1. TIF News2. Taifa

Mashindano ya Qur’an ya afrika yatia fora Dar

Katika kuonesha mapenzi yao na Kitabu Kitukufu cha Allah, Qu’ani, maelfu ya watu walihudhuria Ju- mapilihiikwenyemashindanoya Kimataifayauso- maji Qur’ani kwa ghaibu yaliofanyika uwanja wa Taifa ji- jini Dar es Salaam.

Uwanja huo unaochukuwa watu takribani 60,000, ulifurika na hivyo watu wengi zaidi kulazimika kubaki nje. Hali hiyo ilimlazimu Mratibu wa Mashindano hayo, Sheikh Nurdeen Kishki kuomba radhi na kutoa ombi kwa Serikali, la kupatiwa viwanja viwili vya Taifa na Uhu- ru, kwa pamoja, ili kufanyia mashindano hayo hapo mwakani, ombi ambalo lilikubaliwa na mamlaka za Seri- kali pale pale uwanjani, akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi. Mashindano hayo yaliyoratibiwa na Taasisi ya Al-Hikma Foundation chini ya rais wake, Sheikh Abdulqader Al-Ahdal yalikuwa na washiriki 17 kutoka nchi mbali mbali barani Afrika wal- ioshindana katika kiwango cha juzuu 30.

Washiriki hao wa juzuu 30 ni Fahad Sagar Ahmed (Kenya), Issa Aliyu Abdallah (Nigeria), Khalil Mussa Hussein (Tanzania bara), Hanze Ibrahim Sharifu (Dji- bout), Germiston Umar Sithole (Afrika Kusini), Dush- imimana Said Said (Rwanda), Mohammed Sharifdiin (Ghana) na Ahmed Mohammed Moussa (Ethiopia).

Wengine ni Suleiman Ali Mutebi (Uganda), Seif Ra- madhan Zombe (Tanzania bara), Mahamoudou Ali Chanfi (Comoro), Muhammad Abdallah Aden (Soma- lia), Zaid Niyutunga (Burundi), Mohamed Dumapili (DRC Congo), Ismail Issa Qasim (Zanzibar), Ncade Adenge (Msumbiji), na Abdulkareem Ahmed Fariheena (Sudan).

Kijana wa miaka 12 ang’ara

Mshindi wa mashindano hayo alikuwa Muhammad Abdallah Aden mwenye umri wa miaka 12 kutoka nchini Somalia ambaye alikabidhiwa hundi ya 15,750,000/-, Ipad, kompyuta na pia alipewa ofa na kampuni ya Sky Bus Travelling Agent kutembelea nchi yoyote duniani anayoitaka.

Mshindi wa pili alikuwa Abdulkareem Ahmed Fari- heena (22) kutoka nchini Sudan ambaye alikabidhiwa shilingi 11,250,000/- na Ipad huku mshindi wa tatu, Mahmoudou Ali Chanfi kutoka Comoro (18) akijin- yakulia shilingi 6,750,000/- na Ipad.

Mshindi wa nne alikuwa Khalil Mussa Hussein mwenye umri wa miaka 17 kutoka Tanzania ambaye ali- pewa shilingi 3,250,000/- na Ipad na mshindi wa tano alikuwa Ismail Issa Kassim pia akitokea Zanzibar am- baye alikabidhiwa dola 2,250,000 na Ipad.

Mashindano hayo pia yaliwahusisha washindi wen- gine wa juzuu chache ambao walikabidhiwa zawadi mbali mbali.

Kauli ya Waziri Mkuu

Mgeni rasmi katika mashindano hayo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majali- wa alioneshwa kustaajabishwa na umma mkubwa wa Waislamu waliohudhuria na kusema kuwa hiyo ni ishara njema ya mshikamano.

“Nilipoingia hapa, sikuamini macho yangu, kukuta Waislamu mmejaa kwenye viti zaidi ya 60,000, na wen- gine kukosa nafasi, na umma uliobaki nje ni zaidi yenu,

hii inanihakikishia kwamba Waislamu tunao mshikamano,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu aliongeza: “Mashindano haya yanasaidia sana katika kuwajenga vijana waweze kuwa na maisha mema hapa duniani, lakini pia na kesho akhera, Serikali inaamini kuwa vijana waliopata makuzi ya Kiislamu ni msingi mzuri katika kujenga taifa lenye raia wema.”

Waziri Mkuu pia alihimiza kutumika vema kwa uhuru wa dini, na kusema kuwa dini ni kiungo muhimu katika ujenzi wa amani na utulivu.

“Nafasi hizi za dini zote zitumike vizuri, kwa kujenga mshikamano miongoni mwetu, kwa kuunga mkono jitihada za Serikali, ambayo yenyewe inaamini kwamba dini ndio chombo muhimu kitakachoifanya nchi hii iendelee kuwa na utulivu na amani ya kutosha,” alisema Kassim Majaliwa.

Kuhusu watu wanaotumia jina la dini ili kufanya mambo machafu, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ni lazima watu hao wapigwe vita.

“Sote tuungane pamoja kupinga, na kupiga vita wale wen- zetu wachache watakao kuwa wanachafua jina la dini yetu na kuona kwamba dini hii siyo ya fujo, tuungane kupinga wale watu wanaotumia dini hii vibaya,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu alisema ni muhimu mashindano hayo yakapelekwa katika mikoa mingine ikiwemo visiwa vya Zanzibar ili kudumisha Muungano.

Kukosekana kwa Sudeis

Tofauti na ilivyokuwa imetangazwa hapo, Imamu Mkuu wa Misikiti ya Makka na Madina, Abdulrahman Sudeis, hakuweza kuja nchini na kuhudhuria mashindano hayo na badala yake aliwatuma wawakilisha wake. Katika ujumbe huo Imamu Sudeis aliomba radhi kutohudhuria na kusema

kuwa anatumai atafanya hivyo wakati mwingine.
Dosari nyingine ndogo iliyojitokeza ilikuwa ni mkangan- yiko wa majina ya washindi, ambapo awali mshindi wa tatu alitangazwa kuwa ni Seif Ramadhan Zombe, lakini baadae ikadhihirika kuwa mshindi sahihi wa nafasi hiyo alikuwa ni Mahmoudou Ali Chanfi kutoka Comoro ambaye yeye alipati- wa zawadi na GSM Foundation ili aliyetangazwa kimakosa

asirudishe zawadi alizokuwa ameshakabidhiwa.

Zawadi ya Misahafu ya dhahabu

Zawadi ya msahafu ulioandikwa kwa wino wa dhahabu ili- tolewa kwa Waziri Mkuu, na pia kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye pia ni mlezi wa Al – Hikma Foundation, Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammad Gharib Bilal.

Aidha, Vyombo vya Habari vya Imaan vilivyo chini ya taa- sisi ya Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) vilikabidhiwa cheti cha shukrani kwa kuwa sehemu ya wafadhili wa mashindano hayo. Zawadi hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa TIF, Sheikh Muhammad Issa.

Mashindano hayo pia yalihudhuriwa na watu mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Jam- huri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambae ni mlezi wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation.

Baadhi ya watu wengine maarufu waliohudhuria ni pamo- ja na Naibu Waziri wa TAMISEMI. Jafo Suleiman Jafo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) AbdulRah- man Kinana. Wengine ni mabalozi wa nchi mbali mbali, ikiwemo Saudi Arabia, Oman na vilevile wakuu wa taasisi mbalimbali za kidini na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close