Tujikumbushe

Cassini (satelaiti) ‘itastaafishwa’ leo

Hii ni picha iliyochukuliwa na satellite ya NASA ya Cassini, wakati ambao satellite hiyo ilikuwa inaizunguka Saturn, ikiwa kilomita 1,200,000,000 mbali na Dunia.

Unaweza kuona kwa uwazi pete za Saturn. Na hapo, upande ama ubavu wa nyuma, umbali wa kilomita bilioni 1.2 mbali, kuna mithili ya kidoti kidogo cha bluu, kilichooneshwa na huo mshale , Hiyo ndio sayari yetu ya dunia. Maisha yako yote, na yangu, na kila mtu ambaye umepata kukutana naye, au kumsikia, au kusoma kuhusu mtu huyo, ameishi kwenye hicho kidoti cha bluu.

“Hii ndio uumbaji wa Mwenyezi Mungu! Basi nionesheni, ni kitu gani walichokiumba hao mnaonishirikisha nao?” [Luqman: 11]

“Hakika, uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa (miujiza) kuliko uumbaji wa watu, lakini wengi miongoni mwa watu hawaelewi” [Ghafir: 57].

“Yeye ndiye aliyeumba mbingu saba katika safu, huwezi kuona uharibifu wowote katika uumbaji wa al-Rahman!” Angalia tena – unaona kosa lolote? Na uendelee kuangalia, mara kwa mara … hakika macho yako yatachoka baada ya kujinyenyekeza (kwasababu ya kutoona kasoro/uharibifu katika uumbaji huo).Na kwa kweli tumeifanya anga ya chini iwe ni yenye kuwa na mapambo yake (yaani, sayari na nyota) … “ [al-Mulk: 3-6].

PS. Cassini (satelaiti) ‘itastaafishwa’ leo, na kuangukia katika sayari ya Saturn. Ilizinduliwa(satelaiti ya cassini) kutoka duniani mnamo mwaka 1997, na kufikia sayari ya Saturn miaka saba baadaye, mwaka 2004.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close