Tujikumbushe

Maisha na Itikadi ya Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab

SEHEMU YA 6Wiki iliyopita, tuliona wasifu wa Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab na jinsi alvyojipamba na haiba ya kuhuisha Sunna na kurejesha Tawhid.. Sasa endelea…

Muhammad bin Abdulwahhab kama ‘Mujaddid’

Mujaddid katika katika dini ni mtu aliyekuja kurejesha upya dini kuwa kama vile ilivyokuwa zama za Mtume na Maswahaba. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) kwamba Mtume wa Allah (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) alisema: “Hakika Allah hutuma kwa ajili ya umati huu katika mwanzo wa kila miaka mia moja mtu atakayeifanya upya dini yake (umati huu),” (Abu Daud). Hapana shaka kwamba Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) alikuwa mmoja wa ‘Mujaddiduuna’ hao yaani maulamaa waliokuja kuuhusisha Uislamu sahihi alioufundisha Mtume (rehema na amani ya Allah ziwe juu yake). Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah marehemu) aliacha athari ya aina yake dunia nzima. Uhusishaji alioufanya Sheikh bin Abdulwahhab ulikuwa umejikita katika imani thabiti juu ya kupwekeka kwa Allah yaani tawhid iliy o j e n g w a k at i k a m a p e n z i makubwa ya kumpenda Mjumbe wa Allah (rehema na amani ziwe juu yake) na Sunna zake. Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab aliianza da’wah yake baada tu ya kupata elimu sahihi juu ya Uislamu na kuielewa jamii ya wakati huo ya Waislamu ilikuwa imekosea wapi kuhusu Tawhid na Sunna. Aliujenga uhuishaji wake kutokana na mtazamo sahihi wa Uislamu akijumuisha kusahihisha itikadi (aqidah) potofu kwanza kabla ya kingine chochote. Kwa hiyo aliianza da’wah yake kwa kile ambacho Mtume wa Allah (rehma na amani ya Allah ziwe juu yake) alianza nacho – Tawhid. Kwa hiyo sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) aliitazama Aqiidah kama kitovu cha da’wah yake na akawafundisha watu itikadi sahihi kwa mujbu wa Qur’an na Sunna. Kwa hiyo da’wah yake ikawa tofauti na maulamaa wengi wa zama zake ambao walijikita katika falsafa na itikadi za kimapokeo zisizo sahihi kiasi cha kuzama katika shirki na bid’a mbali mbali. Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) akapata mafanikio makubwa kwa rehma ya Allah Ta’ala. Moja ya sababu za mafanikio makubwa aliyoyapata sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) ni kuielekeza da’wah yake kwa viongozi (watawala) wa watu akijua kwamba watu hufuata viongozi wao. Sheikh alimwendea mtawala Muhammad bin Saud ambaye alikubali da’wah yake na kuona hitajio la kuuhusisha Uislamu kama mfumo wa maisha ya mwanadamu. Matokeo yake, watu waliokuwa chini ya Ibn Saud wakafuata msimamo wa kiongozi wao. Kwa kuwa Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) alijua kwamba kuwa na wafuasi mbumbumbu wanaomfuata tu kibubusa ni kikwazo kwa da’wah yake, alitumia muda wake mwingi kufundisha watu ili waujue Uislamu sahihi na wawe watetezi madhubuti wa itikadi ya Uislamu. Kama Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah ziwe juu yake) alivyofanya, Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) hakutumia upanga kueneza itikadi ya Tawhid na Sunna kama propaganda za maadui wa da’wah yake wanavyodai. Ilipobidi kupigana, ilikuwa ni kujitetea yeye na wafuasi wake dhidi ya uadui mkubwa ulioelekezwa kwake na wafuasi wake kutoka kwa wapinzani wa da’wah yake. Njia kubwa aliyoitumia ni kuwatuma wanafunzi wake na barua alizoandika yeye mwenyewe kwa mkono wake kwenda kwa watawala wa makabila mbali mbali na kwa wanawazuoni akiwafahamisha kwamba hakuja kuleta dini mpya wala kueneza uzushi (bida) na kwamba alikuwa Muislamu mwenye kushikaman ana kitabu cha Allah na Sunnah za Mtume wake (rehma na amani ziwe juu yake). Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) aliuhubiri Uislamu ule ule uliohubiriwa na kufundishwa na wema waliotangulia (Salafu Swalih). Sheikh alipigana na wale wote waliopania kuzuia kuenea kwa da’wah hii tukufu na llah akampa ushindi dhidi ya maadui zake. Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) aliwaonya Waislamu kwamba kubaki kwao nyuma ni matokeo tu ya wao wenyewe kuyaacha mafundisho sahihi ya Uislamu. Aliongeza kusema kwamba maendeleo ya kweli ni kwa kushikamana na Uislamu sahihi pekee. Ni kweli kabisa, Uislamu uliletwa kwa watu mabedui wasiostaarabika na ukawafanya watu walioendelea na kustaarabika, waliokuwa masikini wakawa matajiri, waliokuwa wanyonge wakawa watukufu na wenye kuheshimika na kuogopwa na maadui zao. Kabla ya Uislamu aliokuja nao Mtume Muhammad kuwafikia, watu walikuwa mbali na mafundisho sahihi ya Uislamu Allah akawaongoa, walikuwa wamegawanyika vipande vipande Allah akawaunganisha, walikuwa wasio na elimu Allah akawafanya watu wenye elimu ya dini na dunia. Walikuwa wamezama katika giza la imani potofu na ibada za kishirikina. Walifungika na matendo ya kishirikina na itikadi za kisufi. Kwa rehema za Allah, Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) akaibuka mshindi na ushirikina na bid’a vikafutika katika eneo la Hijaz na kuenea da’wah ya Kisalafi duniani kote ambayo lengo ni kuhuisha Tawhid na Sunna na kupiga vita shirki na bid’a. Kama watawala wote wa Kiislamu wangeipokea da’wah ya Sheikh Muhammad bin Abdulwahaab (Allah amrehemu) kama alivyofanya Muhammad bin Saud, hali ya Uislamu duniani leo ingekuwa bora sana na historia ingegeuza mkondo wake. Sifa zote anastahiki Allah Ta’ala kwani da’wah ya sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) haikufa kwa kifo chake. Kizazi cha Sheikh Ibn Abdulwahhab kiliendeleza kazi y a k e k w a s u b r a n a h e k m a kubwa hadi sasa da’wah yake imefika d u n i a n i kote. Itaendelea Insha-Allah

 

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close