2. Taifa

Tabia Zetu Ziakisi Ujumbe wa Qur’an!

“Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (swaumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu,” (Qur’an, 2:183).

Tupo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Nimweziuliochaguli- wa na Allah ‘Azza wa Jalla’ kama mwezi wa kufunga. Mwenyezi Mungu ameupendelea mwezi huu kuliko miezi mingine yote kwa kuu- fanya kuwa mwezi wa rehema na toba kwa waumini wote. Hakika Ramadhani ndiyo mwezi mkuu ku- liko yote! Mwezi ambao Allah ‘Azza wa Jalla’ alianza kushusha ujumbe wake wa mwisho kwa wanadamu – Qur’an. Ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ra- madhani, tunasoma Qur’an kila siku na tunaisoma kwa kirefu wakati wa Tarawehe. Lakini tunaelewa na kuitekeleza Qur’an hii? Aisha (Allah amridhie) amemueleza Mtume (re- hema na amani ya Allah zimshukie) kuwa tabia yake ilikuwa kama Qur’an inayotembea. Je, tabia zetu zinaakisi ujumbe wa Qur’an? Tun- aitekeleza Qur’an katika maisha yetu? Tunahisi ujumbe wake juu ya mabega yetu? Allah ‘Azza wa Jalla’ anasema: “Lau kama tungeiteremsha hii Qur’an juu ya mlima, ungeliuona ukinyenyekea na kusambaratika kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi Mungu. Nahiinimifanotunawapi- gia watu ili wafikiri,” (Qur’an, 59:21). Mwenyezi Mungu Mtukufu ana- wafunulia wanadamu kwamba kama angeiteremsha hii Qur’an juu ya mlima, ambao ni mkubwa na madhubuti mara nyingi zaidi ya mwanadamu,basiungesambaratika kwa hofu ya Mwenyezi Mungu! Je? Katika miili yetu hii dhaifu, tunahisi unyenyekevu wa Qur’an, ambayo imeteremshwa kwetu na siyo mili- mani? Je? Tunaishi kwa kuzingatia maamrisho na makatazo yake, am- bayo Allah ‘Azza wa Jalla’ ameyawe- ka ndani ya Qur’an, ujumbe wake wa mwisho? Kwa rehema za Mwenyezi Mun- gu, tumeiona Ramadhani ya mwaka huu, lakini je tutakuwa hai kuiona Ramadhani ijayo? Je, hii ndiyo itakuwa fursa yetu ya mwisho kuon- ja rehema za Allah Ta’ala Aliyetuku- ka,ndaniyamwezihuuuliobariki- wa? Lazima tutathmini mwenendo na vitendo vyetu na kisha tuakisi, iwapo siku tutakayokutana na Mola wetu, itakuwa bora kwetu au itakuwa balaa? Kila mmoja wetu atakutana na Allah ‘Azza wa Jalla’ peke yake, bila ya wazazi wa kutu- linda wala mali ya kutunusuru. Mwenyezi Mungu ametufunulia: “Siku ambayo mtu atamkimbia ndu- guye, Na mamaye na babaye, Na mkewe na wanawe, Kila mtu mion- goni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha,” (Qur’an, 80:34- 37).Tutakuwa na amali zetu tu katika maisha haya. Hebu tuangalie nyu-ma mwaka uliopita na tuakisi. Tuan- galie yale tuliyofanya kwa usahihi kwa mujibu wa Uislamu ili tuen- delee kuyafanya, na tuangalie yapi tulikosea ili tumuombe Mwenyezi Mungu msamaha na tujitahidi tu- sirudie tena. Mtume (rehema na amani ya Al- lah zimshukie) amesema: “Ramad- hani inapokuja, milango ya Pepo in- afunguliwa na milango ya moto in- afungwa, nashetanianafungwa minyororo,” (Bukhari na Muslim). Kwa kuzingatia Hadithi hii, wa- nazuoni wanasema kwamba Pepo inafungua milango yake na moto nafunga milango yake na shetani anatiwa nyororo! Kwa hiyo adui pe- kee anayebaki wa kukabiliana naye ni nafsi zetu. Basi tuitumie fursa hii ambayo shetani ametiwa pingu kukabili nafsi zetu na tujizoeshe kumtii Mwenyezi Mungu katika mwenendo wetu wote wa maisha bila kuacha kipengele hata kimoja. Tukiwa msikitini, shuleni, madrasa, nyum- baniaukazinibasitumtiiAllah‘Azza wa Jalla’. Hata tukiwa tunanunua nyumba au kuuza gari. Kwa ufupi, tunapaswa kufuata Uislamu katika vipengele vyote vya maisha yetu. Ramadhani pia ni fursa nzuri ya kutafuta maarifa ya Kiislamu na kuongeza ufahamu wetu wa utama- duni wa Kiislamu. Kadri unavyofa- hamu Uislamu ndipo unapokuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuendesha maisha yetu kwa mujibu wa Uisla- mu. Mwenyezi Mungu amefafanua: “Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa wajawakeniwanazuoni.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ngu- vu, Mwenye kusamehe,” (Qur’an, 35:28). Basi tutafute elimu katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma maana za Aya za Qur’an Tukufu. Tusome maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ya Allah zimshukie) na Mas- wahaba wake (Allah awawie radhi). Waliishi vipi maisha yao? Vipi waliji- tolea mali na maisha yao ili kulifanya neno la Mwenyezi Mungu liwe juu? Tumkumbuke Musab bin Umair (Allah amridhie), Swahaba aliye- toka kuwa tajiri mkubwa mpaka akawa masikini kuliko wote. Alikuwa masikini mpaka alipofariki dunia hakuwa na nguo za kutosha kufunikamwiliwake. Kwaninialik- abiliana na hali hiyo? Kwa sababu alitambua kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Tusome kanuni za kuamiliana (interaction) ndani ya Uislamu, iwe kwenye biashara, fedha, kilimo, mazingira na mengineyo. Tuone Uislamu unasema nini kuhusu uhu- siano kati ya mwanaume na mwan- amke, familianawatoto.Uislamuni mfumo kamili wa maisha na katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani tuweke nia ya kujifunza yale maeneo ya Uislamu ambayo hatukuwa na elimu nayo. Ndugu zangu katika Imani, tu- tumie fursa hii kupanua zaidi ma- daraja ya udugu na kujiongezea tha- wabu kwa kuwakaribisha Waislamu wenzetu kwenye futari kama alivy- osema Mtume wa Mwenyezi Mun- gu (rehema na amani ya Allah zimshukie): “Yuleatakayemfuturi- sha mtu aliyefunga atapata malipo yale yale, bila ya kupungua kutoka kwenye malipo ya mtu anayemfu- turisha,” (Ahmad). Mwezi wa Ramadhani wakati wa zama za Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) ulikuwa ni kipindi cha utakaso, kuamrisha mema, kukataza maovu na kujita- hidi kwa hali na mali kulifanya neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu. Baa- da ya kifo cha Mtume, Waislamu waliendeleza Sunna hii na Allah ‘Azza wa Jalla’ aliwatumia waumini kuathiri mkondo wa historia. Ramadhani ilikuwa ni kipindi cha shughuli nyingi, waliutumia mchana kwenye harakati na usiku kwa Swala, huku wakiomba rehema za Mwenyezi Mungu na msamaha wake. HuondiyomsukumowaRa- madhani, ambao uliwawezesha Waislamu wa awali kukabiliana na changamoto ambazo zilionekana haziwezekani. Nduguzangukatikaimani, tui- fanye Ramadhani ya mwaka huu kuwa mwezi wa swala, mwezi wa ibada, mwezi wa kusoma Qur’an, mwezi wa kutoa zaka, mwezi wa kuimarisha uhusiano na jamaa zetu, mwezi wa ukarimu kwa wahitaji na mwezi wa kuchunga kauli na viten- do vyetu. Ramadhani ya mwaka huu uwe mwezi wa kuimarisha mahusiano yetu na Allah ‘Azza wa Jalla’ na kuzi- takasa nyoyo zetu, uwe mwezi wa kuongeza elimu ya Qur’an, Sunna naFiqhi, namweziwakufanyaulin- ganiaji wa kutekeleza Qur’an na Sunna kwenye uso wa ardhi. Mwenyezi Mungu atuweke mion- goni mwa waja wake wema na tu- utekeleze Uislamu kwa wakati wote. “Ewe nafsi iliyotua! Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. Basiingiamiongoni mwa waja wangu, Na ingia katika Pepo yangu,” (Qur’an, 89:27-30).

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close