheni idadi ya siku 30,” (Bukhari).

Pia amesema: “Fungeni kwa kuuo- na na fungueni kwa kuuona pakiwa na mawingu juu yenu kamilisheni idadi ya idadi ya Shaabani siku 30,” (Bukhari).Imamu Bukhari amepokea Hadithi

kutoka kwa Abu Huraira (Allah amri- dhie), Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema: “Asiitan- gulie Ramadhani mmoja wenu kwa funga ya siku moja au mbili isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga funga yake basi na afunge siku hiyo,” (Bukhari).

Katika Hadithi hizi kuna makatazo ya wazi juu ya kufunga siku ya shaka. Hata hivyo, kwa yule ambaye huwa ana kawaida ya kufunga funga za sun- na kama vile Jumatatu na Alhamisi, ikasadifu siku hiyo, anaweza kuende- lea na funga yake.

Lakini kwa yule ambaye anabahati- sha kuwa huenda ikawa ni siku ya kwanza ya Mwezi wa Ramadhani, na akaamua kuifunga, huyu atakuwa amefanya makosa.

3. Kutolala na nia katka funga ya faradhi

Katika makosa yanayofanyika ni kutolala na nia katika funga ya faradhi, hili ni miongoni mwa makosa wanay- oyafanya watu wengi pale wanapoacha kuhudhurisha nia zao katika kipindi kilichopo kati ya kuzama jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri.

Imepokewa Hadithi katika Sunan kutoka kwa Hafsa (Allah amridhie) kuwa Mtume (rehema na amani za Al- lah zimshukie) amesema: Asiyekusan- ya funga kabla ya Alfajiri hana funga.” (Tirmidhiy na Abu Daud). Katika ri- waya nyingine ya Nasai: “Asiyeilaza nia tangu usiku hana funga.” Pia katika ri- waya nyingine: “Hakuna funga kwa yule asiyeilaza nia tangu usiku,” (Abu Daud na Tirmidhiy).

Hadithi hizi zinatuhimiza kuikusu- dia funga ya faradhi tangu usiku kabla ya kuchomoza Alfajiri.

Nia ni jambo lililopo moyoni na hupatikana kwa makusudio ya ndani ya moyo tu kuwa Allah akipenda kesho utafunga au kwa kufanya jambo lolote litakaloonesha kuwa una dhamira ya kufunga kama vile kula daku.

Wala kunuwia si kama walivyozoea watu wengi kuhudhuria msikitini na kunuwizana kwa sauti baada ya swala ya isha. Hili ni kosa jingine la kiuzushi, na ni jambo ambalo halina mashiko katika dini, si katika Kitabu wala Sun- na wala katika mwenendo wa wema waliotangulia.

Amesema Shaykhul-Islamu Ibnu Taymiyya: “Mahala pa nia ni moyoni kwa makubaliano ya wanazuoni wa Kiislamu katika ibada zote, twahara, swala, funga, zaka, hijja na nyinginezo,” (Taz: ‘Majmuatur Rasaail Al-kubraa’).

Pia amesema Ibnu Qayyim (Allah amrehemu) “Hakika Mtume (rehema na amani za Allah zimshukie) na Mas- wahaba wake hawakuwa wakitamka nia, wala halikuhifadhiwa kwao hilo. Kama lingekuwa ni jambo la kisheria

Allah angelibainisha kupitia kwa Mtume. Kisha, hamna haja ya kutam- ka nia kwani Allah anaijua (anajua kile alichokusudia mja),” (Taz: ‘Zaadul Ma’ad’)

Kauli ya wanawazuoni wengi wak- iwemo Imamu Shafi, Abu Hanifa na ni moja kati ya mapokezi yaliyopokewa kwa Ahmad inazungumzia ulazima wa kuilaza nia kila siku, nayo ndiyo kauliyenyenguvu. Hatahivyo,Imamu Malik, Zufar na kauli mojawapo ya Ahmad inaonesha kuwa inatosheleza nia moja tu kwa mwezi mzima. Lakini kauli ya kwanza ndiyo yenye nguvu za- idi.

4. Kutowashajiisha watoto kufunga

Baadhi ya wazazi wanapuuza suala la kuwahimiza watoto kufunga, na wakati mwingine mtoto mwenyewe huwa na hamasa ya kufunga lakini mzazi anamzuilia kwa madai kuwa hawezi kufunga,.

Jambo hili ni kinyume na utaratibu wa wema waliopita kama anavy- osimulia Rubayyi’I bint Mu’awidh kuwa walikuwa wakiwafungiza wato- to na kuwaandalia michezo, mmoja wao akililia chakula hupewa kitu cha kuchezea mpaka unafika wakati wa kufuturu, (Muslim).

Amesema Ibnu Hajar (Allah amre- hemu), katika ‘Fat-hul Baariy’, Hadithi hii kuna hoja ya kisheria ya kuwazoe- sha watoto kufunga kwani aliye katika umri huo si wajibu kwake kufunga bali hufanywa hilo kwa ajili ya malezi. Ni lazima kuwapa mazoezi watoto waweze kuzoea ibada mbalimbali tan- gu utotoni mwao.

5. Kufunga kuwa sababu ya uvivu na kutofanya kazi

Hutokea mfanyakazi akasimama kufanya kazi yake, mwanafunzi akaacha kujibidiisha katika masomo, wafanyabiashara wakafunga maeneo ya biashara zao wakati wa mchana na kusababisha baadhi ya mahitaji muhimu katika maisha kuwa vigumu kupatikana. Ukiulizia sababu ya yote hayawatuhujibukuwatumefunga,kwa hiyo baadhi ya mambo hatuwezi kuyafanya.

Je, funga ndiyo inayosababisha uvi- vu na kutofanya kazi? Yapo matukio mengi magumu na mazito ambayo yalifanyika katika Mwezi wa Ramad- hani, Vita vya badri, kukombolewa mji wa Makka, kufunguliwa kwa Andalus pamoja na mengine mengi yalitokea katika Mwezi wa Ramadhani.

Ukifuatilia historia utaona kuwa Waislamu walishinda mapambano dhidi ya maadui wa Uislamu katika Mwezi wa Ramadhani. Hili inaonesha kuwa Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kujitahidi katika kila jambo – ikiwemo ibada na kazi.

Ramadhani ni mwezi wa kuhudhu- ria katika vikazi vya elimu, kisimamo cha usiku, kusoma Qur’an na kutafuta riziki.

Kinyume na hali ilivyo sasa hivi watu wameifanya funga kuwa sababu ya uvivu, wakilala mchana kutwa na kujishughulisha na mambo yasiy- okuwa na tija. Kuufanya Mwezi wa Ramadhani kuwa ni mwezi wa ku- punguza uzalishaji na juhudi katika mambo mbalimbali ni kinyume na malengo. Inatakiwa aendelee na mai- sha ya kawaida hata anapokuwa na hisia ya njaa na kiu kutokana na swau.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close