Uncategorized

Kwa heri Ramadhan, Karibu ucha Mungu

Kichwa cha habari cha makala yangu ki- nakaribiana na maneno yaliyosemwa na mwandishi Harith Ghasani katika kita- bu chake maarufu alichokiita, ‘Kwa heri ukol- oni kwa heri uhuru.’ Nimeona niyatumie maneno kama hayo kwa kuwa yanasadifu zaidi kwenye hali zetu sisi Waislamu wa umma huu, hususan katika msimu tuliou- maliza wa Ramadhani. Katika kalenda ya Ki- islamu, Ramadhani ni mwezi wa tisa, na wasifu wa mwezi huu upo tofauti kidogo kwa sababu kuu mbili. Moja ni kwamba wenyewe haukutajwa katika ile miezi mitukufu am- bayo Qur’an imeitaja.

“Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika huku- mu ya Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mi- takatifu. Hiyo ndiyo dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu,” (Qur’an, 9:36)

Miezi hiyo mitukufu ni kama ifuatavyo, Muharram, Dhulqa’ada, Dhulhijja na Rajab. Ukiitazama orodha hiyo Mwezi wa Ramad- hani hauukuti.

Kiufupi ukisema miezi mitukufu basi ndanimwe Mwezi wa Ramadhani haupo la- kini ukisema mwezi mtukufu basi unakuwa ni Mwezi wa Ramadhani pekee ndiyo unata- jwa. Pili, Mwezi wa Ramadhani ndiyo mwezi pekee uliotajwa kwa jina lake ndani ya Qur’an wakati miezi mingine haikutajwa kimajina ndani ya Qur’an.

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeterem- shwa humo Qur’an kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na up- ambanuzi. Basi atayekuwa mjini katika mwezi huu na afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu ka- tika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anaku- takieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mum- tukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa ame- kuongoeni ili mpate kushukuru,” (Quran, 2:185).

Utukufu ama ukubwa wa mwezi huu ni kwa sababu yapo mambo makubwa ambayo yametokea, likiwemo tukio la kuanza kushu- ka ndani yake Qur’an Tukufu. Sasa kimsingi Ramadhani huwa inakuja na kuondoka, ujio wake huleta kitu fulani na kuondoka kwake ni kuacha athari ya hicho kitu.

Sasa tukiwa katika hatua za kuhitimisha mwezi huu mara nyingi mambo ya wanada- mu hutengemaa mwisho ama huharibika mwisho. Kwa msingi huo, Mtume akaambi- wa ya kwamba; “Mwisho ni bora kuliko mwanzo,” Haimaanishi uanze vibaya lakini inasisitizwa uwe makini katika kuhitimisha kila unalolifanya, kama alivyosisitiza Mtume kwa kusema: “Mambo huzingatiwa mwisho wake,”

Hii unaweza kuithibitisha hata katika maisha yetu ya kila siku. Mathalani, unaweza ukawa umeandaa hafla ya chakula, ukichun- guza vizuri nidhamu huharibika punde tu watu wakimaliza chakula, huo ni mfano mmoja na ipo mingi kama hiyo.

Ramadhani inaondoka lakini jambo la maana inatuachaje au inatuachia nini. Kile kinachoachwa ndiyo nataka pia nikieleze namna ya kukienzi.

‘Karibu uchaMungu’ ndiyo slogani/kauli mbinu inapaswa wawe nayo Waislamu na wanadamu kiujumla, na bila ya kuukaribisha uchaMungu hatuwezi kujisifu kwa kingine chochote. Allah Ta’ala katika kuwatazama wanadamu kwa ubora wao hatazami rangi, jinsia wala utajiri bali anatazama uchaMun- gukamakigezochaubora wamtu.

Neno uchaMungu (Taqwa) limetokana na neno WAQAA likimaanisha kukinga ama kulinda au kuhifadhi, pia humaanisha kuwe- ka kizuizi, ama ngao baina ya mtu na cho- chote kingine.

Kwa hiyo tukisema kumcha Allah au ku-muogopa Allah (IT-TAQI-LLAH) Inamaan- isha kuweka kizuizi baina ya ghadhabu za Mungu Muumba na mwanadamu na hiyo ndiyo husemwa kuwa ndiyo uchaMungu, ki-wango cha uchaMungu hupimwa kwa ile ta-hadhari anayoichukua mja dhidi ya aliyemu- umba. Neno hili limetajwa ndani ya Qur’an takriban mara 258, sawa iwe kwa jina tabia ama kitendo. Kwa uwingi huo unaweza kuo- nanamnauchaMungulilivyojambomuhimu sana. Tukitazama kwa mtazamo mwingine, tu- naona kuwa analotaka Allah kwa waja wake ni kwamba wewe, mimi ama yeye tunatakiwa tuwe pale ambapo Allah akitutaka tuwe basi atukute pale anapopataka na wala asitukute asipopataka iwe asubuhi, mchana ama jioni. Kwa msingi huo ndiyo kila pahala ambapo Allah anaeleza jambo zito basi hulishikimani- sha ama huliambatanisha na uchaMungu tutataja mifano michache ya mambo makubwa ambayo Allah ameyashikamani- sha na uchaMungu. Suala la riba ni jambo zito lililofananishwa na kupigana na Allah. Allah Ta’ala anaeleza katika Qur’an: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkipofanya ji- tangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulu- miwe,” (Qur’an, 2:278-279). Jambo lingine lililoambatanishwa na uchaMungu ni talaka kwa uzito na ugumu wake ambao huleta athari mbaya kwa baadhi ya wanajamii. Allah amesema: “Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wape- ni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. “Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasi- toke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mi- paka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulu- mu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mun- gu ataleta jambo jingine baada ya haya. “Basi wanapofikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikieni nao kwa wema.Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu.Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya mwenyezi Mungu.Hivyo ndivyo anavyoagizwa anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kuto- kea. Na humruzuku kwa jiha asiyotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye hum- tosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake. “Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wa- nawake wenu, ikiwa mnayoshaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpa- ka watakapozaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi,” (Qur’an, 65:1-4) Ukitazama katika Aya hizo nne Allah ameweka neno uchaMungu. Hii ni kwa uzito wa mambo anayoyasema. Suala lingine ambalo linachukiza kwa wan- adamu kwa hivyo kuwa linachukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni suala la kusengenya nalo Allah akaliambatisha na uchaMungu. “Enyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyin- gi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu,” (Qur’an, 49:12) Suala la mwisho kwa makala yetu ya leo ni hili tulilonalo na suala la ibada hii ya swaumu ya Ramadhani, kwa uzito na ugumu wake na muda mrefu ambao mja anajizuia Allah Ta’ala akalihusisha na uchaMungu. “Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchaMungu,” (Quran, 2:183).Kwa kuhitimisha tuseme TMuabudu Mola wako hata baada ya Ramadhani umeshauaga Mwezi Mtuku- na ya akhera kwani wachaMun- Muislamu kufungua ukurasa mingine zaidi ya ilivyokuwa ka- mambo mema tuliyokuwa tuki- fu wa Ramadhani, na kwa gu ndiyo wenye kufaulu kama mpya wa kuimarisha uhusiano tika Mwezi wa Ramadhani. Hii yatenda ndani ya Ramadhani. hakika amefaulu aliyejitahi- anavyobainisha: “Hakika wach- mwema na Mola wake, familia, ni kwa sababu Mwenyezi Mun- Hali halisi ni kwamba, uhuishaji di katika kutenda kheri ndani ya mwezi huo, na amepata hasara aliyeipuuza funga na kufanya uvivu katika kutekeleza ibada mbalimbali. Allah Ta’ala anaitaja hatua ya uchaMungu kama zao la mja kuiwajibikia ibada ya funga kikamilifu. Allah analibainisha hilo pale anaposema: “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa funga, kama wal- ivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu,” (Qur’an, 2: 183). Mbali na uchaMungu, pia msingi mwingine wa funga ni Allah Ta’ala kututaka tuyafun- gamanishe maisha ya kidunia aMungu wanastahiki kufuzu,” (Qur’an,78:31). Kwa mujibu wa Aya hizi, ni dhahiri kila Muislamu aliyeidir- iki swaumu ya Ramadhani atakuwa amehitimu mafunzo na kutunukiwa shahada ya juu ya somo la uchaMungu. Lililo muhimu ni kuifanyia kazi sha- hada hiyo kwa kuendelea kufan- ya mema kama ilivyokuwa wakati wa Ramadhani. Ili kutimiza wajibu huo ipasavyo, ni jukumu la kila jamii nzima na kuhakikisha anadumu na hali hiyo hadi mwisho wa maisha yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuusia kwa kusema: “Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie yakini (hadi yakufikie mauti),” (Qur’an, 15:99). Aya hii ni dalili tosha inayohimiza juu ya wajibu wa kudumisha ibada, iwe ni ndani au nje ya Ramadhani. Ili kupata tija, tunapaswa kuwa waja bora katika miezi gu anapenda vitendo vya mwa- nadamu anavyoviendeleza japo ni kidogo, kuliko vitendo vingi asivyoviendeleza. Hili linathibi- tishwa na kauli ya Mtume (Re- hema na amani ya Allah zimfik- ie) pale aliposema: “Vitendo anavyovipenda Allah Ta’ala zaidi (kuliko vyote) ni vile vinavyodu- mishwa japokuwa ni vidogo,” (Bukhari na Muslim). Katika hali ya kujitathmini, inafaa kutafakari ni kwa kiasi gani tumejiandaa na kuhuisha wake ni mdogo kwani baadhi yetu tayari tulishaziacha ibada hata kabla ya kumalizika kwa Ramadhani. Ni jambo la aibu kwa Muisla- mu kudumu na ibada ndani ya Ramadhani kisha kuzitaliki ka- tika miezi mingine, na katika hili inatupasa kumuonea haya Allah Ta’ala kwa kutambua ku- wepo kwake siku zote, na siyo ndani ya mwezi mmoja peke yake. Tunamuomba Allah Ta’ala atukubalie swaumu zetu na atu- lipe yaliyo mema, atusamehe madhambi yetu, pia atujaalie kudumu na ibada yake hadi mwisho wa umri wetu. hUTolewa na KUchaPIShwa, The Islamic Foundation, P.o. box 6011 Morogoro, Tanzania, e-mail: imaanmedia3@gmail.com, chUMba cha habaRI: 0652 777 969 aFISa MaSoKo: 0785 500 502, ToVUTI: www.islamicftz.org Kwa heri Ramadhan, Karibu ucha Mungu yUSUPh aMIn naSaha za wIKI Tuendeleze somo la kusamehe, kuvumilia tulilolipata ndani ya Ramadhani Kwa hakika ngao pekee inayoweza kum- kinga muumini kutokana na dosari za kibinadamu ni kutubia makosa pamo- ja na kukithirisha ‘Istighfaar’ yaani ku- muomba msamaha Mwenyezi Mungu. Mwezi wa Ramadhani ni fursa muhimu ya kutekeleza amali hizi kikamilifu. Pamoja na umuhimu huo, bado mion- goni mwetu hatuna utayari wa kuitekeleza ibada hii kutokana na kuipa thamani ndo- go, na ndio maana kila mwaka tunafunga lakini hatuoni matunda ya funga. Kadhalika, baadhi yetu tumekuwa wa- tenda maovu huku tukiwa wazito wa kutu- bia kwa matumaini kuwa, Allah ni mwingi wa kusamehe hivyo hakuna shaka atatuse- mehe. Hii ni itikadi potofu na yenye kuan- gamiza ambayo Muislamu hapaswi kuwa nayo. Jambo muhimu kwa muumini ni kui- wajibikia ibada ya Allah Ta’ala sanjari na kuomba msamaha kadiri awezavyo.Mja anaposhikamana na jambo hili Mwenyezi Mungu humbadilishia madhambi yake na kuwa thawabu. Hii ni kwa kauli yake Allah Ta’ala pale anaposema: “Isipokuwa atakayetubu na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha mao- vu yao yawe mema.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe, mwenye kurehemu,” (Qur’an, 25:70). Pamoja na faida hii, bado kuna baadhi ya Waislamu ambao katu hawaoni umuhimu wa kuomba msamaha. Huu ni utovu wa nidhamu na ni katika alama ya mtu kuwa na kiburi na majivuno. Si hivyo tu, bali kitendo hiki cha kuto- jishughulisha na kumtaka Allah msamaha ndio chanzo cha wanadamu wengi kuugua maradhi ya nafsi hivyo kuathiri mahusiano ya kibinadamu hususan linapokuja suala la kuombana msahama. Kwa mfano, wapo wanaodiriki kusema: “Katu siwezi kukusamehe, na hata ni- kikusamehe siwezi kukusahau,” Vilevile wapo wanaofikia muafaka kwa kuwaambia waliowakosea: “Tufanye yameisha,” hali ya kuwa bado wana vifundo kwenye nyoyo zao. Katika hili, tunapaswa kutambua kuwa, wanadamu ni viumbe waliokadiriwa na Al- lah Ta’ala upungufu mwingi wa kimaumbile likiwemo suala la kukoseana, hivyo kitendo cha mtu kukataa kusamehe baada ya kuom- bwa msamaha hakikubaliki katika dini. Pia kufanya hivyo kunapingana na asili ya maumbile ya mwanadamu ambayo ni kukosea, na kwa msingi huo, tunalazimika kusameheana kwa sababu hatukuitwa wa- nadamu ila kwa kuwa na sifa ya kukosea. Kwa maana nyingine kuvunja kanuni ya msamaha ni sawa na kuvunja kanuni ya maisha, na ndio maana nasema, tunawa- jibika kujifunza kusamehe.Kushindwa ku- litekeleza hili ni kujivisha kiburi ambacho kwa hakika si katika sifa za muumini. Imesimuliwa Hadithul Qudsiy kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) ya kwamba, Mwenyezi Mungu anasema:“Kiburi ni (mfano wa) vazi langu la chini, na utukufu ni (mfano wa) vazi langu la juu atakaye ( jaribu) kuninya’nganya moja kati ya hizo, nitamtupa motoni na wala sija- li,” (Muslim). kutokusamehe ni kikwazo Bila shaka wengi tunapenda kustawisha imani zetu lakini jitihada hizo zinashindwa kuzaa matunda kwa sababu ya kuto- kusamehe. Wengi pia tuna shida mbalim- bali ambazo kwazo tunamuomba Allah la- kini hatupati majibu. Hii ni kwa sababu kutokusamehe ni kikwazo na kizuizi kikubwa kinachosimama baina ya mtu na majibu ya maombi yake kwa Allah Ta’ala. Utakubaliana nami kwamba, samahani ni neno dogo ambalo lau jamii ya wanada- mu wangezingatia umuhimu wake lingewe- za kusaidia kuokoa maelfu ya watu kuanga- mia, kuimarisha undugu na umoja pamoja na kuepusha chuki na visasi baina ya wana- jamii. Ukweli ni kwamba wengi hatutaki ku- waomba msamaha wale tunaowakosea kwa sababu ya kuhisi kudharaulika au kuoneka- na duni mbele yao jambo linalopelekea mi- farakano na chuki kati ya mkosa na aliyeko- sewa. Hapa inafaa kujiuliza ni kwa nini Wais- lamu wanafikia hatua ya kuchukiana na ku- hasimiana eti kwa sababu tu ya tofauti zao za kimitazamo ya kifiqhi. Siyo hao tu lakini pia wapo waliochupa mipaka ambao kufarakana kwao, kuna- tokana na ushabiki wa timu za mpira pamo- ja na vyama vya siasa. Hali hii imekuwa iki- sababisha maafa makubwa kiasi cha baadhi yetu kushindwa kusemezana, kusaidiana na hata kuzikana. Ni dhahiri makosa tunayomfanyia Allah Ta’ala ni makubwa zaidi ukilinganisha na yale tunayotendeana baina yetu. Pamoja na ukubwa huo, bado Allah huyasamehe huku akiendeleza mapenzi yake kwetu kama ana- vyosema: “Nae (Allah) ni mwenye kusame- he, mwenye mapenzi,” (Qur’an, 85:14). Ikiwa ukweli ni huo basi tujiulize swali hili: Ni kwa nini tunashindwa kusamehe makosa madogo madogo na wakati huo tu- natamani kusamehewa na Mwenyezi Mun- gu madhambi yetu makubwa makubwa? Katika hali ya kutusahihisha, Allah ali- yetukuka anatuzindua akisema: “Na wasamehe, na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mun- gu ni Mwingi wa msamaha (na) mwingi wa rehema. (Basi nyinyi sifikeni kwa sifa hizi),” (Qur’an, 24:22). kwa maoni wasiliana ya kwamba maisha ya thamani kwa mwanadamu ni mai- sha ya kiuchaMungu. Bila kumchaMungu maisha yetu yanakosa thamani bora kwa kuwa ustawi wetu utakuwa ni ustawi wa bandia.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close