1. TIF News

Shule za sekondari Forest Hill, Imaan kuungana

TAASISI ya The Islamic Foundation (TIF) imeziunganisha Shule ya Sekondari ya Imaan na Shule ya Sekondari ya Forest Hill ili kukuza viwango vya taaluma katika shule hizo. Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Imaan katika ukumbi wa Shule ya Forest Hill.

Nahdi alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Bodi ya Shule ya Forest Hill kuomba uongozi wa taasisi ya TIF kuinganisha shule hiyo na Shule ya Imaan, ambazo zote zinamilikiwa na taasisi hiyo.

“Ni muda mrefu tumepokea maombi kutoka kwa Bodi ya Shule ya Forest Hill ya kuunganisha shule hiyo na Shule ya Imaan, sasa leo tumewaita wazazi ili tuwaambie jambo hili ili nanyi mtoe maoni yenu”, alisema Nahdi.

Nahdi alisema kuwa watawapunguzia wazazi wa Shule ya Imaan gharama za vitu mbalimbali, ikiwemo ada pamoja na kutoa usafiri bure kwa wanafunzi wa bweni.

“Pia, tunampango wa kutengeneza mabweni katika shule hii ya Forest kwani tuna eneo kubwa ambalo litasaidia kujengwa kwa mabweni hayo,” Alisema Mwenyekiti huyo.

Nae, Gavana wa Shule ya Imaan, Khamis AlJabr, amewataka wazazi kushirikiana na walimu katika kusima mia maadili, kutokana na muungano wa shule hizo, ili kuimarisha maadili ya Kiislamu katika shule hizo Hali kadhalika, wazazi wa Shule ya Imaan wamepongeza hatua hiyo na kuongeza kuwa itasaidia kuboresha viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close