Uncategorized

Al-Mahdiy wa Sunni ni tofauti na Mahdiy wa Shia

SEHEMU YA 6 Katika toleo lililopita nilielezea upotoshaji wa gazeti Mizani na wasena wao wa Taasisi ya Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania pale waliponukuu kiulaghai nusu ya maelezo yaliyo kwenye, ‘Mizanul I’tidaali fin Naqdir Rijaal’ na kutoa tafsiri za kejeli kwenye baadhi ya istilahi za kiHadithi zilizotajwa na Imam Ad Dhahabiy (Allah amrehemu), gazeti Mizani pia limethubutu kuidhoofisha Ha- dithi tuliyoitaja bila ya kufuata vigezo vya fani ya Jarhu na Ta’adiyl, sanjari na hilo wameacha kwa makusudi kulitafsiri hitimisho adhimu la maelezo ya Imamu Ad Dhahabiy (Allah amrehemu) na ambalo ndiyo mhimili na hukumu ya Hadithi za A’swim bin Abi An-Najud Al-Kuufiy kwa mujibu wa vigezo na istilahi za elimu ya JarhunaTa’adiylkwaMasunni. Sasaendelea

Kama Masunni, nasaba ka-mili ya Al-Mahdiy tulishaitaja siku nyingi kwa kunukuu Ha- dithi na kuitolea maelezo kuto- ka kwa wanazuoni wetu kad- haa wa Kisunni walioonesha uwepo wa tofauti ya kiitikadi kati ya makundi mawili haya ya Sunni na Shia. Aidha wanazuoni wetu wa Kisunni katika maelezo yao walimkana hadharani Al-Mah- diy wa Kishia, ambaye ni Mu- hammad bin Hasan Al-Askariy mzaliwa wa Samuraa, Iraq tan- gu mwezi 15 Shaabani mwaka 255 Hijiriyya (sawa na mwaka 868 Miladiyya) na kutokomea wakujuako Shia wenyewe. Na waheshimiwa wanazuoni wetu wa Kisunni tuliowataja walimthibitisha Al-Mahdiy wa Kisunni, Muhammad bin Ab- dillah ambaye hajazaliwa, na kututajia nasaba yake atakapo- zaliwa mpaka kwa Mtume (re- hema na amani ya Allah iwe juu yake). Ndugu msomaji, kumbuka; hapa tunamjadili Al-Mahdiy kwa mujibu wa itikadi ya Ahlus Sunnat wal-Jama’ah, (ambaye ni Muhammad bin Abdillah), na upande wa pili wa Mizani wanamjadili Al-Mahdiy kwa mujibu wa dini yao ya Shia Im- amiyya (ambaye ni Muham- mad bin Hasan Al-Askariy). Hivyo basi, tarajia kuona to- fauti ya kimtazamo, vitabu re- jea na hata tafsiri za nukuu mbalimbali zinazotolewa kuto- ka pande hizi. Sambamba na hilo, nikuku- mbushe tena kuwa hili ni suala la kiitikadi na Masunni kote ul- imwenguni hawathibitishi masuala ya kiitikadi kama hili na mengineyo kwa kutumia Hadithi dhaifu na zisizokidhi vigezo. Katika jitihada zao za kuta- ka kuipandikiza itikadi yao ya maimamu 12 wanaodai ni watwaharifu/wasiokosea kupitia gazeti lao Mizani, Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania wamekuwa wanatumia mbinu mbalimbali zenye lengo la ku- wababaisha na kuwasahauli- sha wasomaji na wafuatiliaji wa mjadala huu kiini cha mjadala na kutaka kunihami- sha katika mjadala kwa kun- ielekezea binafsi lugha za ku- hamakisha na kukirihisha kwa kudhani nitahamaki au nita- toka kwenye mada na kuacha kuibanisha itikadi sahihi ya Ahlus Sunnat wal-Jama’h kuhusu Al-Mahdiy. Ndugu msomaji, mara kad- haa tumekuwa tukinukuu ma- jina ya vitabu, waandishi, na kurasa zilizoeleza jina na nasa- ba ya Al-Mahdiy, lakini yaone- sha hawa jamaa wa gazeti Mi- zani na Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania, pamoja na kuwa na ajenda yao ya siri katika hili, wana silka ya uba- baishaji na ni watu wenye matatizo ya uelewa au kujitia kutoelewa. Kila tulipowatajia nukuu na hoja zilizo wazi kutoka kwenye vitabu vya wanazuoni wetu wa Kisunni vioneshavyo tofauti ya wazi kati ya Al-Mahdiy kwa maoni na imani ya Shia am- baye ni (Muhammad bin Has- an Al-Askariy), na yule wa Sunni ambaye ni (Muhammad bin Abdillah).Shia hawa wa Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania na gazeti lao Mizani wamekuwa wakiwabeza wanazuoni hao kwa misamiati waijuayo wao, ili kuwashawishi wasomaji waamini;Al-Mahdiyanayehu- biriwa na gazeti Mizani mwenye lakabu ya Al-Mahdiy Al-Muntadhar anayeoana na imani ya Shia Imamiyya, eti ndiye huyo huyo aliye kwenye vitabu vya Masunni. Dai am- balo si sahihi na linapingwa na wanazuoni wa Kisuni.Ni nani A’swim bin Abi An Najud Al-Kuufiy? Wiki hii nitajikita katika kumtambulisha A’swim bin Abi An-Najud kwa kutaja jina na wasifu wake. Kama lilivyoe- lezwa na Al-Imamul Qari-i Abu Bakri Al-Asadiy ni kwamba Jina la Abi An-Najud ni Bahdalah, na (ipo kauli) inayoeleza Bahdalah ni jina la mama yake. Na Abi An Najud ni kuniya yake. Na unaweza ukamwita An-Nujud (kwa Dhwammah) au An- Najud (kwa fat-ha). Huyu, An-Nujud, ni mmoja wa wanazuoni wa mji wa Kufa aliyesoma kwa Abi Abdir Rah- man As Sulamiy na Zirr ibn Hubeysh, na alipokea kutoka kwao. Na alipokea pia kwa Waail na Mus’ab ibn Sa’d na kundi kubwa la watu. Na alikuwa bingwa wa Qiraat (vi- somo vya Qur’an) kwenye mji wa Kufa. Imam Ahmad anasema: “A’swim alikuwa mtu mwema, na Bahdalah ni baba yake”. Abu Zur’ah na kundi kubwa wa- nasema: “Ni mtu thiqah (ana- yeaminika), na kwenye kisomo alikuwa ni mtu thabtun (yaani makini), ama kwenye daraja za Hadithi, Hadithi zake ni Hasa- nun.” A’swim alikufa kati ya mwaka 127, sawa na mwaka 745 Miladiyya au 128 au 129 Hijiriyya, (Al-waafi bil-wa-fayaat 5/318, na wafayaatul Ayaan 3/9)

Na ukisoma kwenye encyclopedia ya majina inayoitwa “Al-a’laam” ya Az-Zirakliy kuna maelezo yafuatayo:”Aswim bin Abi An-Najud Bahdalah, ni mtu wa kufa, na ni mtwana wa Banii Al-Asad, jina lake ni Abu Bakri, ni Taabi’y (yaani ni mwanafunzi wa swahaba) na mmoja wa wasomi saba (wa Qur’an).

Alikuwa thiqah katika Qiraat na ni swaduuqun katika Ha- dithi,” (3/248). Tanbih: Maana ya Swadu- qun: KiHadithi, ni mtu zinazo- andikwa Hadithi zake na kutu- mika baada ya kuchunguzwa. Maelezo ya Al-imam Ad Dhahabiy: Wiki iliyopita tulinukuu ubabaishaji uliofanywa na Abu Dharr Muslim Mission of Tan- zania na kukuletea maelezo ka- mili ya Al-Imam Ad Dhahabiy (Allah amrehemu) kuhusu wasifu wa A’swim aliposema: “A’swim bin Abi An Najud ni mmoja wa wasomaji saba wa visomo (vya Qur’an), Naye ni A’swim bin Bahdalah Al-Kuufiy – ni Mtwana wa Baniy Al-Asad. “Ni thabtu” katika visomo vya Qur’an. Na katika Hadithi, daraja yake ipo chini ya thabtu ni ‘Swaduuqun yahim’. Yahya Al- Qattwan akasema: “Sijamkuta mtu mwenye jina la A’swim isipokuwa hakuwa na hifdhi nzuri”. Na Imam An Nasai anasema: “Hakuwa Haafidh”. Na Imam Ad Daraqutniy anasema: “Kwenye hifdh ya A’swim kuna kitu”. Na Abu Hatim anasema: “Mahali pake (ni daraja la) swidq”. Na Ibn Khirrash anase- ma: “Hadithi yake ni Nakrah”. Ad Dhahabiy mwenyewe akasema: “Huwa Hasanul Hadiyth”. Na Ahmad na Abu Zur’ah wanasema “Thiqah” alikufa mwaka 127. Na Al-im- am Ad Dhahabiy akatamatisha kwa kusema: “Mimi ninasema: Bukhari na Muslim wame- pokea kutoka kwake kwa kui- fanyia majumuisho na mapokezi mengine na si kwa mapokezi aliyoyapokea peke yake,” (Mizaanul I’tidaal 2/357). Uchambuzi na ufafanuzi Maelezo yangu kuhusu uchambuzi na ufafanuzi wa Al-Imam Ad Dhahabiy ni kwamba uchambuzi wake unaashiria kuwa iwapo kama riwaya za A’swim ibn Abi An-Najud zi- tapokewa kwa njia moja pekee, hapo ndipo riwaya za A’swim zitakuwa na walakini kiHa- dithi, lakini kama imepokewa kwa njia zaidi ya moja, hapo ri- waya zake hupanda daraja kutoka katika udhaifu na kuwa ‘Hadithun Hasanun’. Mfano wa hilo ni haditihi il- iyopokewa na Abdullahi bin Masoud (Allah amridhie) al- ipoeleza kuwa Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake) alisema: “Lau haitosalia dunia isipokuwa siku moja, Allah atairefusha siku hiyo mpaka (kwanza) amteue mtu atokae Nami, jina lake litaafiki jina langu na jina la baba yake litaafiki jina la baba yangu, ata- jaza uadilifu duniani kama ili- vyokuwa imejazwa dhuluma”. Hadithi hii imepokewa na Imam Abu Daud As Sijistaniy kwenye Sunan yake (Hadithi Namba: 4282, Imam At Tirmi- dhiy kwenye Sunan yake (Ha- dithi Namba: 2231), Na akase- ma ni Hadithun Hasanun Swa- hih. Na Imam Ibn Al-Qayyim ameuashiria usahihi wake kwenye Al-Manarul Munif uk 84, na imesahihishwa pia na Sheikhul Islam ibn Taymiyah kwenye Minhajus Sunnah 4/211. Maelezo ya makala hii yanaonesha ulaghai wa Shia wa Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania na wasena wao wa gazeti Mizani wa kuzipinga Hadithi zisizounga mkono itikadi zao za Kishia, na kujas- iri kuzidhoofisha na kuziporo- mosha kama walivyotaka ku- fanya kwenye Hadithi hii thabiti ya Mtume (rehema na amani ya Allah iwe juu yake), kwa kufuata utashi wa nafsi pasipo kufuata misingi ya kusa- hihisha au kudhoofisha Ha- dithi kwa Manhaj/mfumo wa wanazuoni wa Kisuni, na kudai eti Hadithi tajwa haina mashiko kwa kuunukuu kila- ghai wasifu (biography) ya A’swim bin Abi An-Najud Al- Kuufiy tofauti na ulivyoelezwa na Al-Imam Ad Dhahabiy kwenye kitabu ‘Mizanul I’tidaali fin Naqdir Rijaal’. Kwa taarifa ya gazeti Mizani na wasena wao wa Abu Dharr Muslim Mission of Tanzania. Elimu ya ‘Jar-hu na Ta’adiyl’ ni fani inayojitosheleza, na wana- zuoni wa Kisunni wana tarati- bu zao katika fani hizi za elimu ya Hadithi ambazo kwa kutu- mia kanuni zake huweza kuitoa Hadithi katika udhaifu na kui- pandisha daraja, hata kama kwenye sanad/mlolongo wa wapokezi wake kuna mtu aliye- fanyiwa ‘Jarhu’ yaani aliyetiwa dosari. Hivyo, tunawashauri waji- funze utamaduni wa kusoma na kunakili kikamilifu kutoka katika vitabu asili vya wana- zuoni wa Kisunni na si kulish- wa maelezo nusunusu kutoka kwa walionukuu kama wafan- yavyo kwenye mjadala huu. Itaendelea InshaAllah

 

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close