1. Habari1. TIF News

Serikali yaahidi kushirikiana na TIF

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) ya mjini Morogoro imemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza- nia Kassim Majaliwa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya utoaji misaada kwa wa- hanga wa mafuriko Pemba na ile ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwezi Septemba, 2016.

Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi alikabidhi ripoti hiyo kwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama am- baye aliyemuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi alisema lengo la taasisi yake ni kuwatumikia Wais- lamu na wasiokuwa Waislamu ili kuchochea maendeleo katika jamii.

Pia, Nahdi alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kutoa msamaha wa kodi katika taasisi yake pale inapoingizamizigombalimbalikwa lengo la kuisaidia jamii yenye watu wenye mahitaji. Naye, Katibu Mkuu wa TIF Sheikh Muhammad Issa, alimuambia Waziri Mhagama kuwa, licha ya kupata mafanikio makubwa katika kuisaidia jamii, TIF imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo

kunyimwa vibali vya kutekeleza shughuli zake za kijamii.

Aidha, alitaja baadhi ya mafani- kio yaliyofikiwa na TIF kuwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ka- tika shule mbalimbali nchini, uch- imbaji wa visima virefu na vifupi katika taasisi za kiserikali ikiwemo shule za serikali na majeshi yak- iwemo ya magereza na polisi.

Kwa upande wake Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na

Walemavu Jenista Mhagama amesema, wizara yake itashirikiana na TIF ili kuboresha huduma za ki- jamii na kuahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu ombi la TIF la kuongeza masafa ya Redio Imaan ili jamii ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu wapate kufaidika na ra- dio hiyo ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhama- sisha jamii kuishi kwa wema na ku- pendana.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close