Tujikumbushe

Kuelimisha vijana kuipenda nchi na thamani ya uzalendo

Mwanadamu huzaliwa huku akiwa mzalendo na mpenda nchi yake. Kwenye hili la uzalendo, watu wa jinsia zote hushiriki, hata wale wenye mitazamo tofauti. Ulipokuja Uislamu ambayo ni dini ya kimaumbile, haikusimama upande wa uelewa huu tu, bali dini hii pia ilimsisitizia Muislamu na umuhimu wa kuipenda nchi yake.

Muislamu anatakiwa kuhakikisha ana uakisi upendo huu wa nchi kwenye nyendo zake zote. Qur’an Tukufu imethibitisha kuwepo kwa kanuni ya kuipenda nchi kwa kuilinganisha uzalendo wa kuipenda nchi na maisha.
Mwenyezi Mungu anasema:

Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingelifanya hayo ila wachach tu miongoni mwao. Na lau kama wangelifanya waliowaidhiwa ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi. Na hapo tunge wapa malipo makubwa kutoka kwetu. Na tungeliwaongoa Njia iliyo nyooka.”
[Qur’an 4: 66-68]

Ni jukumu letu kujikumbusha jinsi Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie), alivyokuwa anaupenda mji wa Makka. Mtume alikuwa anausemeza wakati anahama na kuelekea Madina. Alisimama na kuuambia kwa neno la kuaga nakusisimua:

Mji mzuri uliyoje, ni mji kipenzi kwangu, lau si watu wako kunitoa ndanimo, nisingekwenda kuishi kwingine.” [Tirmidhiy]

Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) kwenye hadithi hii tukufu, anatangaza upendo wake kwa Makka. Huo ni mji mtukufu mji uliobarikiwa, mji ambao Mtume ameuishi akiwa mtoto, kijana, na hata akiwa mtu mzima.Kwa leo ndio inatambulika kama taifa, na hili si geni kwenye umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia binadamu.

Kimaumbile, binadamu huupenda ule mji aliozaliwa, kukulia, na kuishi, kwani kunako mji huo kuna wazazi, ndugu, jamaa, dada, kaka, wapenzi, kumbukumbu za maeneo yake ya mchezo enzi za utoto na hata ujana wake. Binadamu ametumia heri za taifa na kuvuta hewa yake, kunywa maji yake, na kwa mantiki hii ndio mtu hujikuta anaupenda mji na nchi yake hata anaposafiri na kuwa mbali na mji wake. Pia, imedhihirika wazi kuwa, kuipenda nchi ni suala linalohimizwa na Uislamu.

Ni lazima tuwalee wenetu kuipenda nchi walizozaliwa na kukulia, na waiweke mbele ya macho yao hadithi ya Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) ambayo inamuunganisha kimwili Muislamu na mji wake. Na hakuna mtu mwenye akili timamu anayepinga suala la kuipenda nchi kuwa ni uzalendo wa kipekee, hisia za aina yake, na kujitolea. Uzalendo si mavazi, lugha, uraia, kanuni, au rangi inayopakwa usoni, uzalendo ni zaidi ya hivyo. Uzalendo ni upendo wa hali ya juu. Inawezekana tukaupenyeza
kwenye mioyo ya watoto wetu kupitia:

Kwanza, kuwaunganisha wananchi na dini yao, na kuwakuza kwa misingi ya Kiislamu. Pia, yafaa kuliunganisha hilo na utambulisho wao wa kitaifa, na kujenga msingi wa uzalendo na kuipenda nchi tokea umri wa utoto. Hilo, litawezekana kwa njia ya kuimarisha hisia za uzalendo na kufanya kazi kwa ajili ya kujipatia maendeleo.

Pia, hilo litawezekana kwa kujiandaa kufanya kazi, kujihudumia, kujiondolea madhara, kutunza mtu anavyovipata, kuimarisha dhana ya utii kwa wazazi na
watawala kwa watoto, na kujiepusha na kila kinachoweza kuchochea mizozo na chokochoko. Katika hili, yafaa tuzingatie kauli yake Mwenyezi Mungu:

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.”
[Qur’an 4:59]

Pili, itawezekana kupenyeza uzalendo kwa kuwaandaa vijana wawe tayari kuchukua elimu kutoka kwa wanazuoni wa kweli na waadilifu wa nchini, anasema AsShatwibiy: “Bidaa ya kwanza kwa jamii na ikhtilafu inayokosolewa ni ile inayopelekea migawanyiko na kuwagawa watu makundi kwa makundi, kukua kwa tatizo la kutoelewana wenyewe kwa wenyewe, mtu kujiona ni mwanazuoni na mujtahidi katika dini, wakati hajafikia daraja hiyo na mtu kuhesabu mtazamo wake kuwa ndio mtazamo, na kinyume na hiyo ni rai yake ni upinzani.”

Tatu, uzalendo unaweza kupenyezwa kwa kuwazoesha watu kuwa na tahara ya kimaadili, kuilinda nafsi, familia na nchi na maradhi ya kijamii, na tabia mbaya, na kuwahimiza wajipembe na tabia za Muislamu muerevu anayeijua dini na dunia yake.

Nne, uzalendo unaweza kupenyezwa kwa kuwazoesha watu kuheshimu sheria zinazojenga nchi, kulinda haki za wananchi wenzao na kusimamia mambo yao, na kuwahimiza kuzingatia mfumo, kuheshimu kazi na kuboresha tabia na maadili, kuwalea kuwapenda wengine na kuwatendea wema, na kuwajengea upendo wa kujitolea na kutatua shida za wengine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufuatilia maslahi yao kwa inavyowezekana.

Mwisho, inalazimu tuhimize suala la kuipenda nchi kwa vijana, kwa njia ya kukuza uzalendo, kwani familia itaulizwa, jamii itaulizwa, sekta za elimu itaulizwa kuhusu suala hili la kusisitiza upendo kwenye nyoyo za watoto wetu na wanafunzi, na kuwahimiza uzalendo wa
taifa, na hii itawezekana kwa njia ya
mrejesho mwema.

Taifa limetufanyia mengi. Hivyo basi! Nasi tunatakiwa tutimize mazuri kwa ajili ya taifa, kwani wema kwa wema, na hili ndilo tulilohimizwa na dini yetu ya kiislamu, na hili huwezekana kwa njia ya kuthamini na kutunza mali za taifa, kwa kulinda samani na zana
maalum za kujifunzia.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close