1. Habari1. TIF News

Uzinduzi wa Msikiti Al Gafar

WAISLAMU wametakiwa kutokutumia Misikiti kama sehemu yakutangazia biashara zao na matangazo mengine mbalimbali suala ambalo sio mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehma na Amani iwe juu yake) na badala yake itumike katika mambo ya ibada.

Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Mikidadi Lipena wakati wa Khutba yake akiwahutubia waumini katika Msikiti wa Al Ghafar uliopo katika kijiji cha Changarawe kilichopo kata ya Mzumbe wilayani Mvomero.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Sheikh Ibrahim Twaha alichukua nafasi nakuzungumza na waumini hao wakati wa uzinduzi wa Msikiti huo mpya na wakisasa ambao umejengwa na Taasisi ya The Islamic Foundation huku akiitaja mikakati na mipango ya TIF katika utendaji wa sera zake za utoaji wa misaada kama hiyo kwa waumini ama wananchi

Hata hivyo Sheikh Omar Ally ambaye ni Mkuu wa Idara wa Ujenzi wa TIF amewataka waumini wa eneo hilo kuutumia msikiti huo kwa lengo lililokusudiwa.

Ismail Abdallah mdau wa kamati ya Msikiti huo ameeleza malengo waliyokuwa nayo katika juhudi zao za kuendeleza maendeleo mbalimbali yatakayo leta tija kwa waumini na viongozi wa msikiti.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close